TANZIA Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Bugozi Musuguri afariki dunia

Sleep well General. Asante kwa kulitumikia taifa letu. Salute!!!
 
RIP Jenerali David Musuguri

Ulikuwa kiongozi wa division ya 20 ilopewa kazi ya kukamata miji muhimu ya Masaka na Mbarara.

Marehemu Musuguri aliwahi kuelezea kuhusu makombora yaloitwa Katyasha na ule mlima Boma ambao ulikuwa ni lazima utwaliwe na vikosi vya TPDF.

Mimi nilikuwa nikiketi na uncle wangu akinipa madini kuhusu vita hii ambayo ilikuwa na ulazima kwani upande wa Magharibi mwa Tanzania ulikuwa ukichukuliwa kimasihara na Iddi Aminina majeshi yake.

Kulikuwa na Brigedia za 201 (iloongozwa na marehemu Imran Kombe) 207 (iloongozwa na marehemu Brigedia John Walden) na 208 hizi zilikuwa ni "TPDF Special Forces" kukamata miji ya Masaka na Mbarara.

NB:
Mzee M7 na mazee PK walishiriki kwa upande wa majeshi ya Tanzania kusaidia sehemu ya uchambuzi wa taarifa za ujasusi.

Ndo maana kazi ilikuwa rahisi kwa komandoo Mahfudhi na co kushika kasri ya Amini kiulaini.

Ndo chanzo cha Iddi Amin kukimbia.

Ni historia ambayo haiwezi kusahaulika kwa wale tulosimuliwa.
 
Haya nijibu swali langu.
Je, tulishikiwa bunduki kutoka kwenye ujamaa kuingia kwenye ubepari?
Athari za vita ya Kagera ndio sababu kubwa ya watanganyika kuingia kwenye ubepari.
Unakataa halafu unakubali indirect.
Nyerere na wenzake wameharibu nchi
Wakati Nyerere na wazee wenzake wakiharibu hii nchi, wewe wazee wa kwako walikuwa wapi kuokoa nchi isiharibiwe? Au na wewe unatoka kwenye familia/ukoo wa viazi ambao kazi yao ni kukaa wakilaumu bila kuchukua hatua yoyote?
 
Idi Amin aliwahi kusema hapa "Afrika kuna Mafield Marshal wawili tu,Idi Amin Dada na David Musuguri".

Yaani Idi Amin mwenyewe alikuwa anakiri huyu Musuguri alikuwa shida haswaaa. Si unajua waliwahi kufanya kazi kwenye Jeshi la Mwingereza (KAR)?
 
RIP JEMBE MSUGURI
 
Sema ujamaa wao mm siuelewi.
 
Sema ujamaa wao mm siuelewi.

Pengine sababu wote wanatokea mkoa mmoja. Hata hivyo, nafasi hizo sio za upendeleo. Hawa walikuwa wanajeshi wa wakoloni.
Baadae wakawa wanajeshi wa Jeshi letu. Na pengine kule kwao, kuwa mwanajeshi ilikuwa hadhi kubwa. Wakajiunga kwa wingi.
Kule kwetu kusini, kuchonga vinyago was a big deal. Na kucheza ngoma za kutoa mwali. Jeshini walijiunga watu wachache sana.
 
Elimu ya wa missionary ili wakuta kule mapema sana
 
Kama alikuwa Mkuu wa Majeshi 1980 had 1988, inakuwaje yeye aliongoza vita vya Kagera vya 1979?

Anyway, jamaa ameondoka kaacha Landcruiser mpya walizopewa kuwapooza wakuu wa mejeshi wastaafu wakati wa kimbembe cha kuuzwa kwa bandari!😀
Soma makala kuhusu vita ya Kagera na majemedari walioongoza vita hiyo. Utafahamu kila kitu na kwa nn ilikuwa hivyo.
 
Sijaona uhusiano wa biograph yake na pale Mbezi Kwa Msuguri.

Japo tunaambiwa ni kwake ila wasifu hauonyeshi kama aliishi Mbezi.
 
Kama alikuwa Mkuu wa Majeshi 1980 had 1988, inakuwaje yeye aliongoza vita vya Kagera vya 1979?

Anyway, jamaa ameondoka kaacha Landcruiser mpya walizopewa kuwapooza wakuu wa mejeshi wastaafu wakati wa kimbembe cha kuuzwa kwa bandari!😀

..Vita na Iddi Amin vilikuwa na awamu mbili.

..awamu ya kwanza ilikuwa ni kukomboa ardhi ya Tanzania eneo la Kagera iliyokuwa imetekwa na majeshi ya Uganda.

..awamu ya pili ilikuwa ni vita ndani ya Uganda kuyapiga majeshi ya Iddi Amin ili yasiendelee kuishambulia Tanzania.

..awamu ya kwanza ya vita kamanda wake alikuwa ni Brigedia Tumainieli Nderangusho Kiwelu.

..awamu ya pili iliongozwa na Brigedia David Bugozi Musuguri.

NB:

..Meja Jenerali Abdalah Twalipo alikuwa Mkuu wa majeshi wakati wa vita vya Kagera / Uganda.

..Musuguri aliteuliwa kuwa Mkuu wa majeshi baada ya vita vya Uganda kuisha.

..Kiwelu alikuwa Mkuu wa utawala jeshini wakati wa vita vya Kagera. Na baadae wakati wa utawala wa Raisi Mwinyi.

..Musuguri na Kiwelu walipanda vyeo na kuwa Majenerali [ 4 star general ] ktk Jwtz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…