May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Leo asubuhi kwenye taarifa nimesikia ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Talak amewapa siku mbili Wafugaji walioingia mkoani hapo kuondoka.
Kwa upande wangu sioni kama hii imekaa sawa, anachopaswa kujiuliza Kiongozi huyu ambaye ni Muwakilishi wa Raisi wa nchi hapo Mkoani kwake ni "waende wapi ambako ndiko wanahitaji hilo tatizo analoona wamepeleka hapo Mkoani kwake?".
Kama ambavyo ni wajibu wa Raisi tuliyempa madaraka na usimamizi wa ardhi yetu basi na Wasaidizi wake Muwajibike kuangalia namna bora ya kuwafanya Wananchi wote bila kubagua Jamii yoyote wanaishi na kuifurahia ardhi yao.
Sikatai kwamba ujio au uwepo wao unaleta adha kwa wengine haswa wale wanaojishughulisha na Kilimo lakini hilo haliondoi ukweli kuwa bado ni wajibu wa mamlaka kuangalia watu wanaelimika na kufuata taratibu za nchi na si kufukuziwa kwingine.
Kwa hiyo mnawafukuza Watu wa nchi yako ile ile waende sehemu nyingine ndani ya nchi ile ile? hivi kesho na kesho kutwa mkikosa Nyama ndio mtawaita tena?.
Labda tu kama taarifa niliyoisikia ni kwa kifupi sana lakini ni aibu kwa taifa kuwa na viongoi wanaokimbia wajibu wao kwa kutoa tu amri za kutumia nguvu ili tu tatizo lihamie kwa wengine, na vipi kama huko mnapowafukuzia nako watafukuzwa?.
Ifike mahali kama Kiongozi unadhani jambo linakuzidi nguvu basi unyooshe tu mikono juu na kuwaachia waoweza.