JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa dawati hilo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Irene Mayunga ameongeza kuwa walimu wanayonafasi kubwa kuzitambua changamoto wanazopitia wanafunzi kutokana na muda mwingi kukaa na watoto hao ambapo amewaomba kushirikiana kwa karibu na dawati hilo ili kuzimaliza changamoto za ukatili pindi zinapotokea.
A/INSP Irene amewaomba wanafunzi hao kutokukaa kimya pindi wanapoona ama kufanyiwa vitendo vya ukali huku akiwaomba kuzifikisha kwa walimu wao ama viongozi wa dini ili wachukuliwe hatua za kisheia watakao bainika kufanyia ukatili wanafunzi hao.
Koplo Stella akatumia fursa hiyo kuwakaribisha walimu katika dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Nyamagana kupata elimu katika masuala mabalimbali juu ya ukatili na vitendo vya ukatili ili kuwa na uelewa wa vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika Jamii.
Soma :
~ Uliwahi kutamkiwa neno gani baya na Mwalimu wako?
~ Mwaka 2023 kulikuwa na Makosa 37,448 ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania, 15,301 yalikuwa kwa Watoto