Mkuu Rrondo kwa hili la matamshi naomba niwe upande wa watangazaji

Hakuna aliyekataa kama si la walimwengu wote na kwamba si jambo la kawaida,tunachopinga ni watu kutokukubali kurudi kwenye asili ya watu wenye lugha yao kuwa kama mzani wa kujua usahihi wa matamshi,kinyume na hapo ni uharibifu kama tunavyouona hii leo.

Unajua sisi tuna mifano ya watu ambao wanayatamka vyema majina ya watu wengine kama vile wayatamkavyo wenyewe.
Ndo haiwezekani sasa dunia nzima wawe na mtazamo kama wako
 
Ilikuwa lazima uanzishe uzi? Huu ufafanuzi wako si ungeweka kwenye huo uzi?
Nadhani ungeichambua hoja yako mwenyewe mara mbilimbili kuna faida gani ya mimi kuanzisha uzi na pia kuna hasara gani
 
Tuna angalia usahihi na haya ninayo yasema ndio yametufikisha hapa.
Usahihi upo kwa mhusika binafsi tu, na ndio maana tuna tamaduni tofauti ikimaanisha kwamba chochote ambacho hujiri huchujwa na tamaduni husika haijalishi kimetokea wapi ila kinapopokewa na tamaduni ya eneo fulani huendana na hali ya eneo hilo
 
Mimi nilisoma Kiswahili hadi Olevel tu, ila nakubaliana na mtoa mada, tatizo letu TZ waingereza wametuathiri sana kuna watu wanataka kutamka maneno kama Kiinglish kitu ambacho si sahihi.
 
Usahihi upo kwa mhusika binafsi tu, na ndio maana tuna tamaduni tofauti ikimaanisha kwamba chochote ambacho hujiri huchujwa na tamaduni husika haijalishi kimetokea wapi ila kinapopokewa na tamaduni ya eneo fulani huendana na hali ya eneo hilo

Hili linaenda kinyume na misingi ya kielimu na huwezi kupata maarifa kwa mtindo huu.
 
Elimu haimaanishi kubadilisha tamaduni bali kuongeza maarifa
 
Elimu inabadilisha sana tamaduni,kama una amini katika dini hili ni maarufu na zimeondolewa tamaduni nyingi za kininga na kuwekwa kilicho bora zaidi.

Asili ndio chanzo,kama mfatiliaji wa mambo ya kielimu hili utaliona na utakikubali.
 
Elimu huja kututoa katika hali duni kiutendaji na kutupeleka katika hali ya juu zaidi kiutendaji.

Mathalani kwa sisi tunaoamini dini ni kwamba elimu ya dini ilitutoa katika kuabudu (Mizimu,miti,masanamu na mfano wake) visivyodhuru wala visivyonufaisha na kutupeleka katika kumuabudu yule anae stahiki kuabudiwa.
 
Naona unajadili vitu vingine tofauti sasa

Haya bwana umeshinda, si lazima tufananane fikra
Elimu inabadilisha sana tamaduni,kama una amini katika dini hili ni maarufu na zimeondolewa tamaduni nyingi za kininga na kuwekwa kilicho bora zaidi.

Asili ndio chanzo,kama mfatiliaji wa mambo ya kielimu hili utaliona na utakikubali.
 
kuna ukweli kiasi chake...ila kama ndio hivi basi wafanye hivyo kote sio sehemu zingine wanajifanya kunena kama wenye lugha yao tuwaone wajuzi wakati kuna sehemu nyingine ndo hivyo orijojo
 
Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom