Uchumikati
Member
- Dec 8, 2020
- 82
- 97
Pamekuwepo kilio cha mda mrefu sana ambacho hakijawahi tafutiwa ufumbuzi juu ya waalimu wa part-time kunyanyaswa kwenye malipo na si mara moja au mbili malamalamiko yalisharipotiwa.
Tunasema ni manyanyaso kwa sababu kila semester yanajirudia. Licha ya kujaza claim kila mwezi lakini bado malipo hayafanyiki,yaani mtu anajaza claim analipwa baada ya miezi 6 au 7 bila sababu yoyote.
Hapa ninaandika leo ni mwezi wa 9 lakini kuna waalimu hawajalipwa tangu mwezi wa 3. Hii ni sawa? Kila siku wanaambiwa malipo yanashughulikiwa, hivi kweli nini kinashughulikiwa tangu mwezi wa 3?
Wakati huohuo external examiners wakija wanalipwa ndani ya wiki moja. Hivi mnadhani hii hali waalimu wanaifurahia? Wafanyakazi wengine wote claims zao zinalipwa bila shida yoyote ndani ya muda mfupi.
Kwanini ubabaishaji hauishi licha ya malalamiko ya kila siku? Hamuitambui kazi inayofanyika kwa wanafunzi? Au mnataka waalimu wakale kwa wanafunzi?
Tunaamini wewe mkuu wa chuo ni mtu msikivu licha ya kutokua msikivu mara zote huko nyuma,bado tunaamini utarekebisha kasoro na kuwawajibisha watendaji wako wanaokuhujumu na tunaomba waalimu ambao hawajalipwa tangu mwanzo wa semester mwezi March walipwe na ubabaishaji usiwepo tena.