Mkuu wa mkoa kuwaamuru Jamii moja kuondoka mkoani haijakaa sawa

Wafugaji wa Tanzania wana ufugaji wa kijima wa kutembea na mifugo sehemu kubwa.

Serikali pia haijawekeza katika kuwawezesha na kuwafundisha kufanya ufugaji wa kisasa wa kutumia sehemu ndogo na teknolojia ya kisasa.

Halafu wanakutana wote wamekosea, wafugaji wamekosea kwa kuwa hawafugi kisasa, katika nchi ambayo watu wanazidi kuongezeka lakini arhi haiongezeki, na serikali nayo imelala katika sera za "zaeni, nitasomesha" wakati inashindwa kuwapanga wafugaji wake.

Nchi imekosa uongozi kutoka wakuu serikalini, pia imekosa wananchi wanaojiongeza wenyewe.

Kifuatacho ni majanga matupu.
 
Yaani mkoa kama Katavi ulikuwa na mapori mazuri ya uhifadhi mengine yalikuwepo tu wananchi wanaokota kuni tu daa wafugaji sasa wasukuma walikuwa wanatembea pori kwa pori mpaka kule, wanaitana tu bila mpangilio wowote sahizi nikama tu hakukuwahi kuwa na msitu
 
Yaani wale wanaviburi kama ng'ombe zao.
 
Kwahili wakulaumiwa ni hao hao viongozi wa serikali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwenye andiko nimetahadharisha kwa maneno "labda kama hiyo taarifa ipo nusu" mimi nime respond kwa nilichokisikia...sasa kama kuna maelezo ya ziada Mtu alete ndio maana ya jukwaa Mkuu, tofauti na Gazeti.
Kichwa cha habari kimelaumu, directly!!
 
Yeye ndio aondoke akalee watoto wake kazi imemshinda
 
Ng'ombe zaidi ya maelfu utawafuga eneo la heka 100.

Hapo bado maji malisho wakati wa kiangazi..sio mchezo.

Mimi nashauri mkoa wa lindi uwe mkoa wa wafugaji.

#MaendeleoHayanaChama
Sasa unataka ukawalushe ktk ardhi ya nani??
 
Zai has got some probs!Hajui kutatua migogoro?Utatuzi wake ni ku-expell wafugaji kutoka huko kijijini?Atulize wenge na hiyo burka yake!
 
Sasa si muwaongoze hilo lifanyike?.

Sasa kama nyie Viongozi mtaishia kuwafukuza tu mnataka waishie wapi, Msumbiji?.
Mpaka akili iwakae sawa,binadamu timamu huwez fuga ng'ombe 200 kwa kutwgemea kuzurua na kuwalisha mifugo yako mashamba ya watu,faida ya kilimo ni kubwa ktk nchi kuliko kufuga,ni bora tupoteze wafugaji tubaki na wakulima!!
 
Wizara ya mifugo itafute mbinu ya kuelimusha ufugaji bora, tunakoelekea siko kabisa
Tushaelimishana sana kiungwana,sasa ni muda ya kuadhibiana,hizi jamii za wafugaji ni tafsiri sahihi ya ukosefu wa ustaarabu,wakiadhibiwa watajifunza
 
Hao Wafugaji juzi wamemuua Mkulima kisa aliwafukuza kulisha Ngo'mbe kwenye shamba lake la Nyanya, baada ya kumuua wakamfukia kwenye migomba,
Wakulima nao wameua Wafugaji wanne,(kisasi)

Nakumbuka Magufuli aliwahi kuwaambia wapunguze mifugo na kila Kaya iwe na Mifugo ishirini(sina hakika na hii idadi) lakini pia wawe na utaratibu wa kuuza mifugo yao na Pesa wafanyie maendeleo kama kujenga nyumba za kisasa pamoja na ufugaji wa kisasa,

Kuna wajinga walipiga kelele kama hivi lakini leo tunaona tena madhara yake,

Serikali inapaswa kuweka sawa hili suala la ufugaji kiholela na kuja na suluhisho ambalo halitamuumiza yeyote.
 
Hakika ni tatizo kubwa.

Lakini hatuwezi kutatua kwa kuwafukuzia kwingine maana hata huko wataenda kuendeleza tatizo.

Wapewe muongozo na waelekezwe la kufanya na wasimamiwe maana hakuna aliye juu ya sheria.
 
Nashanaga Sana mtu anaye mbuguzi mfugaji kwa kauli Kama hzo

Supu na minyamaa wanojipakulia wanadhani inatoka wapi

Huku tukikosa lishe lawama
 
Ng'ombe zaidi ya maelfu utawafuga eneo la heka 100.

Hapo bado maji malisho wakati wa kiangazi..sio mchezo.

Mimi nashauri mkoa wa lindi uwe mkoa wa wafugaji.

#MaendeleoHayanaChama
Lindi na willaya nzimaa ya kilosa iwe ya kimkakati kwa ajili ya ufugaji tu
 
Maisha ya wafugaji ndivyo yalivyo huwezi kaa sehemu moja una ngombe wengi..sa100 hakuji hata kufuga kuku atajuaje kuhusu mifugo kama ng'ombe na mbuzi.

#MaendeleoHayanaChama
Mijitu inaongeaa Happ hata kufuga kuku hajawai unajuwa kula tu

Lindi na wilay nzima ya kilosa iwe ya wafugani PMj na nkasi ineo la wafugaji
 
Ila Kuna makabila mengine yapo hapa Tz kutesa Watu tu yaani wenzako wamelima tena kwa Kilimo duni wapate Posho Maisha yaende Mtu anaingiza mifugo shambani na ukiwa Mkali juu ya Shamba lako anakuchoma Mkuki wa Mdomo. Hata Kama ni Uhuru wa kwenda upendavyo lakini siyo kwa Hali hii.Wanasababisha njaa Ukame hivyo lazima serikali iainishe mikoa ya kufugia siyo kila sehemu kuwa ruksa kufuga Tena mang'ombe mengi .Kuna baadhi ya Mtindo wa ufugaji lazima upigwe marufuku tu kwenye maeneo ya uzalishaji Chakula. Msimlaumu Mkuu wa Mkoa kwa huu upuuzi wenu na kusababisha Uvunjifu wa Amani Kama mnavyofanya kule Morogoro
 
Hili ni tatizo na wala mimi siungi mkono mambo kuwa hivi.

Lakini pia bado naiona nafasi ya Mamlaka kugeuza hii changamoto kuwa fursa.

Kwa nini tusiwekeze kwenye kulima nyasi na kuvuna pesa kutoka kwa hao Wafugaji?, yaani unakuwa na ekari za nyasi na Mfugaji akija analipishwa kulisha Ng'ombe kwa muda watakaokubaliana.

Tusisahau kuwa hao Ng'ombe nao ni chakula pia, sasa ni vipi tukubali wageuke kero kwetu?, na kama Ng'ombe wapo wengi na wanafugwa hovyo kama wengi tunavyoami kwa nini sasa tusingekuwa tunapata nyama kwa bei nafuu?. Hamuoni kuwa hapo kuna udhaifu mahali? kama hawa Wafugaji wetu wana upungufu kwa ni vipi tena nanyi mnaowazunguka mnakosa namna bora ya kabadilisha mambo?.

Bado naamini tukitumia akili hawa Wafugaji tutawageuza baraka kwa nchi na badala ya kero kama ilivyo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…