Mkuu wa mkoa kuwaamuru Jamii moja kuondoka mkoani haijakaa sawa

Mkuu wa mkoa kuwaamuru Jamii moja kuondoka mkoani haijakaa sawa

Hivi kwa nini wafungaji wasiwe wananunua maeneo yao wenyewe ya kuchungia kama mkulima anavyofanya..
Maana wao kazi ni kupeleka kwenye maeneo ya wezao wakati ,kila mtu ardhi kanunua hajapata bure.
Wanatakiwa wawajibike na kazi zao,hapo ndo watapata mapato makubwa kwenye mazao yao.
Tusiendelee kuendekeza huu ujinga.
Sasa wenye majukumu ya kuwaelimisha na kusimamia utekelezaji wa haya si ni sisi tukiongozwa na Vionozi wetu?.

Hili tatizo la Wafugaji na Wakulima ni matokeo ya kuweka uonozi dhaifu haswa huku kwenye ngazi za chini...Mamlaka za juu zinakuwa na vipaumbele vyake linapokuja swala la uongozi ngazi za chini na kusahahu kabisa umuhimu na unyeti wa hilo eneo.

Hakuna kinachoshindikana ni suala la kuweka utaratibu tu na Raia yeyote awajibike kwa taratibu za nchi.
 
Naona kalewa madaraka..hao wafugaji waende wapi??wakati mkonwa lindi robo tatu ni mapori yasiyo na kazi..hizo ng'ombe wanazipenda tu zikiwa buchani na kwenye mabakuli yao wakila nyama na supu.

Wafugaji wa nchi hii wanaonewa sawa ndani ya nchi yao.

#MaendeleoHayanaChama
Yani wee acha tu
 
Hapo ndio tatizo linapoanzia mapori yasio na kazi wakati ni maeneo ya watu uingize tu mifugo bila ruhusa ya muhusika
Kama ni kweli yapo mapori kwa nini Great Thinkers wkayageuza hayo yakawa miradi ya kuingiza pesa?.

Ipo pesa nyingi sana kwa Wafugaji ni suala la kutumia akili tu...hizi pesa tunawaachia wanazitumia vibaya kwa Viongozi wa ngazi za chini za Kijiji na ndio chanzo kikuu cha kuleta mifarakano ya Wakulima na Wafugaji.
 
Leo asubuhi kwenye taarifa nimesikia ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Talak amewapa siku mbili Wafugaji walioingia mkoani hapo kuondoka.

Kwa upande wangu sioni kama hii imekaa sawa, anachopaswa kujiuliza Kiongozi huyu ambaye ni Muwakilishi wa Raisi wa nchi hapo Mkoani kwake ni "waende wapi ambako ndiko wanahitaji hilo tatizo analoona wamepeleka hapo Mkoani kwake?".

Kama ambavyo ni wajibu wa Raisi tuliyempa madaraka na usimamizi wa ardhi yetu basi na Wasaidizi wake Muwajibike kuangalia namna bora ya kuwafanya Wananchi wote bila kubagua Jamii yoyote wanaishi na kuifurahia ardhi yao.

Sikatai kwamba ujio au uwepo wao unaleta adha kwa wengine haswa wale wanaojishughulisha na Kilimo lakini hilo haliondoi ukweli kuwa bado ni wajibu wa mamlaka kuangalia watu wanaelimika na kufuata taratibu za nchi na si kufukuziwa kwingine.

Kwa hiyo mnawafukuza Watu wa nchi yako ile ile waende sehemu nyingine ndani ya nchi ile ile? hivi kesho na kesho kutwa mkikosa Nyama ndio mtawaita tena?.

Labda tu kama taarifa niliyoisikia ni kwa kifupi sana lakini ni aibu kwa taifa kuwa na viongoi wanaokimbia wajibu wao kwa kutoa tu amri za kutumia nguvu ili tu tatizo lihamie kwa wengine, na vipi kama huko mnapowafukuzia nako watafukuzwa?.

Ifike mahali kama Kiongozi unadhani jambo linakuzidi nguvu basi unyooshe tu mikono juu na kuwaachia waoweza.
Mtanikumbuka
 
Hayo mawazo ya kijamaa ,kwa nini wasinunue tu hata ekari mia wafuge wao wenyewe mpaka wakachukue maeneo ya wengine..
Wauze ngombe wanunue ardhi .sio kuinhia maeneo ya watu.
Sasa si muwaongoze hilo lifanyike?.

