Uchaguzi 2020 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM: Dkt. Hussein Ally Mwinyi achaguliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM. Membe afukuzwa rasmi

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM: Dkt. Hussein Ally Mwinyi achaguliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM. Membe afukuzwa rasmi

Safari hii wajumbe wamesoma conscious ya walio wengi.Huyu kijana hajawahi kipiga vijembe bugeni ameongoza wizara mbili bila longolongo na haimbagi mapambio kama wengine ; ingawa sikufaulu hesabu,anaweza kushinda
Dr. Mwinyi Mgombea Urais Kwa Ticket Ya CCM Zanzibar
Amepata kura 129
 
Sasa zile kelele zenu za eti hoo Membe jasusi mbobevu na takataka nyingine kama hizo mlikuwa mnatoa wapi huku mkijua namna ccm inavyofanya kazi kama taasisi na si kama mtu mmoja?

Umekubali sasa kwamba Magufuli hafanyi yeye kama yeye bali kitaasisi?
Sasa hayo ya membe yametokea wapi ?

Kuna taaisis kama taasis na kuna ustashi wa mtu binafsi...Mimi kuwa ndani ya taasia haiwez nizuia nisiangalie mtu ambae anaweza kuvaa viatu vyangu...Kuna kupendekeza jina kama mwenyekiti so inavyofika kwenye maamuz basi una mute .
 
1'viongozi wote wanaapa na wanatii ndio mana wapo madarakani
2.Hakuna utawala uliishughulika na mafisadi kama huu.Mafisadi yametemeshwa bilioni 200 yalizokwapua na mengi bado yapo jela
3.Tumetoa mikopo ya vijana na akina mama kupitia halmashauri zao na mikopo inaendelea,kila halmshauri imeamriwa kutenga asilimia moja ya pato kwa ajili hiyo
4.ahadi hiyo sikuisikia
5.zaidi ya ajira milioni moja zimezalishwa kutokana na kufunguliwa viwanda vipya zaidi ya 1500 nchi nzima
6.$erikali imeendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake na kuimarisha mazibgira ya kufanyia kazi
Pumba tupu! Hakuna kilichotekelezwa vyote hivyo. Hayo maneno hata kwenye debe tupu yamo. Mimi personally nina project ya kuajiri vijana 20 kwa average salary ya Tshs400,000 per month. Mpaka sasa nimecheleweshwa kuungiwa umeme na Tanesco wiki ya 3 sasa na makadirio ya TRA yako juu sana na hata biashara yenyewe sijaanza. Ajira my backside!
 
U
UPDATES 1315hrs: Matokeo ya Kura za ya wanachama watatu waliokuwa wakiomba ridhaa ya kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM.

1. Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi -kura 129 (78.65%)

2. Dkt Khalid Salim Mohamed -kura 19 (11.58%)

3. Shamsi Vuai Nahodha -kura 16 (9.75%).
Zanzibar 2020 - Wasifu: Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais ajaye wa Zanzibar



Leo Halmashauri Kuu ya CCM inapokea mapendekezo ya Kamati Kuu kuhusiana na waliopendekezwa kugombea Urais wa JMT na ule wa Zanzibar.

Kadhalika itapokelewa ripoti ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 5 iliyopita na kupitishwa ilani ya miaka 5 ijayo.
Mkutano uko mubashara TBC na Channel ten, ITV, Star tv na Upendo tv

Up dates:
Wajumbe wameshaketi ukumbini wakimsubiri mwenyekiti ambaye ataingia wakati wowote kuanzia sasa. Rais Magufuli ameingia ukumbini na wajumbe wote wanamshangilia kwa shangwe na vigelegele.

Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amefungua kikao hiki na kutoa rai kuwa ianzwe ajeda kubwa ya Uchaguzi wa Mgombea Urais Zanzibar

Rais Magufuli pamoja na Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuanza na ajenda ya Wagombea Urais Zanzibar. Mpaka sasa kuna jumla ya majina matano ya Ugombea Urais Zanzibar.

Dr Bashiru amewataka Wagombea watano waliopitishwa na kamati maalumu ya halmashauri kuu kuja mbele ili kusalimia alafu baada ya mchakato huo Mwenyekiti atataja majina matatu yaliyopita.

Rais Magufuli (Mwenyekiti wa CCM) ametoa idhini ya majina matatu yaliyopendekezwa kusomwa na katibu Mkuu wa chama Dkt. Bashiru ambaye amesema kuwa Wagombea watatu waliopita ni:

1. Dkt. Khalid Salum Mohamed.
2. Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi.
3. Shamsi Vuai Nahodha.

Rais Magufuli amewakaribisha Wagombea ambao hawakupita ili kutoa neno la shukrani.

Prof. Mbalawa pamoja na Mh. Hamis Mussa Omari wamekuja mbele ya wajumbe wa mkutano huu na kurumshukuru Mungu pamoja na Wajumbe kwa hatua aliyofikia pamoja na kumshukuru Rais Magufuli katika masuala mbalimbali. Sambamba na hilo, Prof Mbalawa amesisitiza kumuunga mkono Mgombea atakayefanikiwa kupita ili CCM ishinde.

