M/Kiti,
Samahani nimechelewa kwenye mkutano maana kama unavyojua hii nchi yetu usipokuwa dar tum jua uko kwenye unreliable territory ktk intaneti na mambo kama hayo. Nimefika tu na kukuta agizo la mkutano inakwahi huku!
Mkuu mimi priority napendekeza kuwa kama ifuatavyo;
1) Elimu- Mfumo wa elimu ubadilishwe, ubuniwe mfumo utakao endana na hali yetu, na changamoto za soko la ajira duniani. Bado tuna mfumo wa elimu unaopelekea utegemezi wa ajira, ilhali serikali haijawahi na haina mpango wa kubuni ajira kwa wahitimu wetu. Muundo mpya uendane na matayarisho bora ya walimu, mashule, vifaa vya kufundishia. Pia mfumo wa kukopesha elimu ya juu urekebishwe kuwa wa wazi zaidi na wa ki-halisia zaidi.
2) Kilimo- Kwa kuwa toka uhuru kilimo kilikuwa na kimeendela kuwa eneo pekee lenye kuajiri watu wetu kwa zaidi ya 80%, serkali ijayo, kwa makuudi kabisa ifanya mapinduzi ya kilimo ya kweli ili kuboresha kilimo. Hii iendane sambamba na miundo mbinu sehemu za kulima ili kuyapa mazao value badda ya kuvunwa, kuwepo uhuru na uwazi katika soko la mazao, bei za mazao ziwe za uhalisia zaidi. Kwa makusudi kabisa serikali itengeneze mazingira na kuhakikisha mazao yetu yanakuwa processed hapahapa nchini lwa ubora unaokubalika na kuuzwa ndani ili kuondokana na hali ya kuagiza packed food toka nje. Inshallah naamini hili likienda vizuri tutauza nje baada ya kujitosheleza. Haya yafanye kiuhalisia zaidi kuliko KILIMO KWANZA ambayo imekaa kisiasa zaidi.
3) Katiba mpya iandikwe ndani ya mwaka mmoja ili kuleta mfumo mzuri wa kujitawala
Naomba kuwalisha ndugu mwenyekiti.