Mkutano wa uchaguzi wa askofu dayosisi ya mwanga Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania kufanyika machi 10, 2025, mrithi wa sendoro kupatikana

Mkutano wa uchaguzi wa askofu dayosisi ya mwanga Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania kufanyika machi 10, 2025, mrithi wa sendoro kupatikana

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa kamili hapo chini kwa kiswahili:

Mwanga
. Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) inatarajia kufanya mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi, Machi 10, 2025, ili kumpata mrithi wa aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo, Chediel Sendoro.

Dayosisi hiyo inafanya uchaguzi wa Askofu ikiwa ni miezi sita imepita tangu Askofu Sendoro afariki dunia kwa ajali, hivyo nafasi hiyo kubaki wazi.

Askofu Sendoro alifariki dunia Septemba 9, 2024 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Kisangiro, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro saa 1:30 usiku, baada ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Prado, akitokea Kileo kuelekea nyumbani kwake Mwanga, kugongana uso kwa uso na lori.

RELATED​

  • KKKT yakemea matukio ya utekaji, mauaji​

    Kitaifa Sep 17
  • Vilio vyatawala mwili wa Askofu Sendoro ukiagwa Mwanga​

    Kitaifa Sep 16
Historia inaonyesha, Askofu Sendoro ndiye wa kwanza wa Dayosisi ya Mwanga ambaye aliingizwa kazini Jumapili ya Novemba 6,2016 baada ya kuzaliwa kwa dayosisi hiyo mpya iliyotokana na kugawanywa kwa iliyokuwapo awali ya mama ya Pare.
Akizungumza na Mwananchi, leo Alhamisi Machi 6,2025, Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mwanga, Mathias Msemo amesema mkutano mkuu maalumu utafanyika Jumatatu Machi 10, 2025, na utakuwa na ajenda moja ya uchaguzi.
"Uchaguzi wa Askofu ni Jumatatu Machi 10, 2025, na usingetokea ule msiba kusingekuwepo na uchaguzi, kwani Askofu Sendoro bado alikuwa hajamaliza kipindi chake, alishahudumu kwa miaka minane," amesema Katibu Mkuu.
Aidha amesema kwa taratibu zilizopo, Askofu anakaa madarakani kwa kipindi cha miaka 10 na baada ya hapo unafanyika mkutano mkuu ambapo anapigiwa kura ya imani na akishinda anahudumu hadi umri wa kustaafu.
"Kwa taratibu zetu Askofu anakaa miaka 10 na baada ya miaka hiyo anapigiwa kura ya imani akishinda anakaa hadi muda wa kustaafu, na wakati anafariki Askofu Sendoro alikuwa amekaa miaka minane na alikuwa aende mpaka 2026, ndipo ufanyike mkutano mkuu apigiwe kura ya imani," amesema Msemo.
Amesema kwa mujibu wa katiba umri wa kustaafu Askofu ni miaka 65 kwa hiari na kwa lazima ni miaka 70.

Haya hapa matamanio ya Wachungaji
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti baadhi ya wachungaji wa Dayosisi hiyo, wameeleza namna miaka minane ya Askofu Sendoro ilivyokuwa ya mafanikio na kusema kuwa, wanatamani kumpata Askofu mpya ambaye ataweza kuvaa viatu vya mtangulizi wake.
Mkuu wa Jimbo la Mision la dayosisi hiyo, Mchungaji Deogratius Msangi amesema wanaendelea kumuomba Mungu, ili awape Askofu ambaye atasimama vyema kwenye nafasi hiyo na kuendeleza huduma ambazo zilianzishwa na Askofu Sendoro enzi za uhai wake.
 
Back
Top Bottom