Mkutano wa Trump na Zelensky waisha na sintofahamu

Mkutano wa Trump na Zelensky waisha na sintofahamu

Kagombezwa bwana acha basiii huoni kuwa walikuwa wanabishana kabisa mpaka zele akawa kama anataka kususa kwanini mnapenda kuuficha ukweli ??

Leo hii zele yupo uchi dunia nzima clip yake akigombezwa inatembea watu wana mcheka 🤣🤣😃
Alikua hagombezwi bana walikua wanabishana 😁
 
Ukraine hakuna mgogoro, bali ni kwamba Urusi iliivamia Ukraine na kujiemegea ardhi. Ukraine inapigana kulinda ardhi yake. Mazungumzo yalifanyika baina ya nchi za ulaya na Putin kabla hajafanya uvamizi huo, ila yeye akadanganya kuwa Urusi haina mpango wa kuivamia Ukraine. Hata baada ya kuanza uvamizi wenywewe kulikuwa na mkutano wa amani kule Minsky; Uraris wakawa kicha ngumu. Wakarudia mkutano mwingine tena huko huko Minsky, bado urusi ikaweka ngumu, mkutano wa tatu ulifanyika Ankara Uturuki, bado Urusi akasimama pale pale kutaka Ukraine iangushwe. Unakumbuka mikutano hii chini? Kwa hiyo tangu mwanzo mazungumzo yalifanyika lakini Urusi ndiye aliyesngangania vita. Sasa hivi siyo wakati wa maongezi tena baada ya kupigana miaka mitatu yote. Urusi inatakiwa ing'olewe kwa nguvu siyo kwa kubembelezwa tena. Kosa la Trump anafikiri kuwa Ukraine ya wakati inaanza kuvamiwa ndiyo ya leo, na ile Urusi ya wakati wa Soviet Union ndiyo ya leo.

View attachment 3254062

View attachment 3254063

Trump alikulia na kuzeekea New York na hivyo ana tabia zakimafia za kutishia na kulazimisa mambo. kama kwenye muvi hizi za wakati huo huko New York

View attachment 3254067View attachment 3254068View attachment 3254074
Trump kaamua waziwazi kusimama upande wa Putin, huyu Mzee atawavuruga kweli kweli Ulaya magharibi na NATO yao.
 
Hiyo ndo maana halisi ya ubishi dharau na matusi lazima vihusike kwahiyo ukiwa mpole utaonekana umedharauliwa😁
Yule kagombezwa mkuu 🤣🤣🤣
Trump kaamua waziwazi kusimama upande wa Putin, huyu Mzee atawavuruga kweli kweli Ulaya magharibi na NATO yao.
Yaani vichwa vina wauma lakini kwanini kaamua kufanya hivyo ni puppet wa russia ama niaje?? Inakuwaje nchi hasimu leo ziwe kitu kimoja smh
 
Wakati mazungumzo ya amani yakiwa yanaendelea ni vyema kwa Ukraine kutopoteza kuungwa mkono na Wamarekani, ili kufanikisha hilo, rais Zelensky atapaswa kutanguliza diplomasia huku akipigania maslahi ya Ukraine kwenye mchakato huu wa makubaliano.
Huu mchakato umeshaanza bila Ukraine kuhusishwa, kiufupi ameshafanywa daraja la 2.
 
Februari 28, 2025, Donald Trump kupitia mtandao wa X, alimkashifu Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kutoheshimu nchi ya Marekani wakati wa mkutano wake na raisi huyo katika ikulu ya Marekani. Trump alimkosoa Zelensky juu ya kutoheshimu nchi hiyo kwa kuidharau ndani ya ofisi ya "oval" na kuongezea kuwa - "Anaweza kurudi kama atakuwa yuko tayari kwa Amani" -

Ukosaoaji huu umemuweka Zelensky aonekane kama mtu asiye na msimamo katika kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine, jambo linalokinzana na msukumo wa Trump wa kutafuta muarobaini wa mgogoro huo kwa njia ya haraka.

Licha ya rais wa Ukraine kuonekana mtu mwenye kupenda kujibizana, kwenye hili ameonesha kukwepa mitego ya Trump inayolenga kumfarakanisha na watu wa Marekani.

Dakika thelathini tu baada ya kuondoka katika Ikulu ya Marekani alichapisha kwenye mtandao wa X, akiishukuru Marekani na kusisitiza "amani ya haki na ya kudumu" bila ya kujibu shutuma za Trump. Hii inaakisi mtazamo na nia yake ya tangu awali ya kutovunja mahusiano na nchi hiyo: Ukizingatia alipokaa kimya kipindi Trump alipomwita "dikteta" mnamo Februari, Zelensky aliikwepa hoja hiyo kwa kuto kumjibu Trump, huku akihamisha shutuma kwenye upotoshaji wa nchi ya Urusi.

Kujishikiria kwa Zelensky hakutokani na busara tu bali uhitaji wa kuihusisha marekani katika kuumaliza mgogoro wake na nchi ya Urusi.

Wakati mazungumzo ya amani yakiwa yanaendelea ni vyema kwa Ukraine kutopoteza kuungwa mkono na Wamarekani, ili kufanikisha hilo, rais Zelensky atapaswa kutanguliza diplomasia huku akipigania maslahi ya Ukraine kwenye mchakato huu wa makubaliano.
Anachofanya Zelesky ndio kitu mwanaume rijali unatakiwa ufanye sio kwakuwa una nguvu unidharau jamaa ana busara sana Kwa maneno wanayotoa team ya Trump kama huna busara na hekima unaweza kuishia kujibizana nao mitandaoni ila Zelesky akaamua kukaa kimya.

Trump na team yake wamekaa kama mashangingi kutwa kubwatuka tu
 
Hakika Umaskini ni laana. Zelensky anagombezwa kama mtoto mchanga. Viongozi wa Afrika wakifika kwa mwamba lazima wachapwe bakora.

ISOMEKE: Viongozi wa Afrika mna la kujifunza kwa Zelensky
Ila Trump atakuwa mzaramo maana sio kwa kumnanga huko mwenzie.

Na mbaya zaidi huwa hampi nafasi mtu anaemnanga kusema yaan anataka aseme yeye tu.

Ametamka neno stupid president duuuh yule mzee ulaya wajipange vinginevyo tariffs zitawahusu.
 
Si kweli kuwa Ukraine ikishindwa na Ulaya yote itatekwa na Urusi.
Urusi tangu mwanzo haikuwa na nia ya kuiteka hata Ukraine lakini ujinga na jeuri za Zelensky ndizo zilizoifanya Urusi iamue kuitia adabu kidogo.
Vita hivyo vimeonesha kuwa Ulaya yote ni dhaifu sana mbele ya Urusi lakini haina maana kuwa Urusi itathububu kujaribu kuteka maeneo ya nchi yoyote ya Ulaya iwapo kila mmoja ataonesha heshima kwao.
2014 nani alikuwa rais wa Ukraine?
 
Usalama wa Ukraine ndio Usalama wa bara lote la Ulaya, hususani Ulaya Magharibi.

Ukraine ikishindwa Vita maana yake ni kwamba Ulaya yote kabisa itakuwa imetekwa na Urusi. Hili litakuwa jambo baya sana tena ni jambo la hatari kubwa sana kupita kiasi kwa maisha ya Watu wote kabisa wa bara la Ulaya.
Kwa hali kama hiyo, ni Bora Watu wa Ulaya waingie katika Vita ya Tatu ya dunia kuliko kuruhusu Urusi ishinde Vita hiyo.
Kwanza kabisa, lengo Kuu mojawapo la kuanzishwa kwa NATO ilikuwa ni kupambana na Udikteta wa Watawala wababe wa Urusi.

