WOS
mie nimecheka kuliko. ila ndo hivyo tena kama Mwenyewe kasema hizo ni tusiz za nguoni. dawa ni kusema sorry tu kisha tuendelee.
Asante sana mwenyekiti. Mimi hoja yangu ni juu ya hawa jamaa wa usalama wa taifa kujihusisha na siasa. Hii ni hatari sana kwa mstakabali wa taifa. Maana kwa sasa ni wazi kuwa hawa UWT wanawatumikia mafisadi wa CCM. Yaani wamekuwa usalama wa mafisadi na si usalama wa taifa. Uzalendo ni sifuri kabisa. UWT ni kitengo muhimu sana katika taifa lolote lakini kuna upuuzi mwingi sana unaendelea katika idara hii na italigharimu taifa. Nashauri tujadili namna ya kuikarabati hii idara muhimu.
Naona time keeper ananipigia kengele kuwa mda wangu umeisha. Ngoja nirudishe MIC
Tatizo la UwT ni kwamba wanataka wooote waingie ktk madaraka ndo maana wanajikomba kwa mafisadi ili wapate japo mfupa.
Ops mwenyekiti nimedakia hoja hewani
Ni kama nilikuwa nimesinzia vile kikaoni? ila pointi zote za wadau nimezinyapu. Zinahitaji majumuisho makini. Halafu mimi naingia kwenye mengineyo moja kwa moja. M/kiti ulipotualika mkutanoni uliweka kipaumbele kwa vijana wa jukwaa la mapenzi na ninihii. Naomba utoe ufafanuzi wa ninihii kwanza kabla hatujaendelea. Halafu sijaona mchango wa nafasi ya Mapenzi katika katiba mya ijayo au ni nanihii imewasahaulisha wadau? W/kiti pia nifikishie salamu zanzu kwa wajumbe wote walioitikia mwito wa mwaliko mkutanoni.
mkuu Kiby
umenena vyema ila kuhusu suala la mapenzi katika katiba mhhhh!
ngoja tumsubiri mtaalam wa masuala ya katiba atushauri namna ya kuliweka sawa suala hili.
Kuhusu nanihii nadhani akirudi mwenyekiti ataipambanua
Mtanisamehe kujibu kwa niaba yake maana ametokomea kidogo
ila unakaribishwa sana. Uzalendo mbele pia usitumie lugha za kejeli na matusi.
Nashangazwa ulikuwa kimya muda wote huo au weye ndo miongoni mwa waliochelewa?
Tunasubiri maoni na mapendekezo yako mkuu
Sula la afya ya viongozi limejadiliwa na litashughulikiwa. Tutaboresha tume ya uchaguzi kusimamia utekelezaji.
Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi nahisi alipendekezwa Dark City lakini mjadala kutoka kwake kuikataa nafasi hiyo ukawepo mda mrefu.
Labda WOS anajua suala la katibu lipo vipi.
Lakini unaweza kujitolea kuwa katibu maana hata huyu mwenyekiti wetu kajitolea pia.
jamani kuna anayepinga???
Naona kimya chenu kinaashiria tumempata katibu
Hongera Ambassador nakuomba uchukue nafasi yako ya ukatibu.
Turudi ktk mjadala sasa
AGENDA NO:1
AGENDA NO:2
- KATIBA MPYA
AGENDA NO:3
- KUPUNGUZA MAWAZIRI IDADI 20 TUU.
Nawakilisha mheshimiwa mwenyekiti kwa Heshima.
- STOP UNUNUZI WA MASHANGINGI.
.
Sawa mkuu navuta subira. Ila nikunongoneze sikioni kabla ya m/kiti kuja na wala sitaki mjumbe yeyote asikie, ikiletwa hoja ya jinsia moja kuruhusiwa kupumuliana walahi naapa nitapindua meza potelea mbali hata kama mkutano utanikabizi kwa Kova. Unajua mkuu rasilimali watu ni mtaji tosha wa maendeleo kwa taifa makini. Sitavumilia kuona mwendelezo wa uzao ukikomeshwa. NITUNZIE HII SIRI MKUU! SIVYO??
mwenyekiti naomba uniruhusu nitoe mapendekezo kwa ajili ya kikoa kijacho kwani naweza kukosa mda tena
nashukuru wajumbe kwa kutii wito wa huu mkutano kwa vyile ni mara ya kwanza siwezi kuwalaumu ila nawapongeza zaidi ya yote ningependekeza angalau mara mbili kwa mwaka tuwe tunafanya mkutano kama huu online. na minute zitolewa report itumwe bungeni,na jumuia nyingine ambazo tutaziona zinafaa katika mikutano ijayo kuwe kuna daraja kabla post haijawekwa mbele hio itasaidia kuondoa watu wanaofanya joking na kuupuuzia mfano mimi nina changia baada ya kuonana kutuma lakini mwenyekiti na katibu wanazipitia then ndio inawekwa buplic bila kuchujwa kama inaonekana ni mbaya(naamaanisha utani masihara haiendani na mkutano)automatic mnaipeleka kwenye agenda zilizo tupwa kwenye mkutano yaani page nyingine kwa hiyo mtu akilalamika amechangia ila point yake imepuuzwa wajumbe wataiona kwenye page nyingine ila sio hii cream nashukuru wajumbe wote asanteni
Kwanza tunachangia tuuu hata lunch hatupewi ruksa! Sijasikia sitting allowance ni dola ngapi!
Mheshimiwa mwenyekiti natoa hoja