Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Yohana Mbatizaji naomba unijibu swali langu- Sheikh Sharif Majini nae ni kiongozi wa dini???

Hao ni wafanyabiashara wa Dini sio viongozi wa Dini!!
 
Hujui......Yeyote akiwa upande wetu, huyo siyo kinyume chetu....sijui.....Watu mnawafokea viongozi wa dini bure, wakati hamjapewa madaraka ya nchi mmetangaza maombi kwa njia ya Mungu katika karne ya sasa ni upuuzi! Vilevile wanasema vitabu vya dini vipo duniani kuwapumbaza watu! Hata hivyo wacheni kuwa wanafiki, viongozi wa dini wakiwa upande wenu hapo hakuna shida ( Mchungaji Msigwa), sasa je! Na yeye waumini wake si watagawanyika? Wasimpe sadaka! Tufike mahali wa TZ tuache unafiki, Ohoo! Rais gani huyu hata havumilii na kuyatendea kazi mawazo ya watanzania....na sasa tuone kama na nyinyi mtavumilia na kuyatendea kazi mawazo ya viongozi wa dini, hapo tutajua nani ni MNAFIKI.
 
Viongozi wa dini sisi waumini tupo nyuma yenu.nyinyi mnaongozwa na roho wa Mungu,mema mnayofanya hakika ni miongozo iliyobarikiwa na Muumba mbingu na nchi.
Mungu awaongoze mzidishie upendo wenu kwa Rais wetu kipenzi JPM.
Hata Hitler wakati wa utawala wake walikuwepo waliojiita viongozi wa dini waliokuwa wanatumika kumsifu na kumuabudu Hitler na wauaji wenzake
 
Hutaki Serikali iseme mazuri yake?
Ni vizuri kusema/kusemwa mazuri yake lakini ikubali kusemwa mabaya yake ili kujirekebisha. wakitokea viongozi wengine wa dini wakakosoa mabaya yake wasisemwe kuwa wanafanya siasa na wakakamatwa na kutiwa ndani pamoja na kufunguliwa kesi. Ni bora mtu akuseme mabaya ili ujirekebishe kwani mazuri yanaonekana na hakuna haja sana kuyasemea.
 
Wote hao kina Malasusa na Sheikh Hadji wamekuwa "blackmail catch" , mfano Malasusa is paying for his "sex scandals" while Hadji was fixed in his 'sodomy scandal" , jamaa wahuni sana ....waliwafix halafu baadaye wakajifanya wanawasaidia ....so they are now in slavery ...hawawezi kufanya jambo tofauti na hapo .
 
Hata kama wanachofanya ni sahihii lakini sio WAKATI sahii hata kidogo. Na wao ilibidi walione hilo, maana sasa wanakuwa kama sehemu ya kampeni kitu ambacho kimetia doa sana mkutano huu. Kama ni kumshukuru walishafanya sana sasa mkutano huu haukuwa muda wake.
 
Hivi huyu Kakobe alishapewa urai wa Tanzania?
 
Hakuna viongozi wa dini hapo hao ni viongozi wa matumbo yao tu.
 
naomba mnijuze kama kanisa katoliki lipo hapo unafikini...
Watanzania tumeuliwa
Watanzania tumetekwa
Watanzania tumedhulimiwa mali zetu kinyume cha sheria na taratibu...

Kama kweli Mama Kanisa Katoliki yupo kwenye huo udhulumati nijulisheni, sintokaa nikanyage tena kanisani na hata nikikanyaga hawatokaa waine shillingi tano yangu

Watanzania wanyimeni sadaka na zaka hawa wahuni; wanakula sadaka wanavimbiwa na kwa dharau wanatutapikia ufundo mtupo sisi tunaowashibisha kwa sadaka zetu tunazoziokoteza kwa jasho na damu katikati ya mateso na dhuluma za serikali hii. Watanzania tuwakataeni..Sadaka iwe mwiko kutoa na hata makanisani tuasi kwenda. tuchukue hatua sasa.

Naomba watu wote wema na wapenda haki tufanye kampeni kabambe ya kuzikataa hizi dini fake...madhulumati wakubwa.
 
Njaa mbaya sana.
Si vibayakwa viongozi wa dini kuwaombea na kuwashauri viongoziwa serikali. Tatizo hapa ni kwamba sehemu kubwa ya hawa viongozi wa dini wanajipendekeza kwa serikali hili kulinda matumbo yao na si vinginevyo.
Pia si vibaya hao viongozi kuwa wanachama wa chama fulani, lakini kutokana na wajibu wao kwa wahumini wao, ingekuwa vizuri kutoegemea upande wowote kwani wahumini wao ni wanachama wa vya tofauti, sasa wanapoonesha uelekeo fulani, itawagawawahumini wao
 
Lipo
 
Tukiacha kutoa sadaka watatia akili,kwanza ni wahujumu uchumi wanakusanya mapato bila kulipa kodi.
 
Na turudi kwenye dini zetu za asili maana sasa huu ni utopolo
yan kabisa. nakuhakikishia sisi ndo tunaowapa kiburi hawa wezi na madhulumati..tunawapa pesa wanakula mpaka wanavimbiwa halafu wanatuona mapimbi sisi tunaoteswa na mifumo kandamizi. mwenye shibe hamjui mwenye njaa..hawajui tunavoumizwa sababu wao hawaumii kutafuta chakula..ni sisi ndiyo tunaowapelekea...dawa ni kuwanyima na kujitenga nao.
 
Mungu wa isacka,Yacobo,Yohana ndo Mungu aliewapa hekima na busara viongozi wetu wa dini kuamua kukutana na Rais wetu kipenzi Rais Magufuli.
Yangefanyika haya wakati wa kumuaga ingekuwa ni sawa kabisaa.Lakini kuyafanya eti anaelekea uchaguzi(rejea kichwa cha habari cha mkutano) ni jambo baya sana dini kuonyesha upande zilikolalia kisiasa!!
 
Wangezuga tu kwenye dhumuni la mkutano kua ni kuliombea taifa kuelekea uchaguzi. Ingeweka mambo sawa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…