Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

Asante sana mkuu, Mungu ni mwema sana, kipindi ambacho nilihitaji msaada wao hawakunisaidia leo hii mimi ndiyo wananikimbilia niwasaidie, hakuna faida yoyote waliyopata kwa mabaya yote waliyonifanyia wamebaki na aibu tu( baba na mkewe)
Kaa kitaalam mkuu hao sio wema mpaka Leo wanaweza kukuingiza kwenye vita za kiuchumi ukapauka na jua. So usipende wakujue sana, sijamaanisha usiwaaidie ila kata mazoea yao kwako
 
Kaa kitaalam mkuu hao sio wema mpaka Leo wanaweza kukuingiza kwenye vita za kiuchumi ukapauka na jua. So usipende wakujue sana, sijamaanisha usiwaaidie ila kata mazoea yao kwako
Wananipigia na simu kabisa eti unakuja lini nyumbani, nataka nikamilishe mambo yangu nisepe kabisa huu mji wasijue nipo wapi na namba nabadilisha kabisa
 
Wananipigia na simu kabisa eti unakuja lini nyumbani, nataka nikamilishe mambo yangu nisepe kabisa huu mji wasijue nipo wapi na namba nabadilisha kabisa
Usiwakimbie, adui matatizo huwa hayakimbiwi yanakabiliwa, ww vaa miwani ya mbao. Tafuta marafiki wapya na wema bado wapo hao ndio uwaweke karibu. Nikimaanisha Mugu akupe Mume Bora wa kuendana nae huyo ndio atakuwa rafiki Yako WA kudumu ktk maisha yako
 
Mmh labda huenda wapo
wapo mkuu, kuna jirani yangu hapa, pua na mdomo anampenda mtoto wa kambo kuliko hata anavowapenda wa kuwazaa, tena yeye ndo alimlazimisha mumewe akamchukue mtoto kwa bibi yake maana mama yake aliolewa akamuacha kwa bibi, , watoto wake huwa wanamuuliza "mama mbona unampenda sana fulani?" huwa anawajbu kifupi tu.."nampenda kwa sababu ni mtoto wangu" huyo dogo ameoa na ana familia ila kila weekend lazima aje kwa huyo mama au mama aende kwake, kwenye harusi ya dogo yy ndo alikuwa na hamsha hamsha kuliko hata mama mzazi.
 
Pole sana mkuu hauko peke Yako tumeyapitia wengi, mim nilikuwa nanyimwa maji ya kunawa uso Ile asubuhi kwenda shule kisa maji sikuyachota, Kuna siku shule walituma vipande vya Kuni asubuhi yake nikadokoa kimoja kisiri huwezi amini alinifata mpaka shule na kanga Moja kunipokonya ukuni, nilishawahi twanga ntwiri(karanga) kwenye kinu bahati mbaya sikujua kwamba kinu ni kichafu kwahiyo ntwiri zikabadilika rangi kwa uchafu na mchanga nililishwa zote kwa lazima, mtaani na mashoga zake stories ni mm nakula sana, mm mjeuri na Kila aina ya ubaya natwishwa mm. Shuleni niliwahi kuacha kwa mwaka mmoja baba akanirudisha nikiwa drs la 3 Hilo naweza mshukuru Mzee... Shuleni nilikuwa nafanya vzuri sikuwahi kushika namba 3 mpaka namaliza std 7 ilikuwa no1 &2 hicho kitu kilikuwa kinamkera sana huyo mama

Kumbuka sabuni Za kufulia na nguo za kuvaa nilikuwa najipambania baada ya kuwa mkubwa mkubwa, nikifanya vbarua siku za wikendi na kuvua zile kambale ndogo ngodo tunawauzia matajiri wanaosafirisha kwenda visiwani kuvulia sangara... Hapo nikiuza nikapata chenji namkabidhi huyo mama hapo atakenua jino kwa muda huo zikiisha mwendo ni ule ule

Nilifaulu kwenda sec nikapata mfadhili wa kunisomesha mpaka chuo lkn baba akashauliana na mke wake wakanichomoa huko kwa mfadhili kisa eti shule niliyofaulia wanamsumbua wananihitaji nikasonee huko.. mfadhili akakubali mchukueni tu kumbuka nilikuwa form 1 na nilikuwa tayari Nina miezi miwili shuleni.

