Mkutano wa Wadau wa Demokrasia: Kikosi Kazi chawaita wenye maoni kuyawasilisha

Mkutano wa Wadau wa Demokrasia: Kikosi Kazi chawaita wenye maoni kuyawasilisha

Walio na Maoni kuhusu masuala mbalimbali yaliyoainishwa baada ya Mkutano wa Wadau wa Demokrasia uliofunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Desemba 2021 wametakiwa kuyawasilisha kwa Kikosi Kazi kilichoundwa

Masuala makuu 9 yaliyoainishwa na Kikosi hicho ili kuwasilishwa Serikalini na kufanyiwa kazi ni pamoja na Mfumo wa Maridhiano, Katiba Mpya, Mikutano ya hadhara na ndani ya Vyama vya Siasa, Masuala yanayohusu Uchaguzi, Rushwa na Maadili katika Siasa/Uchaguzi na Elimu ya Uraia

View attachment 2200466

View attachment 2200469
Kama wao wenyewe wakitoa maoni yana chakachuliwa je sie wa nje. Mukandal kada mtiufu wa Ccm ati mwenyekiti. Halafu kuna Mtungi ambae hajijui kama ni mlezi wa vyama vyote. Kabaki kuilea Ccm.
 
Msajili wa vyama vingi ndiyo katibu wa kikosi kazi / task force .

Kweli maoni yetu atayabeba kama yalivyo au ata edit au kuyatupa kapuni kuwa siyo kipaumbele cha wakubwa waliomteua kuwa ktk ofisi ya msajili wa vyama.
Hilo neno,
Wanaoleta hoja wanajua sisi ni wajinga.
Wanaokubali kutoa maoni huku wakijua maoni yalishatolewa kwa mujibu wa sheria wanaongeza ujinga
 
Hiki ni kikosi binafsi cha rais wa mpito. Hakuna namna yoyote ya kisheria wala kikatiba ya kuyafanyia kazi maoni ya hiki kikosi.

A gang of illegal group trying to hijack the will of the people. Hawa wahalifu wanaowezeshwa na Rais.

Ipo siku watalipa fedha hizi wanazovuja
 
Jibu la hayo masuala 9 ni moja tu, kuheshimu Katiba iliyopo.
 
No !NO! NOo..Maoni ya wananchi yapo kwenye time ya Warioba.Msitupotezee muda na fedha Hapa.Wajumbe wa Bunge la Katiba walitugeuka,wakachakachua maoni ya tume ya warioba,wakaja na Katiba ya Marehemu Samweli Sita.Sisi wananchi wanyonge ambao Sio wa level ya utawala,MAONI YETU TUNAMUACHIA MUNGU,MAANA NDIYE MWENYE KUAMUA KWA HAKI."AKISEMA NO ! HAKUNA WA KUSEMA YES.NA AKISEMA YES,HAKUNA WA KUSEMA NO! nyie Subirini,mtaziona nguvu zake kwa Mara nyingine.
YES YES YES. Maoni ya Warioba tunayo. Kuna wengine hawakumuona Warioba, nao je? Hapa imetajwa sayansi na teknolojia, Warioba hata Email address hajui na hakuwa nayo. Wakati maoni yanachakatwa na Bunge Maalum la Katiba, CHADEMA na CUF wakakimbia nje walipoona majority hawataki Serkali 3, kumbe walikuwa wamepanga CUF ichuje Zanzibar na CHADEMA wajitawale kwao kwa Ukabila eti Serkali ya Majimbo. Kazi iendelee. Baadaye Wazalendo wa CUF wakaona wanaburuzwa, wakamfutilia mbali Maalim Seif kwa hiyo Waarabu wakajikuta hawana Chama wakajaribu kununua CHADEMA wenye chama wakakataa Uislamu. Wakanunua ACT Wazalendo ya Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa bei nono jamaa akapata nauli kwenda kwa Tundu Lissu kuchukua mkataba wa CUF akaenda hadi World Bank kutetea mimba za utotoni. Waache Wananchi watoe mawazo.
 
Walio na Maoni kuhusu masuala mbalimbali yaliyoainishwa baada ya Mkutano wa Wadau wa Demokrasia uliofunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Desemba 2021 wametakiwa kuyawasilisha kwa Kikosi Kazi kilichoundwa

Masuala makuu 9 yaliyoainishwa na Kikosi hicho ili kuwasilishwa Serikalini na kufanyiwa kazi ni pamoja na Mfumo wa Maridhiano, Katiba Mpya, Mikutano ya hadhara na ndani ya Vyama vya Siasa, Masuala yanayohusu Uchaguzi, Rushwa na Maadili katika Siasa/Uchaguzi na Elimu ya Uraia

View attachment 2200466
View attachment 2200469
Huyu Sisty ni huyu huyu niliyekuwa namskia akiongea wakati wa Magufuli au ni mwingine. Kama ni yeye basi Maza ana utani na Watanzania....!!
 
Back
Top Bottom