TANZIA Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo cha Diplomasia, Dkt. Ahmed Mtengwa afariki dunia

TANZIA Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo cha Diplomasia, Dkt. Ahmed Mtengwa afariki dunia

Habari kwenu ndugu zangu.

Aliyekuwa mkuu wa Idara ya Uchumi wa Chuo cha Diplomasia Kurasini Dar Es Salaam amefariki Dunia mapema leo.

Dkt. Mtengwa alifariki katika hospital ya Muhimbili alipokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwao Masaki DSM.

Pumzika kwa amani Dkt. Mtengwa poleni wanataaluma.

Hiiiiii bagosha!

Hadi aFe nani ndiyo tugutuke?

Tusichuliane wandugu.

Mbona si kila kifo kuwa ni mipango ya Mungu?
 
Aisee yaani kila nikilog in nakutana na Tanzia kuna kitu hakiko sawa kwa kweli ni kweli watu walikuwa wanafariki hapo kabla lakn hii ya sasa imezidi tuweni waangalifu tunawe mikono, tutumie sanitizer tupia na barakoa haikupunguzii kitu ukitenda hayo ila itakusaidia kujiepusha hata kama siyo corona utajiepusha na magonjwa mengine yaambukizwayo kwa njia ya hewa.

Tumepewa maarifa tuyatumie, afya yako inalindwa na wewe binafsi na siyo mwingine
 
Umeona eeh. Sosho media zote zimejaa TANZIA tu, mpaka tunaogopa kuzifungua
 
hizi ni taarifa tu ya watu waliokuwa kwenye vitengo au maarufu, sijui sisi wengine idadi ikoje..
 
Ukisoma kwa Bible kuna story ya Yona, sasa walivyona Jahazi inazama na watu wote wako busy kusaidia jahazi isizame ndiposa wakagundua kuwa iko simblisi moja imetulia, hata haijitingishi. Kura zikapigwa na kura za kishindo zikampata yeye wakaaamua kumtosa kwa bahati Na bahari ikawa shwari Mara moja.

Mutafuteni Yona wenu Tz, lazima Kuna Yona. Huenda amejificha pahali mimi sijui.
pia usisahau Yohana kwa kingereza ni John.

😷
 
Mbona matangazo ya vifo redioni hushituki na kila siku huwa Kuna matangazo ya vifo.
Muda ninaosikiliza redio huwa hakuna matangazo ya vifo mkuu. Tena sikumbuki lini niliyasikia. Redio huwa nasikiliza kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 12.30 asb, then naingia kwa kaisari. Baada ya hapo nasikiliza tena kuanzia saa 12 jioni dira ya dunia.
 
Rest well Ahmed
Pole sana kwa familia na wote walioguswa na msiba
 
Innaa lillahi wa innaa ilayhi raajiuun, Allah ampe kauli thaabit brother na amsamehe makosa yake, aamin.
 
Back
Top Bottom