Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Aisee
kweli hiyo inampasa WOS kukuomba radhi walah.
Mwenyekiti rudi kwenye hoja uendeshe kikao
mie naenda kutabaruku kidogo, ugoro unaiita nje

Asante Mwenyekiti Mwenza . . . . Nimekupata . .
 
Aisee
kweli hiyo inampasa WOS kukuomba radhi walah.
Mwenyekiti rudi kwenye hoja uendeshe kikao
mie naenda kutabaruku kidogo, ugoro unaiita nje

Mashallah, nimekusoma Mwenyekiti Mwenza . . . nipo hapa penye kigoda!
 
WOS
mie nimecheka kuliko. ila ndo hivyo tena kama Mwenyewe kasema hizo ni tusiz za nguoni. dawa ni kusema sorry tu kisha tuendelee.

Sasa mimi nifanyeje . . . Mbona hata kile chama cha kijani na njano walisema kuwa chama cha blue na red wamewatukana?

Sasa nyie hamuelewi vipi?

Hata wewe mwenyekiti mwenza hilo linakupa tabu kweli?
 
Asante sana mwenyekiti. Mimi hoja yangu ni juu ya hawa jamaa wa usalama wa taifa kujihusisha na siasa. Hii ni hatari sana kwa mstakabali wa taifa. Maana kwa sasa ni wazi kuwa hawa UWT wanawatumikia mafisadi wa CCM. Yaani wamekuwa usalama wa mafisadi na si usalama wa taifa. Uzalendo ni sifuri kabisa. UWT ni kitengo muhimu sana katika taifa lolote lakini kuna upuuzi mwingi sana unaendelea katika idara hii na italigharimu taifa. Nashauri tujadili namna ya kuikarabati hii idara muhimu.

Naona time keeper ananipigia kengele kuwa mda wangu umeisha. Ngoja nirudishe MIC

Asante sana Kaburunye, hakika suala uliloongelkea ni nyeti sana. UwT ni kama muhimili wa Uzalendo na Utaifa wetu.

Sasa unashauri hili tuliweke vipi? Hebu litolee ufafanuzi wa kina ili lieleweke.
 
Tatizo la UwT ni kwamba wanataka wooote waingie ktk madaraka ndo maana wanajikomba kwa mafisadi ili wapate japo mfupa.
Ops mwenyekiti nimedakia hoja hewani

Ooh! Mwenyekiti Mwenza kuwa huru tu, in fwakti unanisaidia sana na umeonyesha mshikamano wa hali ya juu kuendesha mkutano huu wa wadau wa JF.

Mimi nadhani hili suala itabidi liingie katika katiba ili lisichakachuliwe. kama vipi basi UwT ivunjwe na iundwe upya huku kikiwa ni chombo huru na nidhamu kikijali maslahi ya taifa na bila kujiingiza katika siasa.
 
Msisahau suala la Muungano

Asante Muacici kwa hili, litaingia katika kura ya maoni ya kuangalia muundo gani wa Muungano tunataka.

Hata hivyo kama una maoni ya ziada karibu uyawakilishe!
 
Time keeper amekupigia kengele kwa sababu umeanza kuelemea kwenye vyama aka umetoka nje ya mada. Elezea mfumo wa usalama wa taifa unataka uweje katika serikali ijayo.

Balozi, Excellent! You said it all . . .
 
Ni kama nilikuwa nimesinzia vile kikaoni? ila pointi zote za wadau nimezinyapu. Zinahitaji majumuisho makini. Halafu mimi naingia kwenye mengineyo moja kwa moja. M/kiti ulipotualika mkutanoni uliweka kipaumbele kwa vijana wa jukwaa la mapenzi na ninihii. Naomba utoe ufafanuzi wa ninihii kwanza kabla hatujaendelea. Halafu sijaona mchango wa nafasi ya Mapenzi katika katiba mya ijayo au ni nanihii imewasahaulisha wadau? W/kiti pia nifikishie salamu zanzu kwa wajumbe wote walioitikia mwito wa mwaliko mkutanoni.

Kiby nashukuru sana kwa hoja zako:

Unajua toka tumeanza kikao jinsia ile nyingine walikuwa hawapo. Akaja Mchungaji moja hapa siju ni padre anajiita Rev. Masanilo, akagoma tusianze kikao hadi ile jinsia nyingine iwepo. Sasa maranyingi nawaona kwenye hilo jukwaa ulilosema. Na vijana wote wanashinda huko.

Ndo maana nimweka msisitizo sana waje.

Sasa wale nao wana vipau mbele vyao. Ila sina uhakika kama vipaumbele vya taifa tukivihusisha na mapenzi hatuwezi kuchakachua.

Au wewe unaonaje?
 
mkuu Kiby
umenena vyema ila kuhusu suala la mapenzi katika katiba mhhhh!
ngoja tumsubiri mtaalam wa masuala ya katiba atushauri namna ya kuliweka sawa suala hili.
Kuhusu nanihii nadhani akirudi mwenyekiti ataipambanua

Umenena Mwenyekiti Mwenza!

Tusichakachue katiba yetu na suala la mapenzi. Litaingizwa katika haki za binadamu " Kuwa kila mtu anao uhuru wa kupenda na kupendwa".
 
Mh.Mwenyekiti mimi nahudhuria lakini natathmini hoja kadhaa halafu nitachangia.

Wewe kijana wangu mbona bado huchangii? Nimekuona muda mrefu sana unatuma SMS na kucheza games. Tutafika kweli?

Haya shika Mic sasa utoe maoni yako.
 
Mtanisamehe kujibu kwa niaba yake maana ametokomea kidogo
ila unakaribishwa sana. Uzalendo mbele pia usitumie lugha za kejeli na matusi.
Nashangazwa ulikuwa kimya muda wote huo au weye ndo miongoni mwa waliochelewa?
Tunasubiri maoni na mapendekezo yako mkuu

Huyu Kijana ni Mtanzania kweli? Ni Raia? Mbona jina lake kama si la Kitanzania? Naona kama Mkutano unachakachuliwa! Kama kuna mdau wa Uhamiaji alete data zake hapa. Simwoni tena huyu kijana.
 
Sula la afya ya viongozi limejadiliwa na litashughulikiwa. Tutaboresha tume ya uchaguzi kusimamia utekelezaji.

Umenena vyema. Moja kati ya vigezo na sifa ya mgombea ni kuwa na afya njema na NEC itabidi iwe na 3 independent Doctors wa kupima faya ya Wagombea.

Hili limekaa vizuri. lazima kiongozi awe na afya njema.
 
Mbona sioni hoja nyingi lakini porojo ndiyo nyingi. Mimi vipaumbele vyangu ni;
1 Kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja (Micro economy) Uwezeshaji kwa wanaotaka kujikwamua kimaisha uanzishwe mfuko wa uwezeshaji uchangiwe na wadau ,wananchi, NGO, Serikali na wafadhili usimamiwe na bodi huru ili usitafunwe na wajanja mfuko utoe mikopo na ruzuku kwa wenye kipato kidogo.
2. Kuendeleza elimu ya juu siyo kufuta ujinga, Huduma bora za jamii elimu,afya,nk siyo bora huduma
3. Kuboresha miundombinu
4. Kodi inayotozwa na TRA iangaliwe wanaoumia ni wafanyakazi wafanya biashara hasa wakubwa Mhhh.
5. Utawala bora uboreshwe zaidi Vita ya rushwa iimarishwe na sheria ziwe kali bila kujali ruswha ndogo au kubwa.
Ni hayo tu wakuu
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi nahisi alipendekezwa Dark City lakini mjadala kutoka kwake kuikataa nafasi hiyo ukawepo mda mrefu.
Labda WOS anajua suala la katibu lipo vipi.
Lakini unaweza kujitolea kuwa katibu maana hata huyu mwenyekiti wetu kajitolea pia.

jamani kuna anayepinga???

Naona kimya chenu kinaashiria tumempata katibu

Hongera Ambassador nakuomba uchukue nafasi yako ya ukatibu.
Turudi ktk mjadala sasa

Ambassador asante sana kwa ukubali wako. Karibu Ieleweke kuwa hii ni kazi ya kujitolea na inataka moyo na uzalendo.

karibu katibu

Karibu Balozi
 
AGENDA NO:1

  • KATIBA MPYA
AGENDA NO:2

  • KUPUNGUZA MAWAZIRI IDADI 20 TUU.
AGENDA NO:3

  • STOP UNUNUZI WA MASHANGINGI.
Nawakilisha mheshimiwa mwenyekiti kwa Heshima.

Asante sana. Agenda ya 1 na ya 2 liko ndani ya katiba. Hili la 3 linahusu uadilifu na uongozi bora ikiwa ni pamoja na matumizi mazuri ya rasilimali za taifa.
 
.
Sawa mkuu navuta subira. Ila nikunongoneze sikioni kabla ya m/kiti kuja na wala sitaki mjumbe yeyote asikie, ikiletwa hoja ya jinsia moja kuruhusiwa kupumuliana walahi naapa nitapindua meza potelea mbali hata kama mkutano utanikabizi kwa Kova. Unajua mkuu rasilimali watu ni mtaji tosha wa maendeleo kwa taifa makini. Sitavumilia kuona mwendelezo wa uzao ukikomeshwa. NITUNZIE HII SIRI MKUU! SIVYO??

Kiby; Kiby Kiby! Out . . . . kupumulia ndiyo nini?

Nyie vijana wa lile jukwaa mmeanza . . . Ohooooo, unaona sasa wamekata matangazo TBC?

Kunong'oneza gani huko unaongelea kwenye MIC na mkutano uko live TBC.

Kova ondoka naye huyu . . . .

(Haaa haaa du! Nimecheka sana)
 
Mwenyekiti, actuale can yangu iliisha nimeenda kurefeel (koh koh koh)

Halafu nimeisikiam hoja ya Eeka Mangi ya sitting allowance naomba uitolee tamko maana inahusu,,,,,,

Sasa ambalo ningependa pia tuliweke wazi ni kwamba tuwe na ukomo wa vipindi vya bunge tukirekebisha katibu, mwisho vipindi 2 vya miaka mitano2,,,,
 
mwenyekiti naomba uniruhusu nitoe mapendekezo kwa ajili ya kikoa kijacho kwani naweza kukosa mda tena

nashukuru wajumbe kwa kutii wito wa huu mkutano kwa vyile ni mara ya kwanza siwezi kuwalaumu ila nawapongeza zaidi ya yote ningependekeza angalau mara mbili kwa mwaka tuwe tunafanya mkutano kama huu online. na minute zitolewa report itumwe bungeni,na jumuia nyingine ambazo tutaziona zinafaa katika mikutano ijayo kuwe kuna daraja kabla post haijawekwa mbele hio itasaidia kuondoa watu wanaofanya joking na kuupuuzia mfano mimi nina changia baada ya kuonana kutuma lakini mwenyekiti na katibu wanazipitia then ndio inawekwa buplic bila kuchujwa kama inaonekana ni mbaya(naamaanisha utani masihara haiendani na mkutano)automatic mnaipeleka kwenye agenda zilizo tupwa kwenye mkutano yaani page nyingine kwa hiyo mtu akilalamika amechangia ila point yake imepuuzwa wajumbe wataiona kwenye page nyingine ila sio hii cream nashukuru wajumbe wote asanteni

Mfuatiliaji, asante sana kwa hoja zako nzito. Zote tutaziingiza katika majumuisho.

Na hili la mwisho jinsi ya kuendesha Mkutano wetu, nadhani ni wazo jema sana. Hii ni experience yetu ya kwanza na tunajifunza kutokana na makosa. Itabidi kupitia michango yote na kuiweka vizuri katika majumuisho.

Kwa sasa, sio mbaya sana kuchanganya issues with light jokes, inawafanya wengi wasichoke kusoma.
 
Kwanza tunachangia tuuu hata lunch hatupewi ruksa! Sijasikia sitting allowance ni dola ngapi!
Mheshimiwa mwenyekiti natoa hoja


Du! Hii kali, kweli wewe ni mangi.

Uko wapi Utaifa wako?

U wapi uzalendo wako?

Hatuna bajeti hiyo ndugu. Tuna kazi nzito mbele yetu.
 
Back
Top Bottom