Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam umenikosha sana leo sakata la wafanyabiashara Kariakoo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam umenikosha sana leo sakata la wafanyabiashara Kariakoo

Vitisho na mitutu haijawahi kuleta amani Wala maelewano,Ukisikia kariakoo kumebuma ujue hazina ya serikali imetikiswa,hapa lazima wajipange kutatua mgogoro la sivyo utasikia serikali yapoteza trillion Kodi ya serikali
Ina maana kariakoo inazalidha Hela nyingi kiasi hicho Cha Kodi? m ona bajeti yetu inasuasua?
 
Unasema kwa wanaanchi anaowaongoza unasahau wafanyabiashara ndio wanaanchi wenyewe.90% ya Dar es Salaam ni biashara iwe kubwa au ndogo.Sikiliza watu mamlaka bila kusikiliza watu ni kujidanganya.Je Kariakoo ibaki kuwa pango kama ilivyo Leo? Haijuikani nani machinga na nani sio machinga?Usichojua ni kuwa startup business nyingi Kariakoo zinahangaika kwa kuwa na ushindani na biashara isiyo rasmi
Zile Biashara zisizo rasmi ndio zinaleta ugumu Kwa wale wanaolipa Kodi.Hao wamachinga wangetengewa maeneo mengine
 
Kwa Mtazamo wangu

TATIZO LA KARIAKOO NI ZAIDI YA WAFANYABIASHARA,WACHUUZI..LETS BE SERIOUS.

Tatizo la kariakoo haliwezi Kwisha ikiwa total supply chain ya mizigo inayouzwa kariakoo isiporekebishwa au kudhibitiwa kupitia maamuzi magumu na kutooneana haya wala aibu..

Bidhaa nyingi zinazouzwa kkoo zinaingizwa (Imported) toka China,India,Uturuki,Thailand,Vietnam,Zambia,Uganda,etc..Mfumo wa uingizaji na ulipiaji kodi wa mizigo husika ndio mzizi wa shida na tatizo lililopo na litakalokuwepo..

Cartel inayoratibu Logistics na supply chain ya mizigo ya wafanyabiashara wa karikoo isipodhibitiwa kila nyakati tutaona fukuto na migomo isiyohitaji siasa Bali utashi wa maamuzi magumu kudhibiti wahujumu uchumi tunaowalinda..

Mathalani,Mfanyabiashara akiagiza mzigo wa viatu Kwa kontena na kulipa ushuru stahiki kisha kuwa na nyaraka zote Za kikodi (Import duties,Port charges,Wharfage,VAT) inamgharimu milioni 45….NOTE:- Ila akiagiza mzigo huo huo kwa kutumia Logistics Cartels inamgharimu Milioni 15 tu pasipo nyaraka zozote lakini Ana uhakika wa kufikishiwa mzigo dukani au warehouse kwake pasipo usumbufu..

Sasa wale wafanyabiashara waliokuwa wakikomaa na kufuata taratibu stahiki wamejikuta wakishindwa kushindana ktk soko na kufirisika ama kufa kibiashara sababu ya ughali wa bidhaa dhidi ya wale wanaotumia Logistics Mafia..

On the other hand wanaotumia huduma za logistics cartel au mafia inawawia Vigumu sana kufanya compliance za kikodi sababu ya kukosa nyaraka muhimu kussuport mapana ya stock zao..Mauzo yao,returns zao..Hapa ndio kwenye shidaa haswaa…Wengi wana stock kubwa kuliko vielelezo vya manunuzi ya stock husika..Wamegeuka wachuuzi..Wanaouza ambacho hawana nyaraka Za wametoa wapi..SHIDA.

Logistics Cartel/Supply chain Mafia:-Ni kundi hatari lenye nguvu kupitia wanasiasa wakubwa waliopo na wastaafu..Wana ukwasi mkubwa na umaarufu mkubwa ktk Kiwango cha kuogopeka na Wakubwa wa TRA,Polisi,Etc..Wana nguvu mnooo ya kufanya wakubwa ktk mamlaka Za kodi watumbuliwe,Wafanyakazi wahamishwe,Wawe demoted..Wapate Stroke..Nina hakika hata CG wa TRA anawaogopa..Hana la kuwafanya..Inasemekana baadhi ya viongozi ni marafiki wakubwa..