Baada ya Wajumbe ambao hawakupita kutoa shukrani Rais Magufuli amewakaribisha Wagombea waliopita kutoa neno lao kwa ufupi

Hussein Ali Hassan Mwinyi
(Salamu)

Nimesimaama mbele zenu kuomba kura zenu, mnichague kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi ujao katika nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Elimu yangu ni shahada ya Uzamili katika fani ya Udaktari wa Binadamu. Uzoefu wangu katika serikali ni wa miaka 20. Nimeingia serikalini mwaka 2000 na nipo hadi sasa.

Naibu Waziri wa Afya tangu mwaka 2020-2005. Baada ya hapo nimekuwa waziri kamili kwa miaka 15 kwa miaka mbalimbali ikiwemo ya Afya, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano; na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, nafasi ambayo nimeishika kwa miaka 11 hadi hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzoefu kwenye chama nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama chetu; nimechaguliwa mara mbili. Nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa vipindi vitatu. Na nimekuwa kwa nafasi yangu ya Ubunge, Mjumbe wa Halmashauri Kuu za mkoa, wilaya na jimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi yangu kwenu endapo mtanichagua basi nitayaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 ya Zanzibar na nitadumisha Muungano wetu.

Lakini pia, nitayaendeleza yote yaliyofanya na awamu zilizotangulia, hususan awamu ya saba (7)chini ya Dkt. Ali Mohammed Shein.

Vilevile niwaahidi kwamba nitatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi yam waka 2020/25 itakayotolewa kwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba mnipigie kura za NDIYO mimi Hussein Ali Hassan Mwinyi.
(Maagano)

Shamsi Vuai Nahodha
(Salamu na Shukrani kwa Mwenyezi Mungu na Chama)

Mimi Shamsi Vuai Nahodha ambaye nagombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi niliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kwa muda wa miaka 17 na ni miongoni mwa watu wachache sana waliopata bahati ya kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama mtekelezaji mkuu wa Ilani kwa muda wa miaka 10 mfululizo. Nadhani rekodi hiyo inashikiliwa na mzee wangu Seif Ali Idd na mimi ninayefuata.

Nimetafakari sana wakati nimataka kugombea nafasi hii adhimu kwa taifa letu. Na nikafikia mahali nikadhani kuna jambo mimi kwa kushirikana na wenzangu ninaweza kulifanya. Kwanini nadahani naweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi sana? Nimejifunza mengi kutoka kwa viongozi wetu wa chama na kitaifa – Dkt. Magufuli na Mzee wangu Dkt. Shein. Katika kipindi chote hiki nimejifunza karama ya uongozi. Namna kiongozi anavyotakiwa awe, tabia za kiongozi.

Dkt. Shein ametuonesha sisi vijana namna kiongozi wa kiataifa anatakiwa awe. Ni mnyenyekevu na mpole sana.

Mwaka 2010 nilisimama hapa kushindana naye. Baada ya hapo hakuonesha nongwa. Alinisikiliza kwa umakini sana. Amenitendea zaidi ya ninavyostahiki.

Watu wengi wanaofanya kazi na Shein wanaweza wanamuona wa kawaida sana kwasababu ya unyenyekevu lakini ana moyo mpana sana.

Kama nitapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mgombea na hatimaye Rais wa Zanzibar, nitafanya kila niwezalo kusimamia Muungano, Mapinduzi na rasilimali za Taifa letu kwa ujasiri wa juu sana.

Dkt. Khalid Salum Mohamed
(Salamu)

….Kufikia nafasi hii ni ndoto.

Nilisoma Donge, skuli ya Msingi. Elimu ya Sekondari nilisoma Fidel Castro, Pemba. Na baadaye nilienda kusoma mafunzo ya Kilimo (certificate) katika Chuo cha Kilimo Naliendele, Mtwara.

Baada ya hapo nilipata mafunzo tena Uyole, Mbeya. Nilifanya mafunzo ya Diploma Mlingano, Tanga. Na baadaye kufanya digrii ya kwanza Sokoine. Digrii ya pili ya Agricultural Economics nilifanyia Chuo Kikuu cha Reading cha UK. Nilirudi nikafanya tena digrii ya uzamivu katika chuo cha Sokoine.

Niliajiriwa toka mwaka 1980 katika Wizara ya Kilimo. Nilifanya kazi kama Afisa Kilimo wa Wilaya na Mkoa. Baadaye nikawa Mkurugenzi wa Mipango na Sera katika Katika Wizara ya Kilimo, Zanzibar. Na baadaye nikawa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto.

Mwaka 2005 nilibahatika kuwa Program Analyst katika Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na baadaye kurudi serikalini na kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo. Nilikuwa Mwenyekiti wa ZSSF, mfuko wa hifadhi ya Jamii kwa miaka 6.

Dk. Shein alinichagua kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Pale nilijifunza mambo mengi kuhusu Muungano. Nilisimamia masuala wanayoyaita “Kero za Muungano”.

Niliingia kwenye siasa mwaka 2016 baada ya uchaguzi wa marudio. Na nilichaguliwa tena na Dk. Shein kuwa Waziri wa Fedha kwa miaka mitatu hadi Machi 2019.

Uzoefu wangu wa Kisiasa. Nimejiunga na CCM tangu mwaka 1980.


Maendeleo hayana vyama

Mndengereko mwingine anaenda kutawala Zanzibar!
 
Imekuaje huyu Mbarawa akatupwa mbali kule wakati kuna wadau humu walisema ni kipenz cha jiwe
 
Back
Top Bottom