Ndugu yangu .... kuvuja, nafuu kwa mchukuzi, naungana nawe kwa asilimia 100%, mambo ya jikoni na chumbani, waachiwe wenyewe, tusiwaingilie kabisa, tatizo hapo mwanzo, Zanzibar ilikuwa ni nyumba ya chumba kimoja, jikoni ndio hapo hapo, chumbani, hapo hapo na sebuleni hapo hapo, ukipakua chakula mbele ya mgeni na watoto wapo, huweza tenga, hiki cha wageni (gesi na mafuta) na hiki cha wote. Mgeni (bara) kala kanogewa mpaka anataka na cha wote.
Sasa nyumba ya Zanzibar imekuwa, sasa kuna jiko linajitegemea na sebule sio chumbani. Kaja tena yule yule mgeni bara, wewe chakula wapikia jikoni, haoni, kwa vile alifaidi, unataka kuamua leo usipakue cha wageni (gesi na mafuta) bali upakue cha wote ili chawageni ukakilie chumbani kwa kujificha, mgeni huyo kama ni mlafi, ujue hapo haondoki mpaka ale kile kinono cha wageni,
Gesi na mafuta hayakuwemo kwenye mambo ya muungano, mgeni bara, kaja mmempakulia bila hiana yoyote, hamkulalakamika hapo mwanzo, mgeni kanogewa, ndio sasa mwataka mwambia mgeni kuanzia sasa kile chakula si cha wageni tena, bali cha wote?!. Its too little too late, madhali mgeni kesha onja, mwache tuu ale na eendelee kula, tena si mafuta tuu, hadi samaki wa bahari kuu ni wa muungano!, tutakuja hadi maji ya bahari ni ya muungano na mwisho kabisa Zanzibar-Mkoa wa muungano!.