Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Kapumzike mkuu, this was good. Natumai mchana watakuja wajumbe wengine na michango zaidi. Ila cha msingi huyo DC apitie post zote assumirise points za muhimu ambazo tutazifikisha kwa hiyo serikali itakayoingia madarakani kwa ajili ya utekelezaji.

Kuna DC mwingine unayemzungumzia au Dark City?? Kama ni huyo nadhani hujasoma vizuri posts zake. Kazi njema na Lunch njema pia.
 
Agenda zetu haziangalii chama . . .Agenda zetu zimeegemea zaidi katika kuweka mbele uzalendo wetu na maslahi ya taifa . . .


Its had for you to be objective while your previous/current perception is already known...
 
:confused2: Zamu yangu ishafika? ........................Naendelea kusubiri!
 
Its had for you to be objective while your previous/current perception is already known...

Kijana umeanza lugha ya matusi na isiyo ya kistaa.

Na declare interest mimi si Mwanachama wa CCM, wala CHADEMA wala CUF.

Nasukumwa na dhamira yangu ya Uzalendo na Utaifa tu katika kuleta maendeleo ya kweli ya Nchi yetu.

So nakanusha habari hiyo.
 
Yote aliyopendekeza N-Handsome ni yanazunguka katika suala moja tu nalo ni mabadiliko ya Katiba, hili suala linapaswa kubebwa na vijana wote pasipo kuingiza mapenzi na ushabiki kwa vyama vya siasa. Tukumbuke kuwa TANZANIA NBILA VYAMA VYA SIASA INAWEZEKANA LAKINI VYAMA VY SIASA BILA TANZANIA HAVIWEZEKANI.
 
M/Kiti,

Samahani nimechelewa kwenye mkutano maana kama unavyojua hii nchi yetu usipokuwa dar tum jua uko kwenye unreliable territory ktk intaneti na mambo kama hayo. Nimefika tu na kukuta agizo la mkutano inakwahi huku!

Mkuu mimi priority napendekeza kuwa kama ifuatavyo;

1) Elimu- Mfumo wa elimu ubadilishwe, ubuniwe mfumo utakao endana na hali yetu, na changamoto za soko la ajira duniani. Bado tuna mfumo wa elimu unaopelekea utegemezi wa ajira, ilhali serikali haijawahi na haina mpango wa kubuni ajira kwa wahitimu wetu. Muundo mpya uendane na matayarisho bora ya walimu, mashule, vifaa vya kufundishia. Pia mfumo wa kukopesha elimu ya juu urekebishwe kuwa wa wazi zaidi na wa ki-halisia zaidi.

2) Kilimo- Kwa kuwa toka uhuru kilimo kilikuwa na kimeendela kuwa eneo pekee lenye kuajiri watu wetu kwa zaidi ya 80%, serkali ijayo, kwa makuudi kabisa ifanya mapinduzi ya kilimo ya kweli ili kuboresha kilimo. Hii iendane sambamba na miundo mbinu sehemu za kulima ili kuyapa mazao value badda ya kuvunwa, kuwepo uhuru na uwazi katika soko la mazao, bei za mazao ziwe za uhalisia zaidi. Kwa makusudi kabisa serikali itengeneze mazingira na kuhakikisha mazao yetu yanakuwa processed hapahapa nchini lwa ubora unaokubalika na kuuzwa ndani ili kuondokana na hali ya kuagiza packed food toka nje. Inshallah naamini hili likienda vizuri tutauza nje baada ya kujitosheleza. Haya yafanye kiuhalisia zaidi kuliko KILIMO KWANZA ambayo imekaa kisiasa zaidi.

3) Katiba mpya iandikwe ndani ya mwaka mmoja ili kuleta mfumo mzuri wa kujitawala

Naomba kuwalisha ndugu mwenyekiti.
 
EEE Ndugu munyaaaaaaakiti. Naomba unisamehe babaangu nimechelewa kidoooo kidoko tu msee. Huku kwetu tunatumia fibajaji. lakini hivi tunaambiwa ni fya mama wajawasito hifyo haviendi kwa haraka ndio manake nikachele nikachewa kwa kweli. Yewuuuwi nimesahau nilitaka kusema nini tena mseee! nikumbusheni basi waseee!
 

