NIna swali hapa kwa mgombea wa nafasi ya juu kabisa......"Hivi huu uchakachuaji wa rasilimali za Watansanyia hasa Ardhi na Madini utaishi lini"? Ili wananji waweze kufaidika na rasilimali zao na sio hao walitutawala enzi kama wakoloni na leo wanarudi kama wawekezaji. Naomba jibu lenye utekelezaji sitaki longolongo
@ Superman,
IM SORRY CHAIR OWNER!
Hayo ndo maneno sasa! Nimekusamehe Mwanaharakati wetu, sote ni binadamu.
Niliogopa sana na nilijua kinachofuata ungeniambia "akili yangu ndogo" kitu ambacho kingenidhalilisha zaidi.
Sasa umefikia wapi na kamati yako ile ya kwenda China? Au bado umechomoa?
Kuhusu kazi ilipofikia naomba kutoa taarifa ifuatayo:
1. Uteuzi wenye bado haujaeleweka. Naomba uteuzi huu uwe ratified kwanza na Bunge?? au sijui na chombo gani.
2. Wanakamati wenyewe hata siwajui na hatujawahi kuonana.
Superman, naomba uwambie hao walinzi wa mgombea urais wasogee karibu maana ana saumu kali na mda wowote anaweza kuanguka.
Pia naomba nafasi ya kuongea maana naona kuna upendeleo. Mbona mimi nimekaa hapa karibu yako na nimenyoosha mkono mda mrefu hunichagui
Haaa haaa kijana acha lugha ya Kejeli . . .
karibu shika Mic utoe mchango wako sasa. Umechelewa sana kufika Mkutanoni.
Time keeper amekupigia kengele kwa sababu umeanza kuelemea kwenye vyama aka umetoka nje ya mada. Elezea mfumo wa usalama wa taifa unataka uweje katika serikali ijayo.Asante sana mwenyekiti. Mimi hoja yangu ni juu ya hawa jamaa wa usalama wa taifa kujihusisha na siasa. Hii ni hatari sana kwa mstakabali wa taifa. Maana kwa sasa ni wazi kuwa hawa UWT wanawatumikia mafisadi wa CCM. Yaani wamekuwa usalama wa mafisadi na si usalama wa taifa. Uzalendo ni sifuri kabisa. UWT ni kitengo muhimu sana katika taifa lolote lakini kuna upuuzi mwingi sana unaendelea katika idara hii na italigharimu taifa. Nashauri tujadili namna ya kuikarabati hii idara muhimu.
Naona time keeper ananipigia kengele kuwa mda wangu umeisha. Ngoja nirudishe MIC
mkuu KibyNi kama nilikuwa nimesinzia vile kikaoni? ila pointi zote za wadau nimezinyapu. Zinahitaji majumuisho makini. Halafu mimi naingia kwenye mengineyo moja kwa moja. M/kiti ulipotualika mkutanoni uliweka kipaumbele kwa vijana wa jukwaa la mapenzi na ninihii. Naomba utoe ufafanuzi wa ninihii kwanza kabla hatujaendelea. Halafu sijaona mchango wa nafasi ya Mapenzi katika katiba mya ijayo au ni nanihii imewasahaulisha wadau? W/kiti pia nifikishie salamu zanzu kwa wajumbe wote walioitikia mwito wa mwaliko mkutanoni.
Mtanisamehe kujibu kwa niaba yake maana ametokomea kidogoMh.Mwenyekiti mimi nahudhuria lakini natathmini hoja kadhaa halafu nitachangia.
Mkuu mimi napenda kufahamu tumefikia wapi na suala la katibu kabla ya kuendelea kuangusha point halafu zipotee hewani.Naona hawa wamenyoosha mkono haya tunaanza na Ambassador wengine wanafuatia
Sula la afya ya viongozi limejadiliwa na litashughulikiwa. Tutaboresha tume ya uchaguzi kusimamia utekelezaji.Naomba niulize swali, katika katunga katiba mpya je kipengele cha afya za viongozi wetu kitawekwa?
Napendekeza wewe wanafanyiwa Medical check up kabla ya kuchukua form mana wengine sio wazima wanaanguka hovyo hovyo