JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwassa ametoa kauli hiyo Februari 11, 2025 kwenye kikako cha wadau wa elimu kilichofanyika katika Kata ya Bakoba kikilenga kujadili mustakabali na mwenendo wa elimu.
Amesema kuwa anasikitishwa na vijana wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakiwatukana viongozi ambapo ameleza kuwa kufanya hivyo ni matokeo ya ufukara.
Aidha, amewataka wazazi kuongeza ushirikiano na walimu ili kuweza kuwezesha mazingira bora ya Watoto wao kupata elimu badala ya kuwaachia walimu mzigo mkubwa wa malez na makuzi ya Watoto.
Awalio akitoa taarifa na mwendo wa elimu katika kata ya Bakoba, Diwani wa kata hiyo Shaban Rashid amesema kuwa serikali imefanya makubwa katika kuboresha miundombinu mbalimbali katika shule zilizopo kwenye kata hiyo.
Aidha, amesema licha ya mafanikio hayo Shule ya Sekondari Bakoba inakabiliwa na changamoto kubwa ya viti na meza zaidi ya 300 hali inayopelekea wanafunzi wengi kukalia mabenchi na kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Chanzo: Wasafi FM