Nimefika home nafanya maandalizi ya kwenda shule husika kumbuka Mzee Hana hata mia mbovu alinitelekeza hapo shuleni bila msaada wowote nalala kwenye mageto ya washkaji. Nikaamua kuacha shule sikusoma hata kwa mwezi mmoja

Ikabidi nijikite tu nyumbani nifanye maandalizi ya kilimo ikibidi baada nioe kumbuka tayari nilikuwa na miaka 12.

Siku Moja akaja ndugu yetu kutoka mjini mkoa flani ni Mzee wa makamo akaja kututembelea akaniulizia maana kila kipindi akijaga huwa ananiulizia Kuna kipindi alikuja kuniulizia anichukue nilikuwa la Tano Mzee akakataa kwamba bado nasoma hata alovyomwambia nitasomea huko kwake akakataa.. ss tyme hii akaja kuniulizia kwa mara nyingine ambapo ndio amenikuta kwenye muda mwafaka sipo shule nimeacha akaniomba kwa baba lkn baba na mke wake wakaweka ngumu nisichukuliwe

Kwa vile tayari nilikuwa najitambua na mm nilomgomea Mzee kwa hoja ndipo akaniruhusu hapo ndio ikwa mwanzo na mwisho wa kutengana na mama wa kambo nikamuacha mdogo wangu ( kumbuka kwa mama wa kambo tulikuwepo wawili mm na mdogo wangu.

Nimefika mjini sitaki kuliongelea sana hili la mjini ila baada ya miaka miwili kukaa hapo kwa huyu Mzee niliamua kuondoka hapo nikaenda kupanga chumba na mfukoni nilikuwa na elfu 28 tu baada ya kunikata madeni yake aliyoona ananidai (nilikutana na changamoto ya mke wake nikasepa)

Hapo ndio nikayaanza majukum ya kiutu uzima huku na miaka 15

Nachoshukuru mungu alikuwa upande wangu nilipambana kwa maumivu mpaka nikauona mwangaza nikapewa taarifa dogo amefaulu mtihani wa la 7 nikaona sio mbaya nimsapot dogo maana mm shule ilinishinda... Nikatuma pesa za maandalizi dogo kuingia 4m1 dogo akaanzq shule.

kumbuka huyo mama alikuwa ananipigia sim kunisihi nisitishe kumhudumia bw mdogo kwamba najisumbua bure dogo hasomi anashinda kwenye kamari na mabanda ya video... Lkn kwa vile nilikuwa namuelewq roho yake na madhumuni yake nikawa nampuuzia mpaka dogo akamaliza 4.

Dogo akafanikiwa kuchaguliwa kujiunga special diploma udom, nikapambana akapata mkopo %100 nikampeleka akaanza masomo

Bahati mbaya magufuli akawafukuza chuo nadhani mnakumbuka lile shakata miaka Ile, dogo nikampokea geto kujipanga kusubili kinachojili bahati nzuri serikali ikawagawanya kwenye vyuo vidogo, yeye akapangiwa Kuna chuo kipo tukiyu mbeya. Dogo amesoma hapo mpaka akamaliza bila Mzee na mke wake kutoa hata mia zaidi ya kutoa majungu tu.

2019 zile ajira za Magufuli dogo aliomba mara moja tu imooo mbaka ss ni mwalimu wa sec hapo shinyanga na anabiashara zake nzuri zinazomuingizia kipato., ana mke na watoto wawili

Mim Nina familia yangu Nina maisha yangu na nipo kwangu ila ukweli Mzee wangu na mke wake siwakibali mpaka kesho japo akinipigia sim nasapot kimtindo.