Sasa kama nyie Viongozi mtaishia kuwafukuza tu mnataka waishie wapi, Msumbiji?.
 
Hawa walisha pewa maeneo huko kilwa, sasa kule Nachimgwea wanako uwa wenyeji, kwa kugombea kulisha mifugo mashamba ya watu, wanastahili kuindolewa.

Nachimgwea Rwangwa ndizo zinazolisha Lindi na Mtwara, ukihamishia wafugaji umewauwa.
Mkuu, hili ni suala la uongozi imara tu, hakuna linaloshindikana na hakuna aliye juu ya sheria.

Uongozi imara na matumizi ya akili, mbona imewezekana kuwahamisha wale wa Ngorongoro kwenda Handeni?.

Tatizo hapa sio wanafanya nini, tatizo ni Viongozi wanatatua vipi hilo tatizo?.
 
Ahsante kwa kutujuza, lakini habari ngumu kama hizi ni bora zikawa na maelezo ya kutosha na sio kurukia rukia tu.
Wafugaji wa lindi eneo gani walioambiwa watoke? Au lindi yote?

Kwa sababu zipi?!!! Au hakuna sababu amekurupuka tu mkuu wa mkoa?!!

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya muda gani wa kuisikilizia amri (km ipo) iliyotolewa na setikali?!!! Au hakukuwa na vikao na makubaliano ya kabla ambayo pengine yamekuwa violated ndo maana imekuja amri hii?!!!!

N.k
Kwenye andiko nimetahadharisha kwa maneno "labda kama hiyo taarifa ipo nusu" mimi nime respond kwa nilichokisikia...sasa kama kuna maelezo ya ziada Mtu alete ndio maana ya jukwaa Mkuu, tofauti na Gazeti.
 
Ifikie wakati haya makabila mawili ya Wasukuma na Wamasai yabadilishe mifumo yao ya ufugaji! Nomadic livestock kwenye karne hii ya 21 ni upuuzi.

Aina hii ya ufugaji inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, ukame, na pia migogoro ya ardhi. Watafute maeneo, watulie! Waanzishe ufugaji wa kisasa.
Mkuu hata mimi pointi yangu inaegemea hapo hapo, TUWASAIDIE, TUWABADILISHE, tusiishie kuwakataa tu kama vile ni Jamii isiyotuhusu.
 
Sasa mtu unafuga ng'ombe 500 wa nini
Wafugaji wafunge mifugo kiasi ikikomaa anakuwa anavuna anapata pesa
Kuzurula na mifugo karne hii haiko sawa
Wapewe mafunzo na mbegu bora wafuge kisasa
Ukiwa na ng'ombe 10 tu wa kisasa unakuwa tajiri tu bila hii migogoro
Mimi nadhani tuishi kwa akili na hawa Wafugaje ili tuweze kula nyama ikiwezekana hata kwa gharama nafuu.

Ikiwezekana kila Mkoa watengewe kambi, ziwe na Majosho, Mabwawa, Madaktari wa mifugo...Hivi inashindikana vipi wakati hao mifugo wenyewe ni pesa?.

Ni wakati sasa sisi jamii tunufaike na hao Ng'ombe badala tu ya kushindana nao miaka nenda rudi.
 
WAFUGAJI WAMEKINUKISHA WENYEWE, WAMELISHA NG'OMBE ZAO, KWENYE MASHAMBA YA CHAKULA, WAKULIMA WAMEHOJI, WAO JIBU LAO NI KUUWA.
 
Ng'ombe zaidi ya maelfu utawafuga eneo la heka 100.

Hapo bado maji malisho wakati wa kiangazi..sio mchezo.

Mimi nashauri mkoa wa lindi uwe mkoa wa wafugaji.

#MaendeleoHayanaChama
Nenda kapate somo kwa waarab wa ihefu au kigwangala pale Mvomero
 
Ifikie wakati haya makabila mawili ya Wasukuma na Wamasai yabadilishe mifumo yao ya ufugaji! Nomadic livestock kwenye karne hii ya 21 ni upuuzi.

