Mkutano wa Hali ya Siasa Nchini na maazimio yake

Mkutano wa Hali ya Siasa Nchini na maazimio yake

Mod, naomba nibadilishie headline ya hii thread isomeke 'Maazimio ya Mkutano wa Hali ya Siasa nchini.

Hivi sasa majadiliano kuhusu mada za leo, yameendelea, Balozi Nicolas Kuhanga, amebonda sana mfumo wa elimu nchini akisema unaendeshwa kwa utashi wa kisiasa na sio kimfumo wa elimu, emesema Tanzania sasa haina walimu tena wa shule za msingi, bali ina watu wanaosimama madarasani. Nilitegemea angesema labda baadhi, amegeneralize hakuna walimu, hakuna mfumo wa elimu ni vurugu mechi tupu.
 
Maazimio 20 ya Mkutano. 1. Redet imepongezwa. 2. Rais Kikwete Apongezwa. 3. Wagombea binafsi waruhusiwe
 
mjumbe apinga rais asipongezwe. Akiuliza apongezwe kwa yapi?. Unless Redet inataka kujikomba komba kwa rais. Sasa hivi Makamo mkuu wa Chuo, Prof. Rwekaza Mukandara ndio anafunga rasmi mkutano huu wa 17 ya hali ya siasa nchini.
 
Last edited by a moderator:
mjumbe apinga rais asisongezwe. Akiuliza apongezwe kwa yapi?. Unless Redet inataka kujikomba komba kwa rais. Sasa hivi Makamo mkuu wa Chuo, Prof. Rwekaza Mukandara ndio anafunga rasmi mkutano huu wa 17 ya hali ya siasa nchini.

Namuunga mkono huyo mjumbe, apongezwe kwa lipi alilolifanya tangu aingie madarakani!? Usanii au uVDG!?
 
Prof. Mukandara afafanua pongezi kwa rais ni kwa hotuba yake ya jana, jana hakufika mwenyewe, katuma mtu muhimu, Waziri Mkuchika.
 
Prof. Mkandala ampiga nyundo za nguvu hoja za Iddi Simba kuhusu udumavu wa akili za wazawa, na kusisitiza mbona kuna wasomi wengi tuu waliotoka kwenye familia fukara. Hoja za Iddi Simba kuwa ukiwa fukara huwezi kusonga mbele zimebezwa kuwa hazina mashiko.
 
Last edited by a moderator:
Prof. Mukandala apongeza majadiliano ya mkutano huu wa 17 kuwa umeenda shwari bila mabishano, malumbano wala jazba za siasa za vyama. kwa lugha nyingine CUF, CCM Chadema wote walikuwa kitu kimoja, kujadili siasa za nchi.
 
Prof. Mukandala akamalizia kwa kukubali madhaifu ya mkutano huu wa 17 wa kujadili hali ya siasa za Tanzania bila kuigusa Zanzibar ama issue za Pemba, ili kurekebisha madhaifu hayo, REDET itaandaa mkutano mwingine mwezi ujao mahsusi kujadili masuala ya Zanzibar tena utafanyikia Zanzibar
 
Kama nilivyosema maazimio ni 20, sijaweza kuyaandika yote, ila nimeyasikiliza kwa juu juu tuu, nimeona kama hakuna kitu vile, ngoja nikiyapata yote na kuyameza, nitajaribu kutafakari zaidi, ila nav mimi pia naiona Redet inafanya kazi zake kwa umakini wa hali ya juu isije ikawaudhi washika mpini, kuna dhani ilijengwa hata Prof. Mkandala kapata ulaji na kuwa hapo alipo kwa sababu REDET imefagilia sana, ikamsafishia njia na si haba jamaa anakumbuka fadhila na ni mtu wa shukrani sana na hayo ndio maendeleo tunayoyataka.
Asanteni na kwaherini.

Mod ukiona vipi unganisha na ile ya jana, maazimio nitayaleta kesho.
 
Mod, naomba nisaidie, please cut mapendekezo na kuyaacha kama attachment, mimi natumia NT 98 haiwezi kuatach chochote.
 
Nimefanikiwa kujimod mwenyewe, maazimio nimeyaweka kwenye atachment.
Asanteni na kwaherini.
 
Prof. Mkandala ampiga nyundo za nguvu hoja za Iddi Simba kuhusu udumavu wa akili za wazawa, na kusisitiza mbona kuna wasomi wengi tuu waliotoka kwenye familia fukara. Hoja za Iddi Simba kuwa ukiwa fukara huwezi kusonga mbele zimebezwa kuwa hazina mashiko.

Prof ameamua kupinga tu, udumavu wa akili (mental stunting) kwa watanzania wengi, ni ukweli uliobainika kwa utafiti makini. Itakuwa vema kama Idd Simba katika presentation yake alirejea findings za utafiti huo
 
Prof ameamua kupinga tu, udumavu wa akili (mental stunting) kwa watanzania wengi, ni ukweli uliobainika kwa utafiti makini. Itakuwa vema kama Idd Simba katika presentation yake alirejea findings za utafiti huo

udumavu wa akili ndiyo mtaji wa CCM. Wananchi watakapovumbuka na kuamua kupiga vita ujinga na kuelevuka CCM na waogo wote watakuwa matatani.
 
Back
Top Bottom