Ushauri kwa wanaume wenzangu;
Kuachana na mke ambaye tayari mlishatengeneza familia nikimaanisha tayari mmeshavileta duniani viumbe vyenu visivyo na hatia ni jambo baya sana, mwanaume fanyeni namna msivunje ndoa, na hata ikishindikana kunusuru hiyo ndoa basi mwanaume mwachie watoto mwanamke ni hayo tu.
Cha ajabu ni ukichunguza maisha ya mtoto aliye lelewa na mama wa kambo nayule wa baba na mama og

Utagundua yule wa kulelewa na mama wa kambo Yuko vizuli kimaisha

Hapo ndipo ubaya wa mama wa kambo hunadilika kuwa wema alio utenda hata bila yeye mwenyewe kujua
 
Mkuu kwa mazingira tuliyonayo wanaume kula mpaka itoke Kila siku ni ngumu sana kuwafuatilia mienendo ya vijana wake, kumbuka ni ngum sana kijana mdogo kuelwzea situation inayompitia yani mtoto anateketea nalo rohoni hasemi sijui kwann watoto tunakuwa hivyo.
Baba Utakuja kugundua tayari either umeshachelewa na kijana ameathirika vya kutosha
Mzazi unatakiwa uwe na ukaribu na wanao.
Mzee wako angekuwa na ukaribu na wewe kama marafiki lazima angejua kinachoendelea.
Tatizo wazazi wengi wa zamani na siku hizi wqchache hawana hiyo.
Mtoto anakuwa na mawazo ila mzazi hagundui.
I
 
Mzazi unatakiwa uwe na ukaribu na wanao.
Mzee wako angekuwa na ukaribu na wewe kama marafiki lazima angejua kinachoendelea.
Tatizo wazazi wengi wa zamani na siku hizi wqchache hawana hiyo.
Mtoto anakuwa na mawazo ila mzazi hagundui.
I
Mzee yupo karibu na mke wake mpaka kesho humwambii kitu, nakumbuka kipindi hicho shule ya msingi ikifika wikendi nilikuwa nawaza sana sabuni ya kufuria napata wapi. Ukitaka Mzee awakie kwenye gear muingizie shida zako
 
Cha ajabu ni ukichunguza maisha ya mtoto aliye lelewa na mama wa kambo nayule wa baba na mama og

Utagundua yule wa kulelewa na mama wa kambo Yuko vizuli kimaisha

Hapo ndipo ubaya wa mama wa kambo hunadilika kuwa wema alio utenda hata bila yeye mwenyewe kujua
Sahihi mkuu, mama etu aliachana na baba akatuacha kwa baba, sababu ya kuachana japo nilikuwa na umri wa miaka 5 hivi ila nakumbuka. Mzee alisafiri kwenda kigoma huko kwenye utafutaji alikaa kama mwaka hivi alivyorudi akaja na mwanamke mwingine yani mzazi mwenzia walieachana miaka mingi nyuma. Eti lengo la Kuja nae eti mwanamke alivyokutana nae huko akamganda eti huniachi Leo nataka nikawaone wanangu nimewakumbuka... Kumbuka Mzee aliachwa na huyo mama Tena kwa kumtelekezea watoto wawili wakiwa bado wadogo
sana wa kiume na kike mpaka wote wanamiji yao eti ndio mwanamke anakumbuka kumrejea.

Mzee akatinga nae halafu Cha kushangaza akatinga nae geto kwetu yani kajimba kenyewe ka tope vyumba vitatu yani chumba/sebule/chumba nadhani hapo umeelewa.

Hapo ndio mama akaamsha siku hiyo hiyo usiku tunamuona anachukua kuku wake anaondoka maana alikuwa na kuku wengi amefuga. Sijui ugomvi wao ilikuwa nn mpaka baba anamletea mama mwanamke mwingine Tena ndani kwake... Mzee jau sana yule
 
1.Nilijitahid kusoma primary nikashika nafas ya pili... ile bimkubwa kachek akasema nimeangalizia..., daah.
Mim nilikuwa nawabomoa haswa niliwahi kushika namba Moja kata nzima mtihani wa la 4, mpaka yule mwenyekiti wa CWT kuamua kunichukua alikuwa tayari uwezo na juhudi zangu ameviona
 
Ukifanya vizuri hupat pongez.. Ukipata msala sasa.. mtaa mzima, ndugu na jamaa wote wanapelekewa taarifa.... So sad
 
Ukifanya vizuri hupat pongez.. Ukipata msala sasa.. mtaa mzima, ndugu na jamaa wote wanapelekewa taarifa.... So sad
Ni Maza mzazi ama ndio Hawa waliotulea ss?
 
Back
Top Bottom