ASANTE M/kiti kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Angenda Kuu 2010 ambazo chama Kitakachopata ridhaa ya
wananchi kisimamie kikamilifu.
Wakati napita hapa nilisikia swala la elimu likitajwa lakini sidhani kama limepewa msukumo wakutosha. Wizara ya Elimu ina matatizo makubwa ya kubadilisha mfumo wa Elimu ya Tanaznia. Kila siku tuko kwenye majaribio, Ni dhahiri kabisa kuna nchi ambazo zimepiga hatua ya haraka sanaKimaendeleo kwa kuwa na mfumo wa elimu unaoeleweka. Sisi kila siku ni
kubadilisha mifumo, mara futa mashindano ya michezo mashuleni siku mbili tena rudisheni michezo,Mara tena futa Shule za Ufundi Kesho yake tena rudisheni hizo shule Kila siku tunayumbishwa Sababu waziri kashauriwa sijui na haw*** yake,Samahani
M/kiti. Leo hii vijana elimu ya kazi za mikono imeachwa kabisa tunatengeneza Taifa la wakaa vijiweni tu maana hawathamini kazi za mikono. Ukifika vijijini sasa hivi kuna vikongwe tu ndiyo wako mashambani lakini vijana wenye nguvu wako Vijiweni. wanauza Soksi na chupi za kina mama,wengine eti wapiga debe tu hivi hiyo ni akili kweli kuruhusu ajila za kijinga namna hii halafu unasema kifua mbele ajira zimeongezwa, HII NI HALALI KWELI M/KITI, Naomba sana swala la Elimu lisifanyiwe mchezo
hapo tunanyonga Taifa kama Hatuelewi. Samahani M/kiti msg imeingia nipeleke uji wa mama mkwe amejifungua watoto wawili, Thanks
bye baadaye
 
Mwenye kigoda!

Ajenda ya kwanza ni kubadilishwa kabisa kwa katiba!

Ili mawaziri wawe waaajiriwa na watu wote walio chini yao! Kuvunjwe huu utitiri wa miko na visingizio vya kusogeza huduma kwa wananchi.

Local goverments zipewe mamlaka zaidi juu ya uendeshaji wa maeneo yao husika nako huko watendaji wasiwe wanasiasa!

Madaraka ya Rais wa Jamhuriya Muuungano yapunguzwe kwa mujibu wa wakati tulionao sasa!

Ajenda ya Pili ni Elimu;
Isukwe upya muundo wake kwani uliopo sasa umepoteza ubora!

Ajenda ya Tatu ni Kilimo;

Yafanywe mapinduzi ya kweli yatakayomshirikisha zaidi mkulima mwenyewe na si haya ambayo viongozi wanapanga na kuwapelekea wananchi! Hii ikiwa ni pamoja na kusimamia zoezi zima la kurasmisha mali zao kwa uaminifu ili waweze kusaidiwa na misaada inayoelekezwa kwao.
 
Aiseee..Foleni imenisababishiwa nichelewa mkutanoni, sijui nayo niweka katika Agenda la jungu hili. Kiukweli Katiba inatakiwa kufanyiwa kazi upya kabisa na pia umakini katika Separation of Power unahitajika sana kupewa kipaumbele na kupitia kwa umakini zaidi.

Katibu wa mkutano huu pamoja wahusika wote, ni vizuri feedback na majumuhisho ya mkutano huu yatolewa, nina uhakika italeta chachu kwa Taifa.
 
Sijaalikwa
ila naomba kushiriki
Vipaumbele vyetu ni vingi ila msingi wa yote ni udhibiti wa matumizi yalioykithiri ya fedha za UMMA.
hatutaweza kulipa mishahara bora, kujenga miundombinu mizuri wala kuinua kiwango cha elimu iwapo serikali itaendelea kutumbua fedha za umma na rasilimali zetu.

Nitakuja tena...
 
Tuvunje muungano..........wazanzibar warudi kwao tuendelee na mambo yetu kwani tunapoteza muda mwingi kujadili kitu hiki
 
Napendekeza:
" AHADI ZA WAGOMBEA: NI KWA VIPI TUTAPIMA UTEKELEZAJI WAKE UKIZINGATIA TUNAPEWA AHADI MPYA KILA SIKU ILHALI ZA ZAMANI HATA HAZIKUMBUKWI?"

( Inanikumbusha wakati nachumbiwa...ahadi kibaooo! ukishaingia ndani...utakoma kuringa!)
naona unatuchuria sisi wanaume we mwali we.
lakini naunga mkono hoja yako kwamba kabla ya ahadi tutazame zilizotolewa zimetimizwa zipi kwa kiwango kipi ndipo zije ahadi mpya. la sivyo ni uongo uongo tu
Inabidi kuwepo na utaratibu wa kuorodhesha ahadi zote kisha wagombea walioahidi waweke sahihi zao. Kisha tuje tuwabane watakapoingia madarakani! ( Breakthrough thinking lol!)
Nadhani Policy forum wanazo au nenda HAKIELIMU wanavijitabu vya ahadi za watawala na zipi zimetekelezwa.
 
Pamoja na kuwa mratibu wa mkutano huu hanipi nafasi. Naanza kuchangia agenda ya ELIMU. Ndugu wajumbe kwa mtizamo( kama sio mtazamo) Ningependekeza sera ya taifa ya elimu ya Tanzania kwa awmu ijayo iwe ya mfumo wa kuchangamana. Mfano Kijana anayezaliwa kiraracha akasomea shule ya msingi kiraracha, sekondari o na a kiraracha na labda pale chuoni marangu mtoni. Hutegemei mtu kama huyu ataweza kuhimili ushindani wa katika soko la Dunia ya sasa! Nikisema kuchangamana namaanisha kuwa Wasukuma waje shule za kiraracha na wale wa uchagani waende mbeya hali kadhalika. Tuwaandae vijana wa kitanzania kwa ajili ya ushindani na sio kuwaacha kama vifaranga wa kuku wa kienyeji. Nasema hivi kwa sababu naamini kuwa Watanzania wengi tu akili sana tena kuliko, sioni sababu ya kuajiri wakenya kwa kigezo cha kiingereza chao tu! Nilkuwa na wakenya fulani pale Nairobi kipindi fulani, Chuo kizima kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa Tatu hakuna mtu alikuwa anaona WaTZ wamepita wapi. Tulikuwa tunawaacha mbali sana. Walikuwa wanafuatia kwa karibu kidogo ni Wasenegali na Wanigeria. Tatizo la kwetu lilikuwa presentation! Kusimama na kutoa mada was one of the biggest issue for the Tanzanians. Nimetumia 'Was' kwa sababu nji kipindi hicho! Elimu ya Tanzania ianjengwa kudhibiti Mtoto wa Tajiri na Msomi na inamwacha mtoto wa mkulima mbali. Tuangalie ni wangapi wenye uwezo wa kuwalipia watoto wao kwenye shule zenye kufaulisha, St Francis, Maria Goreti, Marian? Nk. Je nikweli kuwa hakuna wenye uwezo kuliko hao wanaosoma huko? Je ni mtoto wa mkulima gani atakayeweza kumlipia mtoto huko? Hata kama atafanikiwa kufaulu mitihani yao? Mto kati ya mtoto wa tajiri/msomi mwenye kipato na Mkulima umezidi kupanuka! Pamoja na sera ya taifa eti kiwango cha chini cha elimu iwe kidato cha sita! (kichekesho)! Mtoto anamaliza F4 ya kata hajui kuandika wala kusoma unataka aendelee hadi F6! Si kwamba hataki kujua ila Manpower hakuna. Waalimu Vodafasta unategemea nini? Unakuta mtoto wa mkubwa mkubwa mbumbu kabisa anapewa material na mtaalam anakwenda! Sisi akina sisi nani anajali! Nafikiri mfumo wa elimu Tanzania unahitaji ukarabati mkubwa.
kama muda unaruhusu mwenyekiti niendelee
 
Yote aliyopendekeza N-Handsome ni yanazunguka katika suala moja tu nalo ni mabadiliko ya Katiba, hili suala linapaswa kubebwa na vijana wote pasipo kuingiza mapenzi na ushabiki kwa vyama vya siasa. Tukumbuke kuwa TANZANIA NBILA VYAMA VYA SIASA INAWEZEKANA LAKINI VYAMA VY SIASA BILA TANZANIA HAVIWEZEKANI.

Sawa vijana, nadhani hili la katiba tumeelewana.

Sasa natoa hoja kuwa, wanaomfahamu Dr. Mvungi wamtafute na wamlete hapa. Yeye na wenzake walifanya kazi kubwa ya kuipitia katiba ya sasa na kuandaa mapendekezo ya katiba Mpya. tumwombe atuapatie soft copy tuipitie hapa.

Nadhani walianza kipindi cha NCCR kabala hata chama cha NCCR Mageuzi hakijazaliwa.

Wangapi wanaunga mkono hoja waseme ndiyo?

Waliosema Ndiyo ni wengi na Wameshinda.

Tafadhali Dr. Mlingi atafutwe huko aliko aje hapa.
 
Back
Top Bottom