Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mtaka atoa siku saba kwa wadanganyifu wa ardhi Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mtaka atoa siku saba kwa wadanganyifu wa ardhi Dodoma

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC), Anthony Mtaka ametoa siku saba kwa wakazi wa Msalato waliojiorodhesha kudai fidia ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato kwa njia ya udanganyifu kufika ofisi za Serikali ya Mtaa kuondoa majina hayo kwa hiari.

Mtaka ametoa agizo hilo Ijumaa Julai 22, 2022 wakati akizungumza kwenye mkutano na maafisa ardhi na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuhusu wimbi lililoibuka la Wananchi kuvamia maeneo ya Serikali.

Mtaka amesema kumeibuka wimbi la wananchi hao kutwaa maeneo ya ujenzi wