Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo mnamo Januari 21, 2025 amkimshinda
Freeman Mbowe ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 20.
Mara nyingi kumekuwapo na taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikimuhusisha Lissu juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa ndani na nje ya chama chake. Rejea
hapa,
hapa, hapa na
hapa.
Mnamo tarehe 10 mwezi februari 2025 CHADEMA ilitoa
taarifa kwamba mwenyekiti wa Chama hicho Taifa
Tundu Lissu atalihutubia Taifa siku ya Jumatano Februari 12, 2025, saa kumi jioni, ikitarajiwa kufanyika Makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar es salaam
Kupitia mtandao wa X kumeibuka
chapisho linalosambazwa katika mtandao huo kwamba mkutano huo wa Lissu umehairishwa.
Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa chapisho hilo si la kweli na halijachapishwa na
kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya CHADEMA.
Aidha hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Chama hicho kuhusu kuhairishwa kwa mkutano huo wa mwenyekiti na waandishi wa habari bali unatarajiwa kufanyika kama ulivyopangwa Jumatano tarehe 12, 2025 saa kumi jioni kama ambavyo
taarifa rasmi ya chama hicho ilivyoeleza.
Hata hivyo mkutano huo unatarajiwa kuanyika katika makao makuu ya chama hicho na si Ubungo Plaza kama ilivyoelezwa katika chapisho hilo linalopotosha.