Mkutano wa waandishi: Lipumba, Shelukindo, TANESCO na PPRA



wallllllllllllllllaaaaaaaaaahhhhhhhhhh
 
2010.....2010.....2010......2010.....2010......2010.....2010......2010.....
2010.....2010.....2010......2010.....2010......2010.....2010......2010......

Pesa tutapata wapi????? 1995 Mwalimu Nyerere na Mwinyi walipata wapi? 2000 Mkapa alipata wapi? 2005 zilitoka wapi? Sasa 2010 zitatoka wapi?

MADARAKA, PESA!!!!!! HATARI TUPU
 

Sasa mpiganaji wetu mzalendo ,mkereketwa wa nchi ZITTO KABWE ,naye anatafuta fedha za 2010 ama anapigania maslahi ya Taifa.

Teh teh teh teh teh teh teh teh teh.

Angalia watakuja nakusema mimi ndiye mimi ndiye watafanya miujiza mingi ili mpate kuwaamini NA tazama watabadirisha mawe nakuwa mikate ,wahatakisha hata milima LAKINI tazama kuweni wenye akili kama nyoka.Mmepewa masikio ya kusikia,macho ya kuona na akili ya kutambuwa mema na mabaya.

Sasa kama ndivyo tutamtambuwa je mtu huyu? Kwa matunda yake.
 

Najua mwanakijiji utakuwa umefura sana.Nina hakika akili yako imeja DOWANS isununuliwe na Dowans itanunuliwa kwa kuwa wakubwa wanataka(Hisia Zako)!


Lipumba kaona haja ya kununuliwa mitambo hiyo na mie nazidi kuunga mkono mitambo hiyo inunuliwe.

Niliongea na zitto toka kipindi kile alivyokuwa akiunga mkono suaa hili,alinipa hoja zake za msingi na mie nikapiga ndodo zaidi ili kujua nini tatizo na nikakubaliana naye kuwa kuna haja ya kununua mitambo ya Dowans.

Mie naona Mitambo inunuliwe tu ili mjomba na watanzania wengine waisingie Gizani!Mwanakijiji hauna sababu ya singi ya kukata kunuliwa mitambo hiyo ,umeng'ang'ana kuwa mitambo hiyo imeletwa na tapeli ,inaonesha tatizo siyo mitambo ila tatizo ni mitambo imeletwa na Tapeli..tatizo imeletwa na Rostam(Hakuna ushahidi).yaani kila jmbo wewe lazima uone ni baya?

Tukiendelea kuishi kwa kuhisi kila jambo kuna ufisadi basi nchi haitafika mbali!
 

Unajua wana hisa wa Dowans Tanzania Limited? Tatizo langu si mitambo kwani wakiitaka waichukue kwa nguvu, tatizo langu ni kuinunua kutoka kwa tapeli. Wewe huoni tatizo hilo. Kwako, mtu ambaye amekuibia na bado anakuibia uko tayari kuendelea kununua kutoka kwake alimradi utatue tatizo ambalo unaweza kulitatua bila kununua kutoka kwake. Hii ndiyo tofauti.

Mmiliki mwenyewe wa Dowans kasema aliyepeleka ujumbe wa yeye kuleta majenereta ni Rostam na Rostam alifanya hivyo kwa maelekezo ya Kikwete. Watanzania (kupitia viongozi wao) ndiyo wanadaiwa kutaka alete mitambo hiyo. Walipoileta walimuahidi kuwa mwishoni mwa mkataba watainunua. Sasa mkataba haupo, na majenereta hayajanunuliwa.

Jamaa anawadai, personally na kama serikali kwa kumuingiza mkenge. Urafiki wao na yeye uko mashakani. Na sasa watawala hawana lolote isipokuwa kusema tu tununue.

Mimi nasema tuichukue mitambo hiyo kwani tunaiihitaji, kwanini tuinunue?
 
Merekebisho.... Zitto hakuwapo... Walikuwapo watu wa Tanesco na Lipumba...

Lipumba alianza na kuzungumzia hali ya uchumi then suala la Dowans likaja baadaye.
 
Merekebisho.... Zitto hakuwapo... Walikuwapo watu wa Tanesco na Lipumba...

Lipumba alianza na kuzungumzia hali ya uchumi then suala la Dowans likaja baadaye.

Sasa Zitto naye atakuwa ameandaa mkutano wake binafsi?
 

Oooh mchango mzuri sana. Ile shahada ya pili si haba. Mitambo lazima inunuliwe, hisani lazima ilipwe

Mambo kama Afrika Kusini

......ndiyohiyo
 

sasa Mwanakijiji,

Wat is your Problem?wewe ni nani hasa wa kukata tu jambo lisifanyike,unazungumza kwa niaba ya nani?kama tukifika sehemu kuwa kama Mwanakijiji( au wanasiasa flani) akisema hiki kisifanyike na kweli kikaachwa basi nchi itakuwa ikiendeshwa kienyeji sana.
 