Cartels hizi zimehodhi Supply chain Za uagizaji bidhaa,usafirishaji,Ulipaji kodi,Udanganyifu (under declaration&Falsa Declarations),Uzungushaji mizigo (Taarifa Za kampuni Za tracking devices Za mizigo ya transit zina mengi)..Wanamiriki makampuni ya uagizaji,Usafirishaji,Bonded Warehouses,ICD’s,CFS..yaani acha tu..

Kwa hakika tunapoteza kodi nyingi sana zinazoingia mifukoni mwa wachache tunaowaimbia mapambio ya utajiri na ubilionea huku wachache wakikamuliwa hata kuzirai kibiashara..Bila maamuzi magumu na dhabiti tutaendelea kukwama na kuumiza wasiostahili..

Tukiamua Tunaweza..Viongozi wenye dhamana Simameni kwenye haki na ukweli..
 
Umeongea kimamlaka dhidi ya wafanyabiashara, umenikuna sana kiongozi, kiongozi umeonyesha ujasiri sana kwa wananchi unaowaongoza dar, umenikuna pale uliposema kama nchi inapeleka jeshi kupigana Congo vipi ishindwe kulinda kariakoo...
Huyu jamaa ukute hajawahi kumiliki hata genge ktk maisha yake!

Unafikiri kumiliki biashara kariakoo na kulipa kodi ni mchezo? Huyo RC wako amewahi kuimiliki biashara yoyote na akapata faida na akalipa na kodi?

Machawa wa muwe na mipaka!
 
Umeongea kwa mamlaka dhidi ya wafanyabiashara, na umenikuna sana kiongozi. Umeonyesha ujasiri mkubwa kwa wananchi unaowaongoza Dar es Salaam. Umenigusa sana pale uliposema kama nchi inapeleka jeshi kupigana Congo, vipi ishindwe kulinda Kariakoo.

Dawa yao hao wafanyabiashara wanaotumwa na wanasiasa na kudhani wanamkomoa Rais ni kuhakikisha waliofunga maduka leo wasiyafungue hadi madai yao yatakaposikilizwa ili tuone wanamkomoa nani.

Ulinifurahisha zaidi uliposema serikali haishindwi jambo. Naamu, kabisa kabisa! Yaani wafanyabiashara muishinde serikali? Nyie wafanyabiashara Kariakoo mnaona serikali ni jambo dogo sana?

Halafu, najiuliza kwa nini ujinga huu hawakumletea Hayati Magufuli?

Nani yuko nyuma yao? Hivi mnataka Rais aweke pembeni 4R turudi enzi za Magufuli?

Kuna watu wanasubiri tu mama aweke pembeni 4R ili turudi tulikotoka maana mnafanya mchezo sana nyie wafanyabiashara.

Ni kweli RC Chalamila, wafanyabiashara wa Kariakoo wakwepa kodi wamekithiri, hawataki kukaguliwa. Serikali ikiamua kufanya uchunguzi, watakaobaki salama hawazidi 20 pale Kariakoo.

Kuna uhujumu uchumi mkubwa unafanywa na wafanyabiashara pale Kariakoo. Mfano mzuri, wanaotoa risiti pale Kariakoo hawazidi hata 100 kati ya watu milioni 3 wanaokwenda kupata mahitaji. Serikali inawavumilia sana, lakini leo mnataka kuichezea sharubu.

RC Chalamila, hotuba zako ni za kimamlaka, na hao waliogoma wanataka kuhatarisha usalama wa mkoa.

Ushauri kwa vyombo vya usalama: fuatilieni kwa kina mambo haya ya migomo pale Kariakoo. Nani anaanzisha movement hizi?

Anzeni na wale waliokuwa wakitoa kero kwa DC juzi, wale ndio wa kuanza nao. Wale mkiwapa kesi za uhujumu uchumi, hamtasikia tena upumbavu wa namna hii.

Asante, Mkuu wa Mkoa.

PIA SOMA
- Mgomo wa Wafanyabiashara ambapo Biashara zilifungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024.

- Chalamila kuwasili Kariakoo katika jitihada za kutatua mgogoro

- Baada ya Chalamila kuondoka Kariakoo, bado Wafanyabishara waliendeleza mgomo wa kufunga maduka.
Si tunaambiwa mmepita malengo ya ukusanyaji kodi? Sasa hiyo minyukano na walipa kodi imetoka wapi?
Mna upiga mwingi.
 
Hakika
 
Back
Top Bottom