Mkuu wa Kikundi cha Wagner Yevgeny Prigozhin, ametoa maoni yake juu ya mzizi wa matatizo nchini Niger

Cheki huyu mjinga mmoja ambaye anaamini bila misaada ya nguruwe wa Ulaya , waafrika hawawezi kujitegemea. Hizi fikra za utegemezi kama hujui zinadumaza ubongo na kudhoofisha akili yako.
Vipi ushawai kutengeneza chochote apo nyumbani kwako ambacho tunaweza kulitumia kwa kujitegemea? Au unatumia Tekinolojia ya China, EU, US na Urusi kunitukana. Naamaanisha una Tekinolojia hapo ya Kibantu? Kama unayo una haki ya kunitukana.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo ninayo.

Kwa hiyo wewe huna mpango mkakati wowote wa kujitegemeea na unadhani uliletwa duniani ili uishi kwa kuwategemea wazungu ?
 
Hawa watu ni wanyonyaji wanachukua resources zako za kuwatajilisha na wanakuacha masikini hebu fikiria mkuu 25% ya uranium ya EU inatoka Niger lakini wanapata 5% ya mapato ya mali yao.

Inchi 14 za Afrika zilizowahi kuwa makoloni ya ufaransa kwa pamoja zinamlipa ufaransa dollar billion 500 Kila mwaka.

Harafu anakuja mtu analaani haya mapinduzi ,huyo ni wa kumpiga na vibao kabisa apate akili.
 
Sio vibao watu kama hao ni risasi tu
 
Jamaa ana hoja fikirishi....hizi operations za UN na kupambana na ugaidi ni miradi ya watu tu kuvuna pesa.
 
Ndiyo ninayo.

Kwa hiyo wewe huna mpango mkakati wowote wa kujitegemeea na unadhani uliletwa duniani ili uishi kwa kuwategemea wazungu ?
Kama Baba nimemkuta ana copy na ku paste, Viongozi hivyo hivyo, sasa Mimi nikienda tofauti si ndo CCM wataniita nawachelewesha?. Kama unacho cha tofauti hongera sana, utafika mbali, na naamini nitauona ugunduzi wako kabla sijatoka duniani.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Kununua au kutumia teknolojia ya kigeni kwa manufaa yako sio kosa, maendeleo endelevu ni mchakato mrefu kuanzia kuwekeza kwenye elimu bora kwa raia wako, uhakika wa chakula cha kuwatosheleza na mengine mengi.
 
Ngoja tumsubiri mrusi afike,na baada ya miaka kadhaa tufanye tathimini.
DPW ambayo ndo mjadala wa kitaifa kwa sasa kwa sababu ya dhuruma ni ya ufaransa?
Majadiliano yanayoendelea Zambia kuhusu madeni makubwa ya China na kutaka kutaifisha miundo mbinu ya kitaifa imesimamiwa na ufaransa?

Ninachoweza kusema ni kwamba ulimwengu umekuwa wa kibiashara kuliko ubinadamu.
China ya Mao na urusi ya ujamaa alimaarufu kama wasoviet na sasa ni tofauti,kama nakudanganya watafute waajiliwa wa kampuni za kichina hapa nchini au za kirusi kama zipo uwaulize kuhusu maslahi ulinganishe na waajiliwa wa kampuni za magharibi ulinganishe unafuu uko wapi.
 
Wewe sio MoroOne, Wewe ni Moron
 
Chama kinachotuongoza ni photocopy ya ujamaa na kujitegemea na kina urafiki na chama cha uchina,
vipi kuhusu haki na usawa,au tunaangalia kwa kuwa kimedhibiti uhalifu wa kigaidi?
 
"Without Africa, France will slide down into the rank of a third [world] power."

—Former French President Jacques Chirac, March 2008
France ilikuwa superpower kabla haijaja Afrika, ilikuwa na gold reserve kabla ya kuja na hapa imekuja kuongezea kwa wizi. Tatizo la Waafrika ni kukurupuka bila strategies, na kuibiwa kutoka kwa bwana huyu kwenda kwa bwana yule bila kujipanga na kuja na terms zetu.
Hakuna nchi itatoka Ulaya au Asia ije kutukomboa kama sisi akili zetu ni za kizubaifu, wala hakuna superpower itakuwa third world country kisa imeondolewa influence ya Afrika.

Huwezi kujiliza kila kukicha na huchukui hatua, Algeria walipambana na Ufaransa hawakuwaita Wachina au Warusi kuja kuwaondoa. Leo hii Algeria inaweka terms zake. Misri ilipambania mfereji wa Suez dhidi ya Ufaransa na Uingereza hata kama Marekani iliisaidia Misri iliweka terms zake na haikushangilia tu na kisha kulala kwa kutegemea mabwana wengine. Ukiachana na North Africa wenye uarabu, sisi huku unakuta wanashangilia kubadili bwana kumleta mwingine ambaye hamna kitu atafanya cha maana sababu hakuna conditions kapewa, kujichekesha na kujipendekeza huku na kule.
 
Kwani Niger imesema inamtaka Bwana Mrusi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…