Ahsante sana WoS,
You just proved my everlasting respect to you!! Hata hivyo mimi nimedandia gari kwenye mwendo na kwa hiyo naomba mapendezo ya huko nyuma yafanyiwe kazi kwanza.
My respect dada, ...DC
Mhhh,
Balozi, mbona pendekezo lenyewe la awali halijatulia na tayari limewekewa pingamizi?
Nadhani hoja iendelee kama vile DC hajakanyaga humu ndani au unasemaje?
Wana-JF, Wakuu Wote; Viongozi Wote; Vijana Wetu (hasa wale wa jukwaa la mapenzi na mambo ya nanihii . . .)
Itifaki imezingatiwa!
Amandla!
Asalaam Aleykhum!
Bwana Yesu Asifiwe!
Haki Sawa . . .
Kidumu Chama . . .
Power to the . . .
Leo tumekutana hapa, ili kuzungumzia "Agenda Kuu 2010" ambazo wana-JF watapenda chama kitakachoingia madarakani wazisimamie . . . . Agenda zetu zimeegemea zaidi katika kuweka mbele uzalendo wetu na maslahi ya taifa . . .
Lugha ya matusi (LOL), hairuhusiwi, wala kejeli wala kutumia lugha isiyo ya kistaarabu. Mnatakiwa muwe na uvumilivu wa kisiasa.
Pia tusiegemee katika Udini wala Ukabila . . .
Baada ya Mjadala Mzito; Tutakuja na Vipaumbele vyetu vitatu kama "Agenda Kuu 2010".
Kwa maneno hayo machache sasa niwakaribishe ili muweze ku-propose "Agenda Kuu 2010" ambazo hazitafungamana na chama chochote!
Kila mmoja wenu anakaribishwa kushiriki Mkutano Wa Hadhara wa JF:
https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/71880-mkutano-wa-hadhara-wa-wana-jf-%5Bonline%5D.html#post1058999
karibuni sana!
Kuegemea vyama vya siasa inaruhusiwa?
Nimekusoma. Ukipenda toa ufafanuzi zaidi ili umati huu ukuelewe vema.
DC naona kachomoa, labda utumie nguvu ya veto uliyojipatia.Seconded!
Nilikuwa najaribu kusumbua hili likichwa langu! Nadhani umasikini ni matokeo ya baadhi ya yale niliyoyataja.
1. Katiba: Bila katiba ya maana, chizi anaweza kugeuza bunge lote kuwa Baraza la mawaziri, tutamfanya nini? Na akiamua kujenga Makao makuu ya nchi katika kijiji chake je? Akiamua kila mtu kutoka kwao apatea cheo serikalini je? Akiamua 70% ya budget ya serikali ikanunue vitanda vya mawaziri wake? Akiamua kuwa kila rafiki yake anunuliwe VX na hazina? Na upuuzi mwingine mwingi tu ambao mwisho wa siku unasababisha pesa zisitoshe kwenye huduma za jamii lakini kwa wakubwa vikapu vimejaa.
2. Elimu: bila elimu sisi tunaopepeta midomo tungekuwa wapi? Labda na sisi tungekuwa bado tunawinda digidig (Dik dik).
3. Kilimo: Bila kilimo cha kibiashara na uzalishaji hatuvuki mto mkuu.
4. Miundombinu: Just as an example, ....Hivi nauli ya Arusha Mbeya (about 1200km) ni shilingi ngapi vile? (not more than 30K) na linganisha na Mwanza (about 1300km), ambapo ni karibia 50K na kabla ya barabara kuwa nzuri safari ilichukua karibu 40hrs. Wakati huo mtu keshaenda Mbeya na kurudi A-town.
Hiyo ni mifano tu mkuu,
DC hiyo imekubalika. Ila tafadhali jichunge na lugha ya Matusi . . . haaa haaaa
Anayepinga ajitokeze tumsikie... so far DC huna mpinzani na hata mwenyekiti wa muda ambaye naye amependekezwa athibitishwe mmepita bila kupingwa.
Nilikuwa najaribu kusumbua hili likichwa langu! Nadhani umasikini ni matokeo ya baadhi ya yale niliyoyataja.
