Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) chenye wanachama wanaojumuisha CCM, CHAUMA, ACT Wazalendo, pamoja na NCCRA Mageuzi, leo Septemba 7, 2026 wanakutana kuzungumza kuhusu hali ya demokrasia Tanzania. na matukio ya wakati wa uchaguzi na baada ya Uchaguzi Oktoba 29, 2025.
Dorothy Semu- Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Tanzania ni kwa ajili ya vijana wanaotafuta fursa za maisha; ni kwa ajili ya wanawake wanaotafuta haki, usalama na usawa; ni kwa ajili ya wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wanafunzi na kila mwananchi anayetamani kuona taifa letu likisimama imara na maisha ya wananchi yakiendelea kuwa bora.
Tusibaki katika utamaduni wa kulaumiana pekee. Tanzania inahitaji demokrasia ya kweli—demokrasia inayogusa maisha ya kila mwananchi, inayoheshimu utu na haki za watu wote.
Tanzania inahitaji taasisi zilizo imara, utawala wa sheria unaotanguliza sheria kuliko matakwa ya mtu au chombo, pamoja na Katiba inayosimamia na kulinda haki za Watanzania wote.