Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

Mimi niliwahi kutemewa mate kichwani na mama wa kambo sijui alikuwa anamaanisha ...nimechelewa hata kuyafikia malengo yangu ya kimaisha kwa sababu ya wa kambo..aliwahi kunichoma pasi usoni mpaka ninalo kovu.....mama wa kambo si mama...kiuhalisia Tu mama wa kambo humchukulia mtoto wa mwenzie kama mkubwa mwenzie
Mimi kanipa kilema Cha maisha huu ni mwaka wa 18 napambana kuilejesha Hali yangu ya awali
 
Mzee najua Hana shida ila tatzo lipo kwa huyo mama, ni miaka mingi sana naliwazia Hilo jambo tangu Nina kijana mmoja mpaka ss wamefika wa 4 na sijawahi wapeleka hata mke wangu hapajui wala hawajui
Mkuu binafsi sioni haja ya kuwapeleka. Kama kuna ulazima sana wa kwenda, nenda peke yako na uondoke huko fasta
 
Poleni sana.... Kunakuwa na sababu ya kumfanya awe hivyo alivyo


NB:Sio wote ni wakatili. Niliwahi kulelewa mwanangu na mwanamke mwingine na dogo alikuwa akinipa feedback nzuri kutoka kwa malezi ya mama yake mlezi na sikuona changamoto yoyote iliyojitokeza kwa kipindi walichokuwa wote.
 
Pole sana. Ushauri wako kwenye aya ya mwisho ni wa busara n unafaa kuzingatiwa sana na mwanaume yeyote anayetarajia kuoa na ambaye ameshaoa.
Kweli kabsaa, binafsi hilo nimesha lizangatia na kwakuwa najua kuachana kunaweza tokea at any point, saivi nakula mazoez ya kuishi single.
Kwamba tukiachana na wife staoa ntakaa kimagumashi au nioe mwanamke asiye zaa.
 
Nikweli hajui, mama wa kambo ni mashetani, imagine unakutana na mama wa kambo mshirikina, Bora ww mkuu alikuwa anakupa kipigo ila hakufanyii mazingara yoyote
Mi kwa mazingira hapana.
Picha linaanza mi faza ni wale mafaza wa kitabu an alishanisomea mno yaani acha tuu hayo mambo yapo.mbali na mimi mita mia saba
 
Poleni sana.... Kunakuwa na sababu ya kumfanya awe hivyo alivyo


NB:Sio wote ni wakatili. Niliwahi kulelewa mwanangu na mwanamke mwingine na dogo alikuwa akinipa feedback nzuri kutoka kwa malezi ya mama yake mlezi na sikuona changamoto yoyote iliyojitokeza kwa kipindi walichokuwa wote.
Mkuu mwenyew nimelelewa ktk mazingira kama huyo chalii yako ila we jua tuu kwamba wanawake wanaweza kucheza part ya nyoka kwenye familia.
 
Mzee najua Hana shida ila tatzo lipo kwa huyo mama, ni miaka mingi sana naliwazia Hilo jambo tangu Nina kijana mmoja mpaka ss wamefika wa 4 na sijawahi wapeleka hata mke wangu hapajui wala hawajui
Kama vipi mwambie mzee aje akutembelee ndo awaone wajukuu.
 
Huyu mjinga miaka ya nyuma kanitesa sana akanipausha balaa kidogo anirudishe Tena kijijini mpaka pale niliposhituka kwamba si mtu mzuri sana huyo... Anahela zangu nyingi sana niliamua nimsamehe tu
Huyu jamaa tamfungulia uzi sio mda ili.kule.jykwaa lao la mikeka walifungie
 
Mkuu mwenyew nimelelewa ktk mazingira kama huyo chalii yako ila we jua tuu kwamba wanawake wanaweza kucheza part ya nyoka kwenye familia.
Ni kweli shahidi za uovu wa mzazi wa kufikia(ke) ni nyingi sana
 
mkuu wewe unasema kulala nje, watu tumelala sana juu ya miti ya miembe na kukakucha
Ni kweli hivi vitu vinakwenda kwa kutifautiana ila siku moja nikiwa mazingira fulani mvua kubwa ikinyesha nyakati za usiku mnene nilikumbuka kwamba kumbe mama aliniandaa vyema sana kumudu ile kitu nikaamini alikuwa hanitesi alikuwa ananiandaa.

Kwahiyo hadi leo naamini kila gumu lina sababu zake likitumiwa kwa hali chanya zaidi.
 
Kabisa mkuu, dah nilipata mfadhili wa kujitolea kunisomesha akanichukua akanifanyia shopping akanipeleka shule na naishi nyumbani kwake.. alikuwa mwenyekiti wa CWT wilaya flani. Aisee sijui baba na huyo mke wake walishaulianaje nadhani huyo mama aliona tauri naenda kitoboa akamshauri Mzee akanifata mjini Kuja kunichomoa ni kweli nikafungasha vilago na ndio ikawa mwisho wa elim😃
Sasa mkuu hapi wew unaona kunatofauti gani na yale mapepo yanayokemewa church??? Yaan aseee.
 
Mkuu kwa mazingira tuliyonayo wanaume kula mpaka itoke Kila siku ni ngumu sana kuwafuatilia mienendo ya vijana wake, kumbuka ni ngum sana kijana mdogo kuelwzea situation inayompitia yani mtoto anateketea nalo rohoni hasemi sijui kwann watoto tunakuwa hivyo.
Baba Utakuja kugundua tayari either umeshachelewa na kijana ameathirika vya kutosha
Mtoto anadeliver kile alicholishwa, ni wachache wenye uthubutu wa kupambana.
Na wengi hukata tamaa zaidi akiona baba anamsikiliza zaidi mama kuliko yeye.
 
Mkuu binafsi sioni haja ya kuwapeleka. Kama kuna ulazima sana wa kwenda, nenda peke yako na uondoke huko fasta
Sahihi mkuu huyu mama ni kigagula wale wa nyaheru wa kigoma kama unawajua, nimeishi nae kwa kipindi chote likini sikuwahi kuona tunguri lolote zaidi ya vidawa vya mitishamba vya kawaida na Mzee wala hayo mambo Hana hata chale Hana na anayapinga hayo mambo

Lakini Cha kushangaza huyo mama na kijana wake wa kiume Ambae kwa sas ni marehem, amefariki hawelewani akimtuhum mama yake kumuulia mwanae. Nilikuwa sielewi hii show nikidhani lbd huenda kijana wake wanamabifu tu mengine tusiyoyajua

Kuna kipindi kijijini vifo vya kishirikina na uchawi vilikithiri, viongozi wa Kijiji wakaitisha mkutano kupiga kura ya kuwabaini wachawi wa kijijini hapo ili wafurushwe ebana ee na huyo mama inasemekana alizipata kura zake nyingi ila akapewa onyo Kali Kuna wengine walibomolewa makazi yao wakahama Kijiji... Hapo tayari nilikuwa nipo mjini najipambania

Siku Moja nikasema ngoja nikawasabahi maana ni miaka mingi nilikuwa sijaenda. Nilifunga safari kimya kimya wakaniona nimefika nikamkuta dogo ndio yupo likizo, Cha kushangaza usiku tumelala fresh tunapiga stories na dogo asubuhi naamka nipo uchi wa mnyama nguo nilizokuwa nimevaa usiku ule nikazikuta uvunguni. Nilimuuliza dogo hiyo Hali ni kweli nililala bila nguo? Dogo akakataa na kweli huwezi lala bila nguo halafu umelala na mwanaume mwenzako halafu mazingira yenyewe machafu ambapo hata geto kwangu sikuwahi kulala bila boxa iweje hapa iwe hivyo? Na nikikumbuka nikweli nililala kama nilovyokuja lkn mshangao nimeamka mtupu!

Nilitukana sana nilimnyea sana huyo Maza nikaamini kabisa huyo Maza ni kigagula na tangu siku hiyo nimekuja Pata familia naogopa sana kwenda kujtambulisha familia yangu na sijawahi Rudi Tena mpaka leo
 
Mi kwa mazingira hapana.
Picha linaanza mi faza ni wale mafaza wa kitabu an alishanisomea mno yaani acha tuu hayo mambo yapo.mbali na mimi mita mia saba
Pole sana mhanga mwenzangu🤣 Mimi alinipga kombora nimeishi nalo napambana nalo nakumbuka mwaka 2013 nilimpgia Mshana Jr nalia nikiomba msaada namna ya kunisaidia alinitia moyo sana na kunipa ushauri kadhaa najua hawezi akakumbuka ila mm nakumbuka vyote
 
Back
Top Bottom