Mkutano wa waandishi: Lipumba, Shelukindo, TANESCO na PPRA

Mkutano wa waandishi: Lipumba, Shelukindo, TANESCO na PPRA

There appears to be something seriously wrong with the logic of the TANESCO officials - to go now to buy heavy oil generators wakati nchi ina plenty of natural gas is to say the least ridiculous. Further gas turbines are much easier to manufacture on order than the heavy oil ones especially the one of 100MW capacity! Also use of gas turbines is prefered from an environmental perspective.
UFISADI!

Mjadala ungekuwa unaenda na maoni timilifu yenye kujenga kama haya nina uhakika tungekuwa mbali sana.

Ni wazi itakuwa ni makosa kufunga mtambo wa kutumia dizeli Dar Es Salaam wakati kuna urahisi na unafuu wa kupata GESI ya kuaminika. Inashangaza kama hawa jamaa watafunga mitambo ya mafuta wakati tayari wanabadilisha mitambo mingine iliyokuwa ikitumia MAFUTA kwenda kwenye kutumi GESI. Hili inabidi walieleze zaidi labda wana sababu za kimsingi kufanya hivyo.

omarilyas
 
Last edited:
Hayo majibu yako, tuwekee na alivyojibu JK ili turidhike na kauli zako otherwise tutaona kama una chuki za ''agenda za siri''.


Nadhani hujasikiliza hayo majibu, sijui lilikuwa ni swali gumu kwake au hakulielewa vyama au majibu alotoa ndo ukomo wa mikakati yake?!

Kwamba nina agenda za siri?

Sina.
Kama nina mpango wa kumpiga risasi mtu huwa nasema bila kusita.
Sioni cha kunifanya niwe na agenda ya siri huku sirini.


MH Dar Es Salaam,
Hebu pata Is and Was kutoka kwa MH JMK akifafanua kwa ufasaha kabisa namna nchi ya Tanzania chini ya uongozi na mwongozo kutoka kwake ilivyojidhatiti kuinua uwekezaji katika sekta binafsi.


http://www.changes-challenges.org/concluding-plenary
 
Last edited:
profesa Lipumba anapozungumza: Hatuwezi kukwepa kununua mitambo chakavu

2009-03-21 11:24:27
Na Muhibu Said


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Sheria ya Manunuzi ya Umma, haikuzingatia taratibu na mikakati ya kibiashara kupiga marufuku ununuzi wa mitambo chakavu kwa mashirika ya umma.

Profesa Lipumba alisema hayo alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Sakina Datoo, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema nchi zote zilizo nyuma katika maendeleo ya viwanda, hutumia mashine na mitambo iliyotumiwa sehemu nyingine, tofauti na sheria hiyo inavyotaka.

``Makampuni huhamisha mitambo iliyotumiwa nchi moja na kutumiwa nchi nyingine. Huu ni uzoefu wa kawaida. Katika kuendesha mashirika ya umma ya kibiashara ni muhimu kuzingatia faida inayopimwa na benefit Cost Ratio na Internal rate of return ya uwekezaji,`` alisema Lipumba.

Kutokana na hali hiyo, alisema kama sekta binafsi ingebanwa kuwa lazima inunue mitambo na mashine mpya katika uwekezaji wake wote, shughuli nyingi za uzalishaji bidhaa na huduma zisingefanyika.

Katika mazungumzo yake na wahariri jana, Lipumba ambaye alitilia mkazo kuwapo kwa mjadala wa kitaifa juu ya athari za mgogoro wa uchumi duniani kwa uchumi wa Tanzania na mikakati ya kujikwamua, alisema utawala bora unahitaji Bunge lisimamie na kuyawajibisha mashirika ya umma kuhusu mambo ya sera na kuchambua ufanisi wake wa jumla na kwamba, halipaswi kuingia jikoni kuamua mambo ya kiutendaji.

Alisema ukosefu wa uongozi nchini, unajidhihirisha wazi katika sakata la hivi sasa la Tanesco, ambapo mapande ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yanalipotosha na kuliyumbisha taifa katika masuala mazito ya kutokuwa na mpango mahsusi wa taifa unaotekelezwa na shirika hilo wa kuzalisha na kusambaza umeme.

