Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

SAMEHE NA ACHANA NAO SIO KUFANYA UKARIBU AU URAFIKI, WABAKIA WATU WA KAWAIDA (SIO ADUI WALA RAFIKI PIA SIO NDUGU)
Kusamehe nilishasamehe sababu Sina vinyongo kwamba nilipize kisasi ila tu siwezi kusahau niliyoyapita na aliyoniganya sababu bado nayaishi napambana nayo
 
We jamaa pesa zetu..
Mama wa kambo watutese na wewe pia ututese daah we want our money mkuu
Huyu mjinga miaka ya nyuma kanitesa sana akanipausha balaa kidogo anirudishe Tena kijijini mpaka pale niliposhituka kwamba si mtu mzuri sana huyo... Anahela zangu nyingi sana niliamua nimsamehe tu
 
Ushauri wangu mimi ni huu,ukiachana na mke wako na ukaamua kuoa mke mwingine hakikisha kuwa unakuwa karibu sana na watoto wako,usije ukafanya kosa la kumuamini huyo mwanake kwa jambo lolote linalohusu watoto wako,atakudanganya kuwa anawapenda na kuwatunza lakini nyuma ya pazia anaweza kuwatesa sana kwakuwa anajua tayari kashakuteka ufahamu.WAnawake karibu wote aikudanganya mtu hawawezi kuwapenda watoto amabo sio wakwake,hata unapokuta mwanamke ameweza kuadopt mtoto basi ujue kuwa huyu ana roho ya kipekee sana...
Mkuu kwa mazingira tuliyonayo wanaume kula mpaka itoke Kila siku ni ngumu sana kuwafuatilia mienendo ya vijana wake, kumbuka ni ngum sana kijana mdogo kuelwzea situation inayompitia yani mtoto anateketea nalo rohoni hasemi sijui kwann watoto tunakuwa hivyo.
Baba Utakuja kugundua tayari either umeshachelewa na kijana ameathirika vya kutosha
 
Ndio maana sita oa mpka binti na kijana wangu waweze kujitegemea na kujisimamia kwa sasa wananihitaji 100% kwanza.
Me nadhani ikiwa upo hai na pengine mmeachana na mwenza either ubaki na watoto usioe au waendelee na mama yao!!

Ila Bora nibaki na wanangu kulelewa watoto napo na mtu mwingine jau sisi wanaume tunajijua vzr,

kama mpango wa kando tutakutana huko huko wanangu waishi kwa amani
 
Poleni sana wote mliopitia na wanaopitia misukosuko ya mama wa kambo. Kitambo kuna jamaa aliimba "mama wa kambo, huyo si mama, oo mateso...."
 
Mkuu pole sana, mimi ni moja ya binadamu wa kiume ambaye nahitaji muujiza kutoka mbinguni wa kuamin kwamba wanawake ni viumbe wenye huruma,kama wengi hujaribu kuwapamba.
Siwez kumwonea mwanamke lakin sina huruma naye kama nionavyo kwa wengine.
Yamkin wanawake sio wabaya kihivyo lakin lakin nadhan wao ndo character bora wa kucheza nafas ya shetani hata wao bila kujua.
 
Poleni sana wote mliopitia na wanaopitia misukosuko ya mama wa kambo. Kitambo kuna jamaa aliimba "mama wa kambo, huyo si mama, oo mateso...."
Kabisa mkuu, dah nilipata mfadhili wa kujitolea kunisomesha akanichukua akanifanyia shopping akanipeleka shule na naishi nyumbani kwake.. alikuwa mwenyekiti wa CWT wilaya flani. Aisee sijui baba na huyo mke wake walishaulianaje nadhani huyo mama aliona tauri naenda kitoboa akamshauri Mzee akanifata mjini Kuja kunichomoa ni kweli nikafungasha vilago na ndio ikawa mwisho wa elim😃
 
Mkuu pole sana, mimi ni moja ya binadamu wa kiume ambaye nahitaji muujiza kutoka mbinguni wa kuamin kwamba wanawake ni viumbe wenye huruma,kama wengi hujaribu kuwapamba.
Siwez kumwonea mwanamke lakin sina huruma naye kama nionavyo kwa wengine.
Yamkin wanawake sio wabaya kihivyo lakin lakin nadhan wao ndo character bora wa kucheza nafas ya shetani hata wao bila kujua.
Asante sana mkuu, nikweli kabisa usemalo
 
Mimi niliwahi kutemewa mate kichwani na mama wa kambo sijui alikuwa anamaanisha ...nimechelewa hata kuyafikia malengo yangu ya kimaisha kwa sababu ya wa kambo..aliwahi kunichoma pasi usoni mpaka ninalo kovu.....mama wa kambo si mama...kiuhalisia Tu mama wa kambo humchukulia mtoto wa mwenzie kama mkubwa mwenzie
 
mawasiliano yapo kimtindo namaanisha akinipgia napokea ila siwezi kupiga. Wameshasema sana niipeleke familia yangu waione lkn upande wangu naona haina maana kbs
Mkuu sijui una imani gan juu ya Mungu ila ukiipelek familia hakikisha umefunga na kuomba. Mzee wako hatakuwa shida ila kwa huyo maza yako wa kando hataiacha salama familia yako.
Na hata utakapo amua kwenda usitoe taarifa na uskae muda mrefu.
 
Mkuu sijui una un imani juu ya Mungu ila ukiipelek familia hakikisha umefunga na kuomba. Mzee wako hatakuwa shida ila kwa huyo maza yako wa kando hataiacha salama familia yako.
Na hata utakapo amua kwenda usitoe taarifa na uskae muda mrefu.
Mzee najua Hana shida ila tatzo lipo kwa huyo mama, ni miaka mingi sana naliwazia Hilo jambo tangu Nina kijana mmoja mpaka ss wamefika wa 4 na sijawahi wapeleka hata mke wangu hapajui wala hawajui
 
Back
Top Bottom