Ulimbo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 3,768
- 4,038
Wapi Jechaaaaaaaaaaa...........
Yuko kwenye dust bin. Tambara likisha tumika hawalitaki tena.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapi Jechaaaaaaaaaaa...........
Sasa apimwe kama atafaa kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano 2025.
Kwani chadema mmeapanga kushindwa kule Zanzibar?This is unacceptable nchi mnakula familiya moja tu.
Atakayopewa ndio shughuli nyingine na sio Uraisi tena.Tulia wewe CCM na serikalini nafasi ziko kibao Mbarawa hawezi kosa kupewa
Huko Zanzibar kuna mfaa Nahodha maana amekuwa KWaziri Kiongozi wakati wa Amani Karume. Kwa hiyo, ana uzoefu mkubwa tu.Marekebisho: Zanzibar haina jeshi!
Walimtoa Sultan Mwarabu ili waweke sultani mswahili..Dr. Mwinyi Mgombea Urais Kwa Ticket Ya CCM Zanzibar
Amepata kura 129
Leo Halmashauri Kuu ya CCM inapokea mapendekezo ya Kamati Kuu kuhusiana na waliopendekezwa kugombea Urais wa JMT na ule wa Zanzibar.
Kadhalika itapokelewa ripoti ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 5 iliyopita na kupitishwa ilani ya miaka 5 ijayo.
Mkutano uko mubashara TBC na Channel ten, ITV, Star tv na Upendo tv
Up dates:
Wajumbe wameshaketi ukumbini wakimsubiri mwenyekiti ambaye ataingia wakati wowote kuanzia sasa. Rais Magufuli ameingia ukumbini na wajumbe wote wanamshangilia kwa shangwe na vigelegele.
Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amefungua kikao hiki na kutoa rai kuwa ianzwe ajeda kubwa ya Uchaguzi wa Mgombea Urais Zanzibar
Rais Magufuli pamoja na Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuanza na ajenda ya Wagombea Urais Zanzibar. Mpaka sasa kuna jumla ya majina matano ya Ugombea Urais Zanzibar.
Dr Bashiru amewataka Wagombea watano waliopitishwa na kamati maalumu ya halmashauri kuu kuja mbele ili kusalimia alafu baada ya mchakato huo Mwenyekiti atataja majina matatu yaliyopita.
Rais Magufuli (Mwenyekiti wa CCM) ametoa idhini ya majina matatu yaliyopendekezwa kusomwa na katibu Mkuu wa chama Dkt. Bashiru ambaye amesema kuwa Wagombea watatu waliopita ni:
1. Dkt. Khalid Salum Mohamed.
2. Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi.
3. Shamsi Vuai Nahodha.
Rais Magufuli amewakaribisha Wagombea ambao hawakupita ili kutoa neno la shukrani.
Prof. Mbalawa pamoja na Mh. Hamis Mussa Omari wamekuja mbele ya wajumbe wa mkutano huu na kurumshukuru Mungu pamoja na Wajumbe kwa hatua aliyofikia pamoja na kumshukuru Rais Magufuli katika masuala mbalimbali. Sambamba na hilo, Prof Mbalawa amesisitiza kumuunga mkono Mgombea atakayefanikiwa kupita ili CCM ishinde.
Baada ya Wajumbe ambao hawakupita kutoa shukrani Rais Magufuli amewakaribisha Wagombea waliopita kutoa neno lao kwa ufupi
Hussein Ali Hassan Mwinyi
(Salamu)
Nimesimaama mbele zenu kuomba kura zenu, mnichague kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi ujao katika nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Elimu yangu ni shahada ya Uzamili katika fani ya Udaktari wa Binadamu. Uzoefu wangu katika serikali ni wa miaka 20. Nimeingia serikalini mwaka 2000 na nipo hadi sasa.
Naibu Waziri wa Afya tangu mwaka 2020-2005. Baada ya hapo nimekuwa waziri kamili kwa miaka 15 kwa miaka mbalimbali ikiwemo ya Afya, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano; na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, nafasi ambayo nimeishika kwa miaka 11 hadi hivi sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uzoefu kwenye chama nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama chetu; nimechaguliwa mara mbili. Nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa vipindi vitatu. Na nimekuwa kwa nafasi yangu ya Ubunge, Mjumbe wa Halmashauri Kuu za mkoa, wilaya na jimbo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi yangu kwenu endapo mtanichagua basi nitayaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 ya Zanzibar na nitadumisha Muungano wetu.
Lakini pia, nitayaendeleza yote yaliyofanya na awamu zilizotangulia, hususan awamu ya saba (7)chini ya Dkt. Ali Mohammed Shein.
Vilevile niwaahidi kwamba nitatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi yam waka 2020/25 itakayotolewa kwa upande wa Zanzibar.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba mnipigie kura za NDIYO mimi Hussein Ali Hassan Mwinyi.
(Maagano)
Shamsi Vuai Nahodha
(Salamu na Shukrani kwa Mwenyezi Mungu na Chama)
Mimi Shamsi Vuai Nahodha ambaye nagombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi niliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kwa muda wa miaka 17 na ni miongoni mwa watu wachache sana waliopata bahati ya kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama mtekelezaji mkuu wa Ilani kwa muda wa miaka 10 mfululizo. Nadhani rekodi hiyo inashikiliwa na mzee wangu Seif Ali Idd na mimi ninayefuata.
Nimetafakari sana wakati nimataka kugombea nafasi hii adhimu kwa taifa letu. Na nikafikia mahali nikadhani kuna jambo mimi kwa kushirikana na wenzangu ninaweza kulifanya. Kwanini nadahani naweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi sana? Nimejifunza mengi kutoka kwa viongozi wetu wa chama na kitaifa – Dkt. Magufuli na Mzee wangu Dkt. Shein. Katika kipindi chote hiki nimejifunza karama ya uongozi. Namna kiongozi anavyotakiwa awe, tabia za kiongozi.
Dkt. Shein ametuonesha sisi vijana namna kiongozi wa kiataifa anatakiwa awe. Ni mnyenyekevu na mpole sana.
Mwaka 2010 nilisimama hapa kushindana naye. Baada ya hapo hakuonesha nongwa. Alinisikiliza kwa umakini sana. Amenitendea zaidi ya ninavyostahiki.
Watu wengi wanaofanya kazi na Shein wanaweza wanamuona wa kawaida sana kwasababu ya unyenyekevu lakini ana moyo mpana sana.
Kama nitapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mgombea na hatimaye Rais wa Zanzibar, nitafanya kila niwezalo kusimamia Muungano, Mapinduzi na rasilimali za Taifa letu kwa ujasiri wa juu sana.
Maendeleo hayana vyama
Kitakachomcost Hana asili ya Zanzibar I, mzee mwinyi baba yake Ni mtu wa bara Tena kutoka pwani, Sasa wazanzibar hawawezi kukubali kuwa na raisi mtanganyika
Wapi Jechaaaaaaaaaaa...........
Kwani chadema hamshindi huu uchaguzi?Kura hazijawahi kuchagua Rais Tanzania.
Only Zwazwa mdondo people will trust hilo Genge.
Haya "Keki ya Taifa" Ina Wenyewe.
Wale wenye vitambulisho vya "Machinga" Endeleeni Kuchapa Kazi.
Msisahau Kukusanya Familia Zenu Na Kwenda Kuwaimbia "Wenye Nchi" Ule Wimbo Wa "Baaba Baaba Baba Huyoooo ..... Huku Mkiruka Ruka Juu.
Uzoefu wa wa huko nyuma!UPEMBA NA UUNGUJA ndio uliomnyima PRO. MAKAME