Lipumba alisema badala ya kujadili mbinu za muda mfupi, kati na mrefu wa kuongeza uzalishaji wa umeme, makundi ya CCM yanaendeleza vita vyao vya kugombania madaraka na maslahi ya kibiashara.

``Mbunge wa CCM unamsikia anaushambulia ufisadi unafikiria labda bado wapo wanaotetea maslahi ya taifa, kumbe naye ana maslahi binafsi anayoyaficha,`` alisema Profesa Lipumba.

Pia, alisema mkakati wa kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza nchini, unahitaji kuwa na Bodi huru ya Tanesco inayofanya kazi kitaalamu na kwa maslahi ya taifa kuisimamia
 
Na Stanislaus Kirobo

MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amejitosa katika sakata la ununuzi wa mitambo ya Dowans.

Katika kauli yake wiki mbili zilizopita, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kupitia Jukwa la Wahariri, Prof. Lipumba alijenga hoja yake kwa kutoa sababu za kiuchumi – kikubwa ni kwamba nchi zote zilizo nyuma katika maendeleo ya viwanda hutumia mashine na mitambo iliyotumika sehemu nyingine.

Alisema, “Hatuwezi kukwepa kununua mitambo chakavu. Makampuni huhamisha mitambo iliyotumiwa nchi moja na kutumiwa nchi nyingine, na huu ni uzoefu wa kawaida.”

Prof. Lipumba alisema katika kuendesha mashirika ya umma ya kibiashara ni muhimu kuzingatia “faida inayopimwa kwa uwiano wa gharama kwa mwekezaji.”

Katika hoja yake, Lipumba amezingatia zaidi suala la mitambo ya Dowans “kibiashara” na “kifaida” kuliko suala lingine lolote.

Kwa maneno mengine, anatazama mitambo ya Dowans kama mitambo iliyopo sasa Ubungo; hataki kabisa kuangalia historia nzima na hasa ujio wa kampuni hiyo na utata wa miliki yake.

Kwa maneno mengine, hataki kuliangalia suala hilo kama linahusika na “ufisadi,” “kashfa” au “uovu” mwingine wowote uliotendeka huko nyuma hadi kusababisha kuwepo kwa kampuni ya Dowans.

Pamoja na kulitizama suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans kibiashara, bila shaka Lipumba anatambua kuwa kauli yake ya kuunga mkono imewafurahisha wale watakaonufaika na ununuzi wa mitambo hiyo – yaani mafisadi.

Inashangaza kuona profesa huyo aliyebobea katika mambo ya uchumi hataki kuliangalia suala hilo kama sehemu ya mgogoro ,kubwa na hata vita dhidi ya ufisadi nchini.

Hana habari, au hataki kuzingatia kwamba kampuni hiyo ni mtoto wa kampuni ya kifisadi ya Richmond iliyopigiwa kelele nyingi, kutikisa nchi na kusababisha kujiuzulu mawaziri watatu akiwemo waziri mkuu.

Isitoshe kuna maafisa wakuu wawili wa serikali wengine ambao walidhihirika kuhusika na sakata lenyewe na ambao serikali iliagizwa na Bunge kuwachukulia hatua lakini hadi sasa serikali haijafanya hivyo. Anayejua sababu za kutotenda ni serikali yenyewe.

Ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii kwa waziri mkuu kujiuzulu kutokana na kashfa; tukio ambalo lilionyesha uzito wa ufisadi ulivyofanyika.

Hili pia Lipumba hakutaka kulitia maanani wakati anatoa kauli yake hiyo ambayo bila shaka imewavunja moyo baadhi ya watu katika mapambano haya dhidi ya ufisadi.

Mtazamo wa Lipumba ni kwamba Dowans ichukuliwe kama Dowans tu, mengine yote hayo ni siasa. Nadhani Profesa amesahau kitu kimoja: Vita vyovyote vya dhati dhidi ya ufisadi lazima viendeshwe kimaadili na vizingatie miiko. Bila hivyo, itaonekana ni dhihaka na havitafika popote.

Hakuna maadili yoyote kwa serikali kuamua ghafla kutathmini kitu ambacho tayari ilishaamua kuwa ni uchafu.

