And this is exactly ambacho Magufuli anakipigia kelele kila siku ila watu wanalalamika eti uchumi umedorora. Uchumi upi huo?? Sasa kweli kama mtu aliyekuwa anapata tenda ya kushona sare za ATC Hong Kong.....leo hii si lazima alie?
Chifu, tatizo moja alilonalo Magufuli ni kuwa na a generalised viewpoint kwamba watumishi wa umma ni wezi na watu matajiri ni mafisadi. Hii ni hatari sana! Inakuwa hatari zaidi kwa namna ambavyo anajiweka yeye kuwa si mwizi/fisadi, ila wewe, mimi, wale na yule ndiyo wezi/mafisadi. Na kauli zake (pamoja na waziri wa fedha - wote PhD holders!!) kwamba 'wapiga dili' ndiyo wanalalamika ni za ajabu sana kutoka kwa mtu anayepaswa kuwa analytical na mwenye substance. Jitihada za kupingana na uhalisia zingeelekezwa kwenye kupambana kweli na corrupt system, ndani ya mwaka huu mmoja kungekuwa na ishara za mafanikio.
It is really painful lakini at some point what Magufuli is doing was bound to happen. Si kwamba hiki kibano cha Magufuli wengine hakitufikii. We are all enduring this pain. Lakini what is the way forward?
Naamini kwa miaka 55 ya Uhuru, kuwa na hilo swali "what is the way forward" ni ishara ya kufeli kwa serikali zilizotawala taifa hili.
Kwa mtazamo wangu, njia mojawapo wa kutoka hapa (haswa kwenye mfumo wa kifisadi, ambapo rushwa ipo institutionalised) ni kuandika katiba mpya itakayotengeneza mifumo mipya ya kiutendaji katika kuendana na mabadiliko ya kiutawala, kiteknolojia, kiuchumi, kijamii n.k. ambayo yametokea tangu kutengenezwa kwa katiba ya mwaka 1977. Tunahitaji katiba ambayo itaweka misingi na mifumo ya kitaasisi itakayoiongoza Tanzania kwa miaka 100+ ijayo. Justifications za 'one-man army' zinazotumika sasa, bado sijazielewa, kwa sababu tatizo la nchi yetu siyo uwepo wa mtu mkali, anayefokafoka na anayeogopwa! Maana hili limesha-prove failure; kwani licha ya ukali na ufokaji wake, bado rushwa na uzembe unaendelea. Uwepo wa taasisi imara na mfumo wa kiutawala unaowapa wananchi nguvu zaidi, utawachuja hao wezi na wazembe, bila ya kusubiri rais afoke au akaripie watumishi.
Kuna walioona mbali. Tukaona hela ya umma ni haki ya elites! Mtu unaanzisha biashara ukiwa unalenga pesa ya umma (kupiga). Lazima biashara za namna hiyo zife kifo cha mende! maana leo unaambiwa lipa kodi (kitu ambacho hukutegemea kwa sababu shareholder wa kampuni alikuwa ni waziri Fulani)...leo unaambiwa mahesabu yakaguliwe na upeleke returns TRA....hukuwahi kuwaza hilo..I mean tumeishi kwa ujanja ujanja mno.
Hili ndilo uwa linanishangaza kutoka kwa Magufuli's advocates: Magufuli amekuwa sehemu ya mfumo huo wa 'kiujanja ujanja' kwa miaka 20. Na kwa kipindi chote sijawahi kumwona au kumsikia akikemea huo ujanja ujanja au kujiuzulu katika kuonyeshwa kutoridhishwa na huo ujanja ujanja. Lakini alichokifanya ni naye kutumia ujanja ujanja katika kuuza nyumba za serikali (utasema ulikuwa uamuzi wa baraza la mawaziri, lakini yeye si ndiye aliyekuwa waziri mhusika, hivyo ndiye aliye-table hilo wazo kwenye baraza, siyo?) na kununua kivuko kibovu cha MV Dar es Salaam. In fact, nakumbuka kulikuwa na scandal ya yeye kuongwa fedha na wahindi waliokuwa wakitengeza nyavu za kuvulia samaki zilizokuwa hazitakiwi kisheria! Ndiyo maana kwa maajabu, Magufuli alipambana na watumiaji wa nyavu hizo (wavuvi) badala ya kupambana na wazalishaji (kwa kutumia common sense, alipaswa afanye kinyume na alivyofanya).
Jambo moja ambalo anaweza kulifanya na nikamwona ni true reformist ni kutuomba radhi watanzania (kwa niaba ya serikali za CCM, alizokuwa ndani yake) kwa madudu yaliyofanyika na serikali alizokuwa kiongozi mwandamizi. Huo utakuwa mwanzo mzuri wa kusonga mbele.
Biashara nyingi Tanzania zilishamiri based on false assumptions. Very few and genuine business will survive in this period. And that will be the beginning of our journey.
Hapa tena nasisitiza juu ya upekee wa Magufuli miongoni mwa viongozi waandamizi waliokuwa chanzo cha kushamiri kwa biashara za namna hiyo! Je, alikemea hilo? Kama siyo, kwanini hakufanya hivyo? Utasema hakuwa na mamlaka. Sawa, lakini kutokuwa na mamlaka hakukumzuia yeye kulisemea na kumshauri mwenye mamlaka afanye vile Magufuli alivyoona sahihi. Utasema alimshauri lakini hakushaurika, well, hili litakuwa ni vigumu kuli-prove. Lakini hata kama hakushaurika, kiongozi makini na aliye principled anapoona ushauri wake haufanyiwi kazi, ukaa pembeni (stepping down) ili historia isimhukumu kama mshiriki wa mfumo huo mbovu. Je, alifanya hivyo? Kama hapana, kwanini hakufanya?
Tuanze upya. Tujifunze kulipa kodi. Kuheshimu mali za umma. Ukipewa gari ya serikali kwa cheo chako. Uiogope kuipeleka kwenye harusi au kuibebea mkaa simply because you had a trip mkoani.
Hapa nakubaliana nawe kwa asilimia zote. Ni kweli watanzania hatulipi kodi kabisa (ukiondoa wafanyakazi walio kwenye mfumo rasmi). Lakini ni vyema kutambua kwamba mahala popote duniani serikali ndiyo inapaswa iweke mifumo ambayo itafanya watu walipe kodi. Yaani ni lazima serikali 'ilazimishe' watu walipe kodi. Serikali isitegemee watu watajitolea kulipa kodi; hakuna binadamu kama hao. Na la muhimu ni vyema Rais naye akawa mfano kwa yeye kuanza kulipa kodi (baada ya kuweka in public mshahara wake na mishahara ya viongozi waandamizi).
Hilo la matumizi mabaya ya magari ya serikali, nalo haliwezi kuondoka kama serikali haitoondoa hizo privileges! Ni heri kuwalipa watumishi mishahara mizuri kuliko kutoa privileges kama magari, nyumba n.k. Hapa tunapaswa kuiga jinsi mataifa yaliyoendelea yanavyofanya. Haiwezekani makamu mkuu wa chuo apewe magari matatu ya serikali. Ningekuwa ni maamuzi yangu, viongozi waandamizi wakuu (rais, makamu, pm, spika na cj) tu ndiyo ningewapa privileges za gari na nyumba! Tena siyo magari ya kifahari kama wanayotumia sasa! Kwa wengine wote, watumie magari yao binafsi (na kukodi kutoka kwenye government car pool pale wanapokuwa na safari za kikazi za nje ya wanapoishi). Nyumba wakae kwenye za kwao; ila nitawalipa mishahara mizuri. Ningeondoa kabisa hizo privileges kwa viongozi waandamizi wastaafu, ambao wanapata 80% ya mishahara (kama sikosei) ya viongozi waandamizi wa sasa. Hawa ningewepa pensheni kutokana na kile walichochangia walipokuwa watumishi.
Ukipewa madaraka siyo passport ya kujitajirisha. Ukipewa dhamana ya kufanya manunuzi..unataka 50% ya pesa iingie mfukoni mwako. How can we move on like this? Pathetic!
Success starts with discipline. Tuanzie hapo.
Kwa hakika, nakubaliana nawe katika hili pia. Ingawa pengine tunaweza kutofautiana katika namna ya kuondoka hapa! Hadi sasa sioni utaratibu anaoutumia Magufuli utaweza kututoa hapa na kusonga mbele! Huko very mechanical, rigid na selective. Taifa linahitaji fluid na flexible mechanisms za kutupeleka mbele! Naamini tena, kwamba katiba itakayoweka mifumo imara ya kiutawala, kitaasisi na kiuongozi, na itakayowapa wananchi mamlaka kamili ndiyo suluhisho litakalotuwekea misingi (ambayo Mwalimu aliiweka, lakini imeshavunjwa baada ya Azimio la Arusha kutupiliwa mbali na uliberali mamboleo kushika hatamu).