Nilikuwa najaribu kusumbua hili likichwa langu! Nadhani umasikini ni matokeo ya baadhi ya yale niliyoyataja.
1. Katiba: Bila katiba ya maana, chizi anaweza kugeuza bunge lote kuwa Baraza la mawaziri, tutamfanya nini? Na akiamua kujenga Makao makuu ya nchi katika kijiji chake je? Akiamua kila mtu kutoka kwao apatea cheo serikalini je? Akiamua 70% ya budget ya serikali ikanunue vitanda vya mawaziri wake? Akiamua kuwa kila rafiki yake anunuliwe VX na hazina? Na upuuzi mwingine mwingi tu ambao mwisho wa siku unasababisha pesa zisitoshe kwenye huduma za jamii lakini kwa wakubwa vikapu vimejaa.
2. Elimu: bila elimu sisi tunaopepeta midomo tungekuwa wapi? Labda na sisi tungekuwa bado tunawinda digidig (Dik dik).
3. Kilimo: Bila kilimo cha kibiashara na uzalishaji hatuvuki mto mkuu.
4. Miundombinu: Just as an example, ....Hivi nauli ya Arusha Mbeya (about 1200km) ni shilingi ngapi vile? (not more than 30K) na linganisha na Mwanza (about 1300km), ambapo ni karibia 50K na kabla ya barabara kuwa nzuri safari ilichukua karibu 40hrs. Wakati huo mtu keshaenda Mbeya na kurudi A-town.
Hiyo ni mifano tu mkuu,