Ni kama vile lori lililokamatwa kwa kusheheni pembe za ndovu au nyara nyingine za serikali na mwenyewe kuhukumiwa kufungwa – halafu serikali inakuwa tayari kununua lori lake ili kumsaidia.

Au jambazi aliyethibitika kunyan’ganya na kuua na baadaye kufungwa, halafu serikali ikawa tayari kununua nyumba yake ili kumsaidia. Tungekubali iwapo serikali ingetafuta namna au vipengele vya kutaifisha mitambo hiyo yenye harufu mbaya ya rushwa kuliko kuinunua.

Aidha, hata kama haiwezekani kukwepa kununua mitambo chakavu, lakini siyo lazima kununua hii ya Dowans ambayo hata utaratibu wake wa kuingizwa nchini ulighubikwa na udanganyifu.

Si vyema inunuliwe mitambo mingine basi, chakavu kama sheria/kanuni ya serikali ya ununuzi itapindishwa au kurekebishwa? Inunue mitambo isiyokuwa imetia dosari na kuitikisa serikali na nchi nzima.

Serikali lazime ionyeshe angalau kaujeuri ka-kuzingatia maadili na heshima katika kuendesha vita hii ya ufisadi na masuala yanayotokana nayo. Hakuna haja ya serikali kuonekana kuwapa ahueni mafisadi.

Kwani leo hii, serikali ikiwaambia Dowans waondoe mitambo yao ndani ya miezi miwili ama sivyo itakokotwa na kuwekwa nje, itakuwa na kosa gani? Kwa nini serikali inakuwa na woga mkubwa katika masuala ya msingi?

Na hapa bado sijazungumzia suala la umiliki wa mitambo – yaani nani mmiliki. Kwa muda mrefu mmiliki alikuwa hajulikani. Lakini ajabu ni kwamba lilipozuka tu suala la ununuzi, ikabidi mmiliki aundwe au atangazwe ili apatikane wa kufanya biashara na serikali.

Wiki iliyopita gazeti hili liliandika kuwa mtu mmoja, raia wa Oman, anayedai kuwa mmiliki wa mitambo hiyo, hapo awali aliwahi kuikana kampuni hiyo, kwamba wala haiijui. Ushahidi upo. Na hadi sasa hajasema chochote kuhusu kusutwa huko.

Hili suala nalo limeongezea dosari hoja hiyo ya Lipumba na kuipa nguvu ile kambi inayopinga ununuzi, kwani inaonekana kwamba suala zima ni mwendelezo wa ulaghai wa awali kupitia Richmond.

Inavyoonekana, masuala ya ufisadi siyo anga za Lipumba na ndiyo maana CUF haishupalii sana suala hili kama vile Chadema. Inawezekana ni kwa sababu Lipumba amebanwa sana na suala la muafaka kiasi kwamba hana muda kushughulikia masuala ya aina hii.

Tayari baadhi ya wadadisi wanaona kauli ya Prof. Lipumba inaweza kupunguza mvuto na guvu ya chama chake. Kuna haja ya kutafiti alikojikwaa na kwa nini.
 
Huyu ndie Lipumba

BRIEF RESUME
Professor Nguyuru Haruna Ibrahim LIPUMBA
Senior Research Fellow
The Multi-Environmental Society (MESO)
P.O. Box 70949
Dar Es Salaam,
Tanzania.

Field of expertise: International Trade and Finance, Macroeconomics
Development Economics and Agricultural Economics.
Current research focus: (1) Impact of Liberalization of Foreign Exchange and
Other Financial Markets on Economic Development in Sub-Saharan Africa. (2)
Globalization and Economic Development in Sub Sahara Africa (3) Policies to
Promote Growth in Sub Sahara Africa.
Date of Birth: 6th June 1952

Education:
1978-83 Ph.D Economics, Stanford University, Stanford, CA 94305
1977-78 M.A. Economics, Stanford University, Stanford, CA 94305
1976-78 M.A. Economics, Faculty of Arts and Social Sciences
1973-76 B.A. (Hons) Economics, University of Dar es Salaam

Academic Honors:
1977-1983, Rockefeller Foundation Fellowship

1986-1989, Kellog International Fellow in Food Systems

1976, Best Student Award, Faculty of Arts and Social Sciences, University of
Dar es Salaam

Employment:
1999- Independent Consultant, Dar es Salaam

1996-1998, Senior Research Fellow at the World Institute for Development
Economics Research, UNU/WIDER, Finland.