Aina hii ya ufugaji inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, ukame, na pia migogoro ya ardhi. Watafute maeneo, watulie! Waanzishe ufugaji wa kisasa.
Amina
 
WAFUGAJI WAMEKINUKISHA WENYEWE, WAMELISHA NG'OMBE ZAO, KWENYE MASHAMBA YA CHAKULA, WAKULIMA WAMEHOJI, WAO JIBU LAO NI KUUWA.
Duh, haipaswi kufikia huko kabisa.
 
Ahsante kwa kutujuza, lakini habari ngumu kama hizi ni bora zikawa na maelezo ya kutosha na sio kurukia rukia tu.
Wafugaji wa lindi eneo gani walioambiwa watoke? Au lindi yote?

Kwa sababu zipi?!!! Au hakuna sababu amekurupuka tu mkuu wa mkoa?!!

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya muda gani wa kuisikilizia amri (km ipo) iliyotolewa na setikali?!!! Au hakukuwa na vikao na makubaliano ya kabla ambayo pengine yamekuwa violated ndo maana imekuja amri hii?!!!!

N.k
Nazani juzi utakuwa umepata wasaa wa kuangalia taarifa ya habari ITV na umeona wasukuma walivyo kuwa wana lisha ktk mashamba ya wakulima ktk wilaya za kibiti rufiji na mkoa wa lindi

Yeye kama kiongozi wa ulinzi na usalama wa mkoa, anapo Ona kuna jambo hatarishi kwenye eneo lake la kiutawala/mamlaka basi ana paswa kuchukua hatua shahiki kuepusha uvunjifu wa amani kutokea

Na hili mh rais kali zungumza pale kigamboni, kuwa wafugaji wana fanya uharibifu mkubwa na pia hayupo tayari kusikia hizi jamii mbili zikifanya mauaji ya visasi nk

Akataka hatua zichukuliwe kudumisha amani na utulivu
 
Ng'ombe zaidi ya maelfu utawafuga eneo la heka 100.

Hapo bado maji malisho wakati wa kiangazi..sio mchezo.

Mimi nashauri mkoa wa lindi uwe mkoa wa wafugaji.

#MaendeleoHayanaChama
Lindi ukiwa mkoa wa wafugaji na hao wenyeji wakulima waende wapi? Hao wafugaji mikoa yao ndiyo ya wafugaji kwanini wametoka huko!
 
Wafugaji wa nchi hii hawana amani ndani ya nchi yao kila mahala wanafukuzwa.

#MaendeleoHayanaChama
Hivi wewe ufugaji wa kuswaga Ng'ombe unaufahamu wewe? Mfano leo mtu na Ng'ombe zake leo yupo tegeta kesho kutwa yupo g/mboto, baada ya wiki Mbagala sasa humo anamopita ni mapori tuu hakuna mashamba ya watu?
 
Hayo maeneo yanayo itwa mapori, wenyeji wameishi huko kwa miaka nenda rejea bila mtafalku, lakini hawa wafugaji walio kuja juzi kuanzia mwaka 2000+ ndio chanzo cha migogoro

Hawa chagui kwa kulisha mifugo, kwenye hifadhi na mapori tengefu, kwenye mashamba na vyanzo vya maji

Ni uharibifu ambao tukiukalia kimya madhara yake ni makubwa mno mno...

Ndio kukosa maji nk... Dar wana taabika miundo mbinu ipo lakini maji hamna
 
Maisha ya wafugaji ndivyo yalivyo huwezi kaa sehemu moja una ngombe wengi..sa100 hakuji hata kufuga kuku atajuaje kuhusu mifugo kama ng'ombe na mbuzi.

#MaendeleoHayanaChama
Kwahiyo bora kuchungia katika mashamba ya watu?
 
Hivi wewe ufugaji wa kuswaga Ng'ombe unaufahamu wewe? Mfano leo mtu na Ng'ombe zake leo yupo tegeta kesho kutwa yupo g/mboto, baada ya wiki Mbagala sasa humo anamopita ni mapori tuu hakuna mashamba ya watu?
Mimi natoka jamii ya waswaga ngombe naelewa madhara yake...

Huo ufugaji ni tatizo
 
Back
Top Bottom