Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam umenikosha sana leo sakata la wafanyabiashara Kariakoo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam umenikosha sana leo sakata la wafanyabiashara Kariakoo

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Umeongea kwa mamlaka dhidi ya wafanyabiashara, na umenikuna sana kiongozi. Umeonyesha ujasiri mkubwa kwa wananchi unaowaongoza Dar es Salaam. Umenigusa sana pale uliposema kama nchi inapeleka jeshi kupigana Congo, vipi ishindwe kulinda Kariakoo.

Dawa yao hao wafanyabiashara wanaotumwa na wanasiasa na kudhani wanamkomoa Rais ni kuhakikisha waliofunga maduka leo wasiyafungue hadi madai yao yatakaposikilizwa ili tuone wanamkomoa nani.

Ulinifurahisha zaidi uliposema serikali haishindwi jambo. Naamu, kabisa kabisa! Yaani wafanyabiashara muishinde serikali? Nyie wafanyabiashara Kariakoo mnaona serikali ni jambo dogo sana?

Halafu, najiuliza kwa nini ujinga huu hawakumletea Hayati Magufuli?

Nani yuko nyuma yao? Hivi mnataka Rais aweke pembeni 4R turudi enzi za Magufuli?

Kuna watu wanasubiri tu mama aweke pembeni 4R ili turudi tulikotoka maana mnafanya mchezo sana nyie wafanyabiashara.

Ni kweli RC Chalamila, wafanyabiashara wa Kariakoo wakwepa kodi wamekithiri, hawataki kukaguliwa. Serikali ikiamua kufanya uchunguzi, watakaobaki salama hawazidi 20 pale Kariakoo.

Kuna uhujumu uchumi mkubwa unafanywa na wafanyabiashara pale Kariakoo. Mfano mzuri, wanaotoa risiti pale Kariakoo hawazidi hata 100 kati ya watu milioni 3 wanaokwenda kupata mahitaji. Serikali inawavumilia sana, lakini leo mnataka kuichezea sharubu.

RC Chalamila, hotuba zako ni za kimamlaka, na hao waliogoma wanataka kuhatarisha usalama wa mkoa.

Ushauri kwa vyombo vya usalama: fuatilieni kwa kina mambo haya ya migomo pale Kariakoo. Nani anaanzisha movement hizi?

Anzeni na wale waliokuwa wakitoa kero kwa DC juzi, wale ndio wa kuanza nao. Wale mkiwapa kesi za uhujumu uchumi, hamtasikia tena upumbavu wa namna hii.

Asante, Mkuu wa Mkoa.

PIA SOMA

- Mgomo wa Wafanyabiashara ambapo Biashara zilifungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024.

- Chalamila kuwasili Kariakoo katika jitihada za kutatua mgogoro

- Baada ya Chalamila kuondoka Kariakoo, bado Wafanyabishara waliendeleza mgomo wa kufunga maduka.
 
Vitisho na mitutu haijawahi kuleta amani Wala maelewano,Ukisikia kariakoo kumebuma ujue hazina ya serikali imetikiswa,hapa lazima wajipange kutatua mgogoro la sivyo utasikia serikali yapoteza trillion Kodi ya serikali
 
Umeongea kimamlaka dhidi ya wafanyabiashara, umenikuna sana kiongozi, kiongozi umeonyesha ujasiri sana kwa wananchi unaowaongoza dar...
Kukaa kimya wakati mwingine ni busara sana kuliko 'kutapika' maneno machafu Kama hayo.

SIYO kila mtu ambaye yupo kimya ukadhani Hana la kusema au hajui kusema, la hasha!
 
Umeongea kimamlaka dhidi ya wafanyabiashara, umenikuna sana kiongozi, kiongozi umeonyesha ujasiri sana kwa wananchi unaowaongoza dar, umenikuna pale uliposema kama nchi inapeleka jeshi kupigana Congo vipi ishindwe kulinda kariakoo...
Unaposema Serikali haishindwi jambo unamaanisha nini?

1. Serikali imekiri mara kadhaa kushindwa kudhibiti Wala RUSHWA, na ndio sababu ya Kugawa Bandari!!

2. Serikali imeshindwa kusaidia Umaskini uwaondoke Watanzania na imekiri kushindwa!!

3. Imeshindwa kuzuia wizi wa kura katika chaguzi.

4. Imeshindwa kutuhakikishia USALAMA wa Maalbino, wanawindwa kama swala porini!!

5. Serikali imeshindwa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji!!

Sijui umeandika nini!!
 
Umeongea kimamlaka dhidi ya wafanyabiashara, umenikuna sana kiongozi, kiongozi umeonyesha ujasiri sana kwa wananchi unaowaongoza dar, umenikuna pale uliposema kama nchi inapeleka jeshi kupigana Congo vipi ishindwe kulinda kariakoo...
Unasema kwa wanaanchi anaowaongoza unasahau wafanyabiashara ndio wanaanchi wenyewe.90% ya Dar es Salaam ni biashara iwe kubwa au ndogo.

Sikiliza watu mamlaka bila kusikiliza watu ni kujidanganya.Je Kariakoo ibaki kuwa pango kama ilivyo Leo?

Haijuikani nani machinga na nani sio machinga?Usichojua ni kuwa startup business nyingi Kariakoo zinahangaika kwa kuwa na ushindani na biashara isiyo rasmi
 
Umeongea kimamlaka dhidi ya wafanyabiashara, umenikuna sana kiongozi, kiongozi umeonyesha ujasiri sana kwa wananchi unaowaongoza dar, umenikuna pale uliposema kama nchi inapeleka jeshi kupigana Congo vipi ishindwe kulinda kariakoo...
Walipe kodi hakuna lelemama
 
Back
Top Bottom