1993-1995, Fullbright Visiting Professor, Centre for Development Economics
Williams College, USA.

1991-1993, Personal Assistant to the President (Economic Affairs) i.e.
Economic Advisor to the President of the United Republic of Tanzania.

1989-1996, Associate Professor Department of Economics, University of Dar es
Salaam.

1996-1998, Senior Research Fellow, World Institute of Development
Economics Research, United Nations University, Helsinki, Finland.

Consultant to
The World Bank, UNDP, Global Coalition for Africa, Preferential Trade Area
for Eastern and Southern Africa (now COMESA), Swedish International

Development Agency (SIDA), NORAD, DANIDA, Ministry of Foreign Affairs
Finland, Bank of Tanzania, Macroeconomic and Financial Management

Institute of Eastern and Southern Africa, African Capacity Building Foundation.

Other Responsibilities:
2000, Presidential Candidate, Civil United Front, General Election of the
United Republic of Tanzania, General Election October 2000.

1999- Present, Chairman, Civic United Front, a Liberal Democratic political
party in Tanzania.

1996-1998 Visiting Professor of Development Economics, University of
Helsinki.

1995, Presidential Candidate, Civil United Front, General Election of the
United Republic of Tanzania, General Election October 1995.

1995-Present, Member United Nations Committee for Development Policy.

1993, Chairman, Probe Committee on the Management and Leadership crisis
facing the National Insurance Corporation.

1992, Chairman, Presidential Commission of Enquiry on the financial problems
of Shinyanga Region Cooperative Union.

1991-1993, Commissioner, Presidential Commission on Parastatal Sector
Reform, Dar es Salaam, Tanzania.

1990-1993, Chairman, Board of Directors, Imara Wood Industries, Moshi,
Tanzania.

1990-1993, Member, Board of Directors Tanzania Wood Industries Corporation
TWICO, Dar es Salaam, Tanzania.

1992-1993, Member, Board of Directors, National Insurance Corporation, Dar
es Salaam, Tanzania

1990-1993, Member, Board of Directors, Tanzania Karatasi Associated
Industries (TKAI), Dar es Salaam, Tanzania.

Selected Publications:
Stabilization Policies in Tanzania, University of Dar es Salaam, 1984.

African Unity, Some Practical Guidelines, MAWAZO Vol. 1. No. 2, May 1983.
Published by Stanford African Students Association.

Problems and Prospects of African Economic Integration , MAWAZO Vol. 1.
No. 1, April 1982.

The Brandt Commission Report: A General Overview, Journal of Economic
Reflections, January 1982.

Book Review, R. H. Green (et al.) Economic Shocks and National Policy
Making. Tanzania in the 1970s. UCHUMI Journal of the Economic Society of
Tanzania.

The Economic Crisis and Basic Needs in Tanzania, ILO Basic Needs and
Development in Tanzania 1983 Addis Ababa.

Basic Needs and Agricultural Development Policy: A Critical Review. ILO
Basic Needs and Development in Tanzania. 1983 Addis Ababa.

"Macroeconomic Management of the Tanzania Economy", International
Development Research Centre. The Zambian Economy: Problems and Prospects
1984.

"Policy Reforms for Economic Development in Tanzania", published in
Stephen K. Commins (ed.) Africa Development Challenge and the World Bank.
Lynne Rienner Publishers. Boulder/London. 1988.

"The Global Trading System and Economic Development of Tanzania" in John
Whalley (ed.) Dealing with the North. Centre for the Study of International
Economic Relations (London, University of Western Ontario) 1987.

"Domestic Supply Constraints versus Market Access Problem in International
Trade and Economic Development of Tanzania" in John Whalley (ed.) The
Small Among the Big. Centre for the Study of International Economic Relations
(London, University of Western Ontario).

"A Supply Constrained Macroeconometric Model of Tanzania" Economic
Modelling Vol. 5 No. 4. October 1988 with Ndulu, Horton and Plourde.

"Market Liberalization and Food Security in Tanzania", with Amani, Ndulu and
Kapunda. Proceedings of SADCC Food Security Conference Harare 1987.

