Habari wakuu. Kwa mujibu wa Rais wakati anawaapisha wakuu wa mikoa wapya leo Ikulu alitamka kuwa aliyemteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera alikuwa Mkuu wa Intelijensia ya jeshi ( MI).
Je ni sawa kutamka hadharani kuwa alikuwa Mkuu wa MI? Hakuwezi kumfanya akawa target zaidi huko anakoenda ukizingatia anaenda mpakani?
Pia naona Mkuu wa MI ni mkubwa sana kuwa RC. Sio mjuzi ila ni mtu ambaye yuko karibu sana na cheo kikubwa kabisa cha jeshi( mtanikoa kama ntakuwa nimekosea) kwani hata RC aliyekuwepo hapo Kagera kabala ya kusataafu alikuwa Meja jenerali tu. Huyu ni Brigedia jenerali