LGE2024 Mkuu wa mkoa Tanga: Wasimamizi wa uchaguzi Tumieni 4R za Rais Samia

LGE2024 Mkuu wa mkoa Tanga: Wasimamizi wa uchaguzi Tumieni 4R za Rais Samia

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian Batilda Burian amewataka viongozi wote ambao wana nafasi za kusimamia michakato ya uchaguzi,kusimamia agizo la kutumia 4R za Rais Samia katika kufanya kazi zao za uchaguzi.

Amesema hayo wakati akitoa taarifa za michakato ya uchaguzi ulipofikia kwa mkoa wa Tanga na kusema kuwa hali ni shwari ,hivyo kwa kuzingatia agizo la kusimamia 4R za Rais litaweza kuondoa malalamiko na uvunjaji wa haki za wagombea ambao wameomba nafasi mbalimbali za kugombea uongozi.

Amesema lazima wote wahakikishe kuna kuwa na sababu za msingi za kukatwa jina la mgombea,kwani kila chama kina taratibu zake hivyo katika kuhakikisha demokrasia inakuwepo kila chama kipewe nafasi kwenye mchakato wa uchaguzi.

Ameagiza viongozi wa vyama rafiki endapo wanaona kuna sehemu haki haijatendeka kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa mkoa,ili kuweza kuchukua hatua zaidi na kuondoa malalamiko madogo madogo

Pia soma: Makalla: CCM itatumia 4R za Rais Samia katika hatua yake ya kuuteketeza kabisa Upinzani kabla, wakati na baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa


 
Yaani Sasa hivi tunaendeshwa na utashi wa mtu na siyo Sheria. So bad
 
Back
Top Bottom