1. Katiba: Bila katiba ya maana, chizi anaweza kugeuza bunge lote kuwa Baraza la mawaziri, tutamfanya nini? Na akiamua kujenga Makao makuu ya nchi katika kijiji chake je? Akiamua kila mtu kutoka kwao apatea cheo serikalini je? Akiamua 70% ya budget ya serikali ikanunue vitanda vya mawaziri wake? Akiamua kuwa kila rafiki yake anunuliwe VX na hazina? Na upuuzi mwingine mwingi tu ambao mwisho wa siku unasababisha pesa zisitoshe kwenye huduma za jamii lakini kwa wakubwa vikapu vimejaa.
2. Elimu: bila elimu sisi tunaopepeta midomo tungekuwa wapi? Labda na sisi tungekuwa bado tunawinda digidig (Dik dik).
3. Kilimo: Bila kilimo cha kibiashara na uzalishaji hatuvuki mto mkuu.
4. Miundombinu: Just as an example, ....Hivi nauli ya Arusha Mbeya (about 1200km) ni shilingi ngapi vile? (not more than 30K) na linganisha na Mwanza (about 1300km), ambapo ni karibia 50K na kabla ya barabara kuwa nzuri safari ilichukua karibu 40hrs. Wakati huo mtu keshaenda Mbeya na kurudi A-town.
Hiyo ni mifano tu mkuu,
DC naona kachomoa, labda utumie nguvu ya veto uliyojipatia.
Mkuu inapofika kwenye fund ndo ngoma inanoga. Andika neno "JF Uchaguzi 2010" tuma kwa SMS kwenda namba 15010. Utakuwa umechangia sh 1,000.00. Nadhani hii inafaa.Haaa haaa Viscious Cyle Mkuu . . . Mfuko maalumu si inabidi uchangiwe kwa harambee? ama?
Mhhh mkuu, na wewe umeuvaa mkenge wa WoS?
WoS, pendekezo lako ni hatari sana. Tafsiri yake kwangu ni kama vile linalenga kukata kidomo domo. Ukijifanya kuongea sana tutakuita hapa mbele uanzishe wimbo (kama ilivyokuwa kule JKT). Please acha mjadala usonge mbele.
Nitarudi kabla ya Lunch, ngoja nikapeleke mzigo wa bwana anayeniweka mjini!! Si unajua tena, mwendo wetu ni... "punda afe mzigo wa bwana ufike salama"!!
Mbona unamuadress WoS ukinitazama mimi mkuu?Haaa haaa WoS hueleweki kabisa.
Nilikuteua wewe kwa kutumia Veto ukachomoa na kunisindikiza na matusi Kibao ya kawaida na ya nguoni. Cha ajabu umati wote wanakushangilia tu.
Nimewaambia TBC wakatishe matangazo hawataki
Kova nimemwambia akutoe na kukuweka Selo kagoma
Sasa mimi nifanyaje . . . Nina wasiwasi kuna harufu ya rushwa hapa.
Any way Dark City yuko vizuri na amekubali. In fact yupo kazini.
Mkuu inapofika kwenye fund ndo ngoma inanoga. Andika neno "JF Uchaguzi 2010" tuma kwa SMS kwenda namba 15010. Utakuwa umechangia sh 1,000.00. Nadhani hii inafaa.
Du!!!! La haula Kijana wangu!
Hakutapigwa Mizengwe kwenye makampuni ya simu hiyo namba isifanye kazi?
Kapumzike mkuu, this was good. Natumai mchana watakuja wajumbe wengine na michango zaidi. Ila cha msingi huyo DC apitie post zote assumirise points za muhimu ambazo tutazifikisha kwa hiyo serikali itakayoingia madarakani kwa ajili ya utekelezaji.Mkuu, niwie radi sana. Ni hizo Alvatar zenu zimesimama . . .
Nasikia kizunguzungu na uchovu . . . sorry naomba nipumzike kidogo sasa
Mkuu nadhani umeupotosha mjadala. Kuna watu wanasubiri kutoa maoni sasa hizi case ndani ya mjadala zinaweza kututoa kwenye hoja. Au agenda 2010 zimekamilika? :confused2::confused2: