Mkuu wa Chuo Ang'olewa Ukuu

Mkuu wa Chuo Ang'olewa Ukuu

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
280
Serikali imemvua ukuu wa chuo Mkuu wa chuo cha ualimu Korogwe Bw. Mwiga pamoja na makamo wake. Hii ni kutokana na ubadhilifu wa mali ya umma. Mkuu huyo amekuwa akilalamikiwa na watumishi wa chuo hicho kwa muda mrefu. Pengine hilo linaweza kuwa fundisho kwa wakuu wengine wa taasisi za umma wenye tabia kama hiyo.
 
Malipo ya dhambi ni mauti
 
Hapo tu ndo huwa naikubali serikali yetu, ku deal na vidagaa na kuachia papa wakichanja mbuga
 
Afisa gani siyo mwizi tanzania?ajitokeze

Ambaye hajawahi kuzini na awe wa kwanza kumpiga jiwe, wote waliondoka kimya kimya, alipoinua kichwa alijikuta yupo yeye na mama yule, akamwambia: "Nenda zako usitende dhambi tena"- JESUS CHRIST
 
Kuna mwanangu anasoma pale mwaka wa pili, walitakiwa waende BTP tokea january ila hadi sasa hawajaenda, inasemekana huyo mkuu wa chuo amefuja fedha ambazo walitakiwa wazitumie kwa ajili ya hilo zoezi, yeye kapangiwa maeneo hayo hayo ya korogwe nauli alitakiwa apewe sh 17,000/ kwenda na kurudi akaambulia sh 2000/. Mwanafunzi aliyetakiwa apewe karibu laki tatu anapewa elfu themanini, wamegoma sijajua mufaka wake!
 
Back
Top Bottom