Mkutano wa Waziri, Prof. Palamagamba Kabudi na Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji, Desemba 18, 2024

Mkutano wa Waziri, Prof. Palamagamba Kabudi na Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji, Desemba 18, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-12-17 at 19.57.15_f2c7066a.jpg


View: https://www.youtube.com/watch?v=-yZfMNUBE8U

Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi na Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa: Kuna Vyombo vya Habari 1,023 vilivyosajiliwa Nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema licha ya sekta ya Habari kupitia changamoto mbalimbali bado imeendelea kukua na sasa ina jumla ya Vyombo vya Habari vilivyosajiliwa Nchini ni 1,023.

Ametaja Vyombo vya Habari vilivyosajiliwa kuwa ni; Magazeti 179, Majarida 174, Vituo vya Redio 247, Vyombo vya Habari vya Mtandaoni 355, Vituo vya Televisheni ni 68, ambapo vimetoa ajira kwa Waandishi wa Habari zaidi ya 2,000 na ajira nyingine za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Amesema hayo katika Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi na Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji, leo Desemba 18, 2024.


Sungura: CoRI imesaidia mazingira wezeshi ya utendaji kwa Wanahabari
Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema CoRI imekuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha Wanahabari kufanya kazi yao kutokana na ushiriki wake katika mabadiliko ya Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na kuwa Media Service Act ya Mwaka 2016.


Sungura: CoRI tunaamini mchakato wa kupitia Sera ya Habari utaharakishwa
Akizungumza katika Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi na Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji, leo Desemba 18, 2024, Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema #CoRI inaamini mchakato wa kupitia Sera ya Habari na Utangazi ya Mwaka 2013 utaharakishwa.






 
Back
Top Bottom