Uchaguzi 2020 Mkutano wa Kimei Vunjo. Sijui atapitaje?

Kwaiyo katika watu milioni karibia 60 yeye ndio wa maana katika pesa na mipango??

Tanzania inahitaji kuendeshwa kimfumo sio kutumia fikra na ushawishi wa mtu.

Tanzania siku zote litabaki kuwa taifa la wajinga kwa kutegemea hayo
Ukisema Tanzania ni taifa la wajinga na wewe umo.

Tofautisha majukumu ya viongozi ambao ni wanasiasa serikalini na watumishi wa umma wa ndani ya serikalini (makatibu wa kuu kwenda chini). Kulijua hili utaelewa nani anajukumu ya kuujenga na kuulinda mfumo serikalini.

Sioni tatizo lolote kwa Dkt. Kimeo akiwa waziri kwenye serikali. Ni Mtanzania, ni msomi na ana uwezo wa kuongoza.
 
Haya ni mawazo yako kwa Dr kimeo Kama ulivyomuita! Hukatazwi kuwaza hivi

Tanzania inahitaji mfumo kukuwa katika sekta zote badala ya kuhitaji mtu

Think
 
Aisee!! Yaani atashinda kwa kupigiwa kura na hao watu 200 hapo pichani?
 
Haya ni mawazo yako kwa Dr kimeo Kama ulivyomuita! Hukatazwi kuwaza hivi

Tanzania inahitaji mfumo kukuwa katika sekta zote badala ya kuhitaji mtu

Think
Huo mfumo unaendeshwa na binadamu au robot? Kama ni binadamu basi Dkt Kimei ni mmoja ya hao binadamu pamoja na wengine wengi tu.
 
D
Dk Kimeo ndo nani mnashindwa hata kuandika vizuri, ni utopolo tu wa CCM.
 
D

Dk Kimeo ndo nani mnashindwa hata kuandika vizuri .ni utopolo tu wa ccm .
Mtambo ndio wa kulaumiwa sio mimi, nimeandika Dkt Kimei mtambo imebadilisha na kuweka Dkt Kimeo. Kumradhi.
 
Huo mfumo unaendeshwa na binadamu au robot? Kama ni binadamu basi Dkt Kimei ni mmoja ya hao binadamu pamoja na wengine wengi tu.
Naona hatuelewani tuko katika level tofauti, msubiri le mutuz level yako
 
Hawa wanasiasa wanarahisisha maisha. Anyway hakuna asiyependa kujiajiri kama uwezo wa kufanya hivyo upo ni jambo bora.
Angejiajiri yeye kwanza lakin ndo kwanza anasaka kura.
 
Kule Mbatia anapita mapema sana
hapiti nakumbuka 2015 alikuja Makomu uwanjan hakuna alichoongea zaid ya kumtukana Mrema sijui kazaa na mpwa wake, Kimei sasa ana pointi za kutosha hata kama hatokuja kuzitekeleza ila anaongea point
 
Dr Kimei na mke wa Kikwete wote wanajidhalilisha. Kwa fedha walizonazo kama kweli wangekuwa werevu wangezitumia kuinua hali za wengine kwa kuanzisha miradi chanya sehemu mbalimbali hapa nchini.
Kama Dr Kimei anafaa kwenye siasa basi angojee ateuliwe na rais ajaye kwenye zile nafasi 10 za Rais kama waziri wa fedha Dr Mpango alivyoteuliwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…