"The Arusha Declaration and Economic Development of Tanzania", in
Hartmann, J. The Arusha Declaration Twenty Years After (Copenhagen Centre
for Development Research) 1990.

"Reflections on Economic Development in Tanzania", in UCHUMI Journal of
Economic Society of Tanzania 1987.

The Impact of Market Liberalization on Household Food Security, with Amani,
Ndulu and Kapunda. SADCC Conference on Food Security Conference
Proceedings. 1988.

Reflections on Long Term Development Strategy in Tanzania, in World Bank
Sub-Saharan Africa: From Crisis to Sustainable Growth A Long Term
Perspective Study, Vol. I. 1990.

The Record and Prospects of the Preferential Trade Area of Eastern and
Southern African States in Chhibber Ajay and Stanley Fischer Economic
Reform in Sub-Saharan Africa World Bank 1991.

Determinants of Appropriate Exchange Rate, in UNDP Aspects of Exchange
Rate Determination United Nations, New York 1991.

Exchange Rate Policy in Tanzania, UNDP, Stabilization and Adjustment United
Nations, New York 1991.

Tanzania: Medium Term Development Issue and Prospects, African
Development Bank, African Development Report 1994.

Structural Adjustment Policies and the Economic Performance of African
Countries.

United Nations Conference on Trade and Development International Monetary
and Financial Issues for the 1990s. Vol. V. 1995.

African Beyond Adjustment, Policy Essay No. 15 Overseas Development
Council Washington, D.C. 1994.

"Financing Long Term Development in Sub-Sahara Africa" in Culpeper Roy,
Caroline Pesteau, IDRC, Development and Global Governance 1995.

"The Liberalization of Foreign Exchange Markets and Economic Growth in
Sub-Sahara Africa" UNU/WIDER Research for Action No. 35, 1997.

"An evaluation of the institutional set up and technical capacity of the Ministry
of Finance - Namibia." A Consultancy Report to The Macroeconomic and
Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa (MEFMI) 1998

"An evaluation of the institutional set up and technical capacity of the Ministry
of Finance - The Kingdom of Swaziland." A Consultancy Report to The
Macroeconomic and Financial Management Institute of Eastern and Southern
Africa (MEFMI) 1998

"The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And
Southern Africa, Mefmi - Midterm Review" Consultancy Report to MEFMI
Liason Committee (1999).

"Opportunities and challenges of globalization: Can sub-sahara Africa avoid
marginalization?" in UNDP(1999) Back ground papers to the 1999 Human
Development Report.

"Globalization of Finance and Development Prospects in Africa." In UNDP
Cooperation South No. 1 1999

"Debt Relief and Sustainable Development in Sub Sahara Africa" Paper presented
at the Fifth Group meeting on Financial Issues of Agenda 21, Nairobi Kenya
December 1999.
 
Mwiba,
Mkuu wangu huyu Lipumba nilikuwa namheshimu sana lakini baada ya maelezo haya nimemdharau sana na kuwa elimu yake ni ya kutundikwa...
Nchi gani inatumia mitambo mitumba..Kisha anatumia nchi ambazo ni maskini kuonyesha sijui kitu gani?.. namuomba atuambie nchi hata moja iliyonunua mitambo ya kufua Umeme - Mitumba, huu ndio mfano utakao fanana na hoja ya wananchi..
Ni huyu huyu Lipumba alisema hata mitambo mipya tunaweza kuuziwa feki? can U imagine! yaani kweli mtambo wa kufua Umeme unaweza kuwa feki vipi?..sijawahi kuona gari feki hata liwe made in China sii feki ni mali inayotengenezwa na kampuni ya China..
Sifa zote ulizobandika hazina maana yoyote ikiwa hata maisha yake yeye mwenyewe yanamshinda..Lip[umba yule nimjuaye sii huyu nadhani kaishiwa baada ya kukaa nje ya Uchumi na kujiingiza ktk siasa.. Anachosha kumsikiliza..
 
Hata mimi nimejiuliza hilo swali....na saa ingine huonekana kama vile tuna ma co-presidents!!

Yule Comical Salva alishatuambia Watanzania kwamba Rais hahusiki kabisa na Dowans, hivyo hana cha kuongea.
 
Back
Top Bottom