Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Askofu wangu Ruwaichi nae yupo? RC wamepeleka mwakilishi? Kama wapo nitapunguza zaka na sadaka kanisani..nitaongeza nguvu kwa vituo vya watoto yatima! Shame on them...
 
Ukweli viongozi wa dini wamefanya jambo la hovyo sana . Kwanza hawakupaswa kuwa hivyo
Lazima kuna kitu kikubwa nyuma ya pazia, ambacho mimi na wewe hatukijui. Sisi tunawaona wana siasa maarufu akina Magufuli na akina Tundu Lissu; wao wanaona zaidi ya hapo, na wanajua zaidi ya hayo. Muwe mnaangalia matukio. Usiku wa tarehe 12.08.2020 kumetokea nini? Mnakula maandazi tu bila hata kuangalia mambo mengine yanakwendaje?
 
Lazima kuna kitu kikubwa nyuma ya pazia, ambacho mimi na wewe hatukijui. Sisi tunawaona wana siasa maarufu akina Magufuli na akina Tundu Lissu; wao wanaona zaidi ya hapo, na wanajua zaidi ya hayo. Muwe mnaangalia matukio. Usiku wa tarehe 12.08.2020 kumetokea nini? Mnakula maandazi tu bila hata kuangalia mambo mengine yanakwendaje?
wanaona nini bana na wewe!! hamna lolote ni ubatili tu. watu , wanatekwa wanauliwa wanapotezwa hawasemi lolote leo useme eti kuna wanaloliona?! lipi hilo zaidi ya uhai?
 
Ni vizuri kusema/kusemwa mazuri yake lakini ikubali kusemwa mabaya yake ili kujirekebisha. wakitokea viongozi wengine wa dini wakakosoa mabaya yake wasisemwe kuwa wanafanya siasa na wakakamatwa na kutiwa ndani pamoja na kufunguliwa kesi. Ni bora mtu akuseme mabaya ili ujirekebishe kwani mazuri yanaonekana na hakuna haja sana kuyasemea.
Umenena vema mkuu.
Ukipenda misifa, ukubali pia kukosolewa.
 
johnthebaptist
1597742932086.png
 
Ndomana nilishaachaga KWNDA kwenye makanisa yao

Ova
 
Sikuwaona mkuu
nitamshukuru sana Mungu kama ni kweli RC wamejitenga na uovu huu. Kwa historia ndefu na mapito lukuki ya imani Katoliki ni aibu na fedheha kubwa kwa Mama Kanisa Katoliki kujihusisha kwenye aibu za aina hii. Acha hao kina kakobe wafanye haiumi sana lakini si Mama Kanisa Katoliki
 
Go to God yourself, achana na watu wanaoitwa viongozi wa dini, tunahitaji viongozi wa kiroho and we know them.
 
Tunalo tatizo kubwa kuliko tunavyoweza kulielezea kwa maneno. Mungu atunusuru.
 
Hilo kongamano limenisikitisha sana. Ni dhahiri viongozi wa dini wanaonesha upande. Namuunga mkono JPM lakini hii ni too much. JPM hahitaji yote haya kushinda

Hii ni kufuru kwa taifa hili. JPM anapiganiwa na watu wenye ufahamu mdogo sana; wahuni na watu wanaotumia nguvu badala ya hoja na ushawishi wa kisiasa. Matokeo yake wanadhalilisha na kunajisi nchi yetu. Kwa hakika wana ccm asilia hawakutegemea chama chao kufika hapa.
 
Hao viongozi wa dini wanatakiwa kujua kua Mungu ndio aliye na wafuasi wengi kuliko wafuasi wa hao viongozi wa dini. Ko wasidhani kua kwenye makanisa wanaweza kufanya biashara zao za siasa
 
Back
Top Bottom