Urusi ikishinda Vita hii, bado ataendelea kuteka maeneo mengine zaidi na zaidi hadi Ulaya yote kabisa iwe chini ya Utawala wa Urusi, Putin hataishia kuiteka Ukraine peke yake.
Duuh...
We jamaa ni muongo balaa
 
Ukraine hakuna mgogoro, bali ni kwamba Urusi iliivamia Ukraine na kujiemegea ardhi. Ukraine inapigana kulinda ardhi yake. Mazungumzo yalifanyika baina ya nchi za ulaya na Putin kabla hajafanya uvamizi huo, ila yeye akadanganya kuwa Urusi haina mpango wa kuivamia Ukraine. Hata baada ya kuanza uvamizi wenywewe kulikuwa na mkutano wa amani kule Minsky; Uraris wakawa kicha ngumu. Wakarudia mkutano mwingine tena huko huko Minsky, bado urusi ikaweka ngumu, mkutano wa tatu ulifanyika Ankara Uturuki, bado Urusi akasimama pale pale kutaka Ukraine iangushwe. Unakumbuka mikutano hii chini? Kwa hiyo tangu mwanzo mazungumzo yalifanyika lakini Urusi ndiye aliyesngangania vita. Sasa hivi siyo wakati wa maongezi tena baada ya kupigana miaka mitatu yote. Urusi inatakiwa ing'olewe kwa nguvu siyo kwa kubembelezwa tena. Kosa la Trump anafikiri kuwa Ukraine ya wakati inaanza kuvamiwa ndiyo ya leo, na ile Urusi ya wakati wa Soviet Union ndiyo ya leo.

View attachment 3254062

View attachment 3254063

Trump alikulia na kuzeekea New York na hivyo ana tabia zakimafia za kutishia na kulazimisa mambo. kama kwenye muvi hizi za wakati huo huko New York

View attachment 3254067View attachment 3254068View attachment 3254074
Waziri mkuu mstaafu wa German aliwahi kukili kua mikataba waliyoingia na Urusi ilikua kuipumbaza Urusi huku Ukrein ikiendelea kujipanga kwa vita na Urusi.
 
Trump kaamua waziwazi kusimama upande wa Putin, huyu Mzee atawavuruga kweli kweli Ulaya magharibi na NATO yao.
Trump anauona ukweli kuliko wengi na upande aliosimama Trump ndio upande sahihi.
 
DU
Si kweli kuwa Ukraine ikishindwa na Ulaya yote itatekwa na Urusi.
Urusi tangu mwanzo haikuwa na nia ya kuiteka hata Ukraine lakini ujinga na jeuri za Zelensky ndizo zilizoifanya Urusi iamue kuitia adabu kidogo.
Vita hivyo vimeonesha kuwa Ulaya yote ni dhaifu sana mbele ya Urusi lakini haina maana kuwa Urusi itathububu kujaribu kuteka maeneo ya nchi yoyote ya Ulaya iwapo kila mmoja ataonesha heshima kwao.
dU
 
Zelensky alitamani ardhi ipasuke azame chini kwa kusimangwa kama mtoto aliyejinyea mbele ya media kwa upumbavu wake wa kuingia vitani na Urusi taifa lenye nguvu kubwa Duniani kwa kutegemea silaha za misaada[emoji1787][emoji1787]
Mkuu, akilizako hazina tofauti na za Tramp, iviulitaka Zelensk afanyeje wakati urusi wanavamia nchi yake, tuanzie hapo.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Trump anauona ukweli kuliko wengi na upande aliosimama Trump ndio upande sahihi.
Tramp anaona maslahi zaidi ya ukweli, unadhani angepewa madini angezuiavita kwa njia gani.

Ameulizwa swali kwamba kama ikitokea Putin akikataa kuondoa majeshiyake Ukraine atafanya nini, hatoijibu linalo eleweka anarukarukatu.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Tramp anaona maslahi zaidi ya ukweli, unadhani angepewa madini angezuiavita kwa njia gani.

Ameulizwa swali kwamba kama ikitokea Putin akikataa kuondoa majeshiyake Ukraine atafanya nini, hatoijibu linalo eleweka anarukarukatu.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Atoe jibu gani, wakati kashasema Zele asahau maeneo yaliyochukuliwa na Putin.

Zele anachotaka ni USA na EU kupeleka majeshi kabla ya cease fire. Trump anachotaka ni security guarantee after cease fire.
 
Back
Top Bottom