Pole sana mkuu hauko peke Yako tumeyapitia wengi, mim nilikuwa nanyimwa maji ya kunawa uso Ile asubuhi kwenda shule kisa maji sikuyachota, Kuna siku shule walituma vipande vya Kuni asubuhi yake nikadokoa kimoja kisiri huwezi amini alinifata mpaka shule na kanga Moja kunipokonya ukuni, nilishawahi twanga ntwiri(karanga) kwenye kinu bahati mbaya sikujua kwamba kinu ni kichafu kwahiyo ntwiri zikabadilika rangi kwa uchafu na mchanga nililishwa zote kwa lazima, mtaani na mashoga zake stories ni mm nakula sana, mm mjeuri na Kila aina ya ubaya natwishwa mm. Shuleni niliwahi kuacha kwa mwaka mmoja baba akanirudisha nikiwa drs la 3 Hilo naweza mshukuru Mzee... Shuleni nilikuwa nafanya vzuri sikuwahi kushika namba 3 mpaka namaliza std 7 ilikuwa no1 &2 hicho kitu kilikuwa kinamkera sana huyo mama
Kumbuka sabuni Za kufulia na nguo za kuvaa nilikuwa najipambania baada ya kuwa mkubwa mkubwa, nikifanya vbarua siku za wikendi na kuvua zile kambale ndogo ngodo tunawauzia matajiri wanaosafirisha kwenda visiwani kuvulia sangara... Hapo nikiuza nikapata chenji namkabidhi huyo mama hapo atakenua jino kwa muda huo zikiisha mwendo ni ule ule
Nilifaulu kwenda sec nikapata mfadhili wa kunisomesha mpaka chuo lkn baba akashauliana na mke wake wakanichomoa huko kwa mfadhili kisa eti shule niliyofaulia wanamsumbua wananihitaji nikasonee huko.. mfadhili akakubali mchukueni tu kumbuka nilikuwa form 1 na nilikuwa tayari Nina miezi miwili shuleni.
Nimefika home nafanya maandalizi ya kwenda shule husika kumbuka Mzee Hana hata mia mbovu alinitelekeza hapo shuleni bila msaada wowote nalala kwenye mageto ya washkaji. Nikaamua kuacha shule sikusoma hata kwa mwezi mmoja
Ikabidi nijikite tu nyumbani nifanye maandalizi ya kilimo ikibidi baada nioe kumbuka tayari nilikuwa na miaka 12.
Siku Moja akaja ndugu yetu kutoka mjini mkoa flani ni Mzee wa makamo akaja kututembelea akaniulizia maana kila kipindi akijaga huwa ananiulizia Kuna kipindi alikuja kuniulizia anichukue nilikuwa la Tano Mzee akakataa kwamba bado nasoma hata alovyomwambia nitasomea huko kwake akakataa.. ss tyme hii akaja kuniulizia kwa mara nyingine ambapo ndio amenikuta kwenye muda mwafaka sipo shule nimeacha akaniomba kwa baba lkn baba na mke wake wakaweka ngumu nisichukuliwe
Kwa vile tayari nilikuwa najitambua na mm nilomgomea Mzee kwa hoja ndipo akaniruhusu hapo ndio ikwa mwanzo na mwisho wa kutengana na mama wa kambo nikamuacha mdogo wangu ( kumbuka kwa mama wa kambo tulikuwepo wawili mm na mdogo wangu.
Nimefika mjini sitaki kuliongelea sana hili la mjini ila baada ya miaka miwili kukaa hapo kwa huyu Mzee niliamua kuondoka hapo nikaenda kupanga chumba na mfukoni nilikuwa na elfu 28 tu baada ya kunikata madeni yake aliyoona ananidai (nilikutana na changamoto ya mke wake nikasepa)
Hapo ndio nikayaanza majukum ya kiutu uzima huku na miaka 15
Nachoshukuru mungu alikuwa upande wangu nilipambana kwa maumivu mpaka nikauona mwangaza nikapewa taarifa dogo amefaulu mtihani wa la 7 nikaona sio mbaya nimsapot dogo maana mm shule ilinishinda... Nikatuma pesa za maandalizi dogo kuingia 4m1 dogo akaanzq shule.
kumbuka huyo mama alikuwa ananipigia sim kunisihi nisitishe kumhudumia bw mdogo kwamba najisumbua bure dogo hasomi anashinda kwenye kamari na mabanda ya video... Lkn kwa vile nilikuwa namuelewq roho yake na madhumuni yake nikawa nampuuzia mpaka dogo akamaliza 4.
Dogo akafanikiwa kuchaguliwa kujiunga special diploma udom, nikapambana akapata mkopo %100 nikampeleka akaanza masomo
Bahati mbaya magufuli akawafukuza chuo nadhani mnakumbuka lile shakata miaka Ile, dogo nikampokea geto kujipanga kusubili kinachojili bahati nzuri serikali ikawagawanya kwenye vyuo vidogo, yeye akapangiwa Kuna chuo kipo tukiyu mbeya. Dogo amesoma hapo mpaka akamaliza bila Mzee na mke wake kutoa hata mia zaidi ya kutoa majungu tu.
2019 zile ajira za Magufuli dogo aliomba mara moja tu imooo mbaka ss ni mwalimu wa sec hapo shinyanga na anabiashara zake nzuri zinazomuingizia kipato., ana mke na watoto wawili
Mim Nina familia yangu Nina maisha yangu na nipo kwangu ila ukweli Mzee wangu na mke wake siwakibali mpaka kesho japo akinipigia sim nasapot kimtindo.
Ushauri kwa wanaume wenzangu;
Kuachana na mke ambaye tayari mlishatengeneza familia nikimaanisha tayari mmeshavileta duniani viumbe vyenu visivyo na hatia ni jambo baya sana, mwanaume fanyeni namna msivunje ndoa, na hata ikishindikana kunusuru hiyo ndoa basi mwanaume mwachie watoto mwanamke ni hayo tu.