Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

Sijawahi kumuamini mwanamke kulea uzazi wa mwanamke mwenzie
 
Daah pole Sana mkuu huenda mzee alifanyiwa jambo usilo lijua isingekuwa rahisi mwanaume kufanya jambo lakipuuzi Kama hilo
 


Nimeishi na mama wa kambo kabda ya kuanza shule hadi namaliza masomo yangu na kuanza kujitegemea nilipokuwa mdogo kiukweli niliona huyu mama ananitesa hata yeye mwenyewe alikuwa akihisi kwamba ananikomoa kumbe ilikuwa tofauti bali alikuwa akiniandaa kuyastahimili maisha 👉 nilikuja kugundua hilo baada ya kukua na kuwa mwana kiukweli moyoni mwangu sina kinyongo na yule mama hata MUNGU ninae muabudu kwa roho yangu ni shahidi wa hili


Waswahili husema MTOTO kwa mama hakui, hi kauli ni Kweli na hakika kwamba mtoto kwa mama yake hawezi kukua na kua mwana kwasababu moja tu 👉 mara zote mama wa Kweli lazima atampendelea mtoto wake sababu ya kuwa na mapenzi na yeye na hiyo hali kiukweli huzuia ukuaji na ukomavu halisi wa mtu na Ndio maana waswahili wakaja na hiyo kauli ya kwamba mtoto kwa mama hakui


Mama yoyote yule hawezi kumpendelea mtoto ambae sio wake never i.e mama kuwa na mapenzi na mtoto ambaye sio wake ni nadra sana Ndio maana mama wa kambo anakuwa neutral (kati) kwa mtoto na hiyo ndiyo maana ya UPENDO yaani kutenda upendo


Hakika mama wa kutuzaa huzani kwamba wanatupenda kumbe wanatenda kinyume na UPENDO i.e wanatupendelea na kupelekea kutudumaza katika ukuaji halisia yaani tunakuwa kimwili tu lakini kiakili tunadumaa na Ndio maana hata wanandoa kuishi katika ndoa inakuwa ni mtihani mkubwa mno kwani kupendelea hukuza kiburi ndani ya mtu


Check watoto wengi waliolelewa na mama zao wamefail maisha i.e maisha yapo mbali na wao ila wanaweza kuwa wamefanikiwa katika mambo ya maisha kama kupata nafasi fulani kwaajili ya kupata kipato ila maisha yapo mbali na wao hawajui Amani hawajui furaha kwasababu walipendelewa na mama zao


Lakini mtoto alielelewa na mama wa kambo mafanikio ni dhahiri kwake ya maisha na mambo ya maisha kwani mama wa kambo alikuwa neutral(kati) kwake na hiyo ndiyo nadharia ya kweli katika kutenda upendo kwa mtu

Reference

1 Yohana 4.8

"Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo"

👉Mungu ni upendo


Yakobo 2.9

"Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi"

👉Kuna tofauti kati ya kupenda na kupendelea, hi dunia kamwe haiwezi kufundisha kupenda itakufundisha kupendelea ambapo ni kutenda kinyume na upendo wenyewe na ni dhambi na Ndio wakinamama wengi wanakosea hapa na kudumaza watoto wao kiakili


MT 10:34

".........Hakika natambua ya kuwa Mungu hanau pendeleo"


Mungu hana upendeleo, anaetenda upendeleo anatenda kinyume na mapenzi ya muumba wake iwe kwa kufahamu au kutokufahamu lakini madhara ya upendeleo yapo pale pale


Mithali 31:30

"Upendeleo hudanganya....."

Kwahiyo ndugu yangu mshukuru MUNGU kwa kulelewa na mama wa kambo kwani alikupenda bila hata yeye kufahamu kwamba anakupenda kwa yale aliyokuwa anakutendea akidhani kwamba anakukomoa, hakukupendelea i.e alikuwa kati na ndio maana Leo upo hapo

That's mine view 👉Nawasilisha 🙏🙏
 
Shukurani mkuu kwa maoni yaliyobora nimekuelewa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…