Mitambo ya Dowans haipaswi kununuliwa; watueleze kwanza muuzaji nani? Anauza kwa bei gani? Tupate tathmini huru ya ubora wa mitambo kwanza. Lakini kwanini tupotezeane muda wote huo wakati tunaweza kununua mitambo mipya? Wizi mtupu huu!

Tuwasomee dua mahayawani wote wasio na haya

Asha
 

Katika yale makaratasi ya BRELA wamiliki wa DOWANSa ni Brigedia mstaafu peke yake?au kuna wengine?

unachotakiwa ni kuwa jasiri na kutaja kuwa ni flani na flani wanahusika na dili.ulilshasema kuna Mkulu ,RA,Mwingine ni nani?na ulete vithibitisho
 

Hata bila kununuwa mitambo mipya,hiyo fedha wakiitumia kukarabati mabwawa yetu yaliyopo inatosha kabisa umeme na kusaza.

Mosi. Udhalula uliopo ni wa kutengenezwa si kweli ,wanafanya makusudi kabisa ili wapate uhalali wa kufanya biashara na UFISADI.

Pili. Tanzania haina viwanda na watumiaji asilimia 98% ni wawasha taa tu kwa masaa mawili matatu.
Hivyo kwa asilimia 99.9999% Tz haiwezi kuwa na udhalula wowote wa umeme

Watuite sisi ma Engineer huru tukafanye Tathimini ya udhalula wa umeme,wasituandalie propaganda zao ktk makaratasi bali twende kabisa huko jikoni tuone tufanye tathimini na tahimini ya matumizi ya umeme kwenye HIGH Peek.
Mimi sidhani kwa mabwawa tuliyonayo na watumiaji wa watanzania kuna udhalula wowote.

Akina Zitto tatizo nasiasa tu walizoandaliwa anaongelea mambo ya Technical Know how wakati yeye ni mwanasiasa ndio maana kunasehemu alikuwa anasema SOCKET BREAKER badala ya CIRCUIT BREAKER.
 
Oooh mchango mzuri sana. Ile shahada ya pili si haba. Mitambo lazima inunuliwe, hisani lazima ilipwe

Mambo kama Afrika Kusini

......ndiyohiyo

Una maana gani kuandika hivi kwa Gembe?. Fafanua tusiojua tujue kuna nini?.
 
Achaneni na Lipumba. Mambo ya Al Adawi kamuulizeni Maalim Seif na Ismail Jussa. Uchaguzi 2010 uko karibu. Haba na haba hujaza kibaba. Karume fungua macho. Kikwete ameshafika

PM
 
jussa huyo ana undugu ya yule jussa wa flamingo restaurant ya uwanja wa ndege wa nyerere ??
 

mbona nimesema nini kifanyike!? au hujaona hapo?
 
Katika yale makaratasi ya BRELA wamiliki wa DOWANSa ni Brigedia mstaafu peke yake?au kuna wengine?

unachotakiwa ni kuwa jasiri na kutaja kuwa ni flani na flani wanahusika na dili.ulilshasema kuna Mkulu ,RA,Mwingine ni nani?na ulete vithibitisho

hapana.. nimesema wenye hisa; zile ni fomu zinaonesha mkurugenzi na usajili.. angalia fomu zinazoonesha hisa kama zile zilizotolewa kuhusu Mwakyembe...
 
Watu hawajui kuwa Al-Adawi ni mzaliwa wa Zanzibar pia; kuna maslahi makubwa tu kwa yeye kuleta hayo majenereta na KULIPWA! Kikwete kabanwa..
 
Huyo ni Lipumba amesha mwaga hoja. Bado PPRA na Zitto nao si watazungumza na wahariri leo leo na kumwaga hoja? Hongera Ngeleja na Dr Iddrissa, nchi haipaswi kuwa gizani kwa sababu ya ushabiki wa wakina Mwakyembe.........ndiyohiyo

Kama Lipumba ameamua mitambo inunuliwe basi ameshaona ipo haja ya kununuliwa na tusilete ubishi kwani WaTz wenyewe huwa wananunuaga vyombo vya wizi na kuwafaa.Chenye matattizo si Mitambo ni mikataba ,mikataba imevunjwa mitambo imekaa inapigwa na mvua ,ikiwa wenye mitambo watauza kwanini isinunuliwe ,najua mtasema sheria haziruhusu kununua second handa items au mitumba lakini hii si mitumba ni mitambo ambayo ililetwa kwa ajili yetu.

Na jingine Lipumba ni mtu wa mawazo yenye kutazama kwa kina hapa WaChadema lazima muone umoja wa upinzani kama Lipumba ameonelea ipo haja ya kuinunua mitambo hiyo basi ni moja kwa moja anaungana na Zitto au anampa sapoti Zito ,kwa kuonyesha umoja huo kuwa ulazima wa kuwepo pamoja ni kitu kinachotakiwa katika kupambana na CCM. Lipumba angeweza kurapu na kumuweka Zitto pabaya zaidi.

Natumai kabisa pindipo Lipumba atabana kwenye ununuaji basi Zitto Kabwe atapata afuweni kwa kiasi fulani na hivyo kumfanya Lipumba aonekane ni defender.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…