Mkuu wa Majeshi wa Iran auawa na shambulizi la Israel

Mkuu wa Majeshi wa Iran auawa na shambulizi la Israel

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
28,477
Reaction score
40,278
Iran Leo wamepata pigo la kuondokewa na Mkuu wa Majeshi kufuatia shambulio la Israel. Apumzike kwa amani Jenerali

jukwaahuru__12678863.jpg

===
Kamanda Mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi Jenerali Hossein Salami, ameuawa katika shambulio la Israeli, mashirika ya habari ya Iran Tasnim na Mehr yameripoti, huku televisheni ya taifa ikiripoti kuwa makao makuu ya kikosi hicho yameteketea kwa moto na moshi ukifuka kutoka kwenye jengo hilo lililoko mtaa wa Pirouzi mashariki mwa Tehran. Mkuu wa majeshi ya Iran Mohammed Bagheri pia ameuawa katika shambulio hilo, televisheni ya taifa imesema.

Jeshi la Israeli limeripoti kuwa ndege zake za kivita zinaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya vituo vya kijeshi na nyuklia vya Iran.

"Marubani wetu wameshambulia na wanaendelea kushambulia maeneo ya kijeshi na malengo zinazohusiana na mpango wa nyuklia katika maeneo mbalimbali ya Iran," amesema msemaji wa jeshi la Israeli Brigedia Jenerali Effie Defrin.

Source: RFI Swahili
 
israel ni nchi mkakati wa kuanzisha vita ya 3 ya dunia,nashanga sana wakristo wa sasa wanavyoisapoti na hata hao waislamu kwa saudia nao siyo wale wenye misingi ya mtume.
 
Iran Leo wamepata pigo la kuondokewa na Mkuu wa Majeshi kufuatia shambulio la Israel. Apumzike kwa amani Jenerali
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC Swahili

Hawa ndio watu ambao wamethibitishwa kuuawa, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Irani:
  • Hossein Salami, kamanda mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
  • Gholamali Rashid, kamanda wa Makao Makuu ya Khatam-al Anbiya
  • Fereydoon Abbasi, mwanasayansi wa nyuklia na mkuu wa zamani wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran
  • Mohammad Mahdi Tehranchi, mwanasayansi mwingine wa nyuklia anayehusika na mpango wa silaha za nyuklia wa Iran
  • Mohammad Bagheri, Mkuu wa Majeshi ya Iran
  • Ali Shamkhani, mshauri mkuu wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, amejeruhiwa vibaya, kwa mujibu wa ripoti za Iran.
Anga ya Iran huwa iko emptiness sana viongozi wote hao wa ngazi za juu wanauliwaje kizembe hivo kwa wakati mmoja ina maana rada zao hazifanyi kazi au kuna uzembe mahali.

Namsikiaga Ibrahim Rabi pale Azam TV anasema Israel itachezea, Syria, Iraq, Kuwait , Lebanon lakini sio Iran
Haya sasa
 
israel ni nchi mkakati wa kuanzisha vita ya 3 ya dunia,nashanga sana wakristo wa sasa wanavyoisapoti na hata hao waislamu kwa saudia nao siyo wale wenye misingi ya mtume.
Kwani wewe hujui kuwa kila kitu Mungu alishasema kwenye Biblia? Hata hivyo vita vilishatabiriwa. Iran, Urusi Uturuki na nchi zingine za kiislamu zitaungana kuipiga Israel na Mungu atawashangaza! Na ndipo wote mtafahamu kuwa Israel ni taifa teule la Mungu na Mungu mwenyewe ndiye aliyewaleta hapo mashariki ya kati.
 
israel ni nchi mkakati wa kuanzisha vita ya 3 ya dunia,nashanga sana wakristo wa sasa wanavyoisapoti na hata hao waislamu kwa saudia nao siyo wale wenye misingi ya mtume.
Hao Middle East wote wanamsaidia Israel kwa hali na mali
Kuanzia US na UK wote wamo kwenye hii vita ya kummaliza nguvu za Iran

Hawajaanza leo hii mikakati ni tangu Iran/ Iraq war
Waarabu wote walikuwa upande wa Iraq kwa kila kitu ila walishindwa

Nguvu sio ya Israel peke yake bali nyuma yake kuna waarabu wengi wanaomuogopa Iran

Tukiacha ushabiki wa kidini hii vita ni kumuogopa Iran kuivamia Saudia na washiriki wake

Iran hana nguvu mbele ya wakubwa
Hata Gaza Waingereza wameshiriki sana kuwamaliza Palestinians
Rejea maneno ya Nigel Farage kuhusu involvement za UK huko Gaza
 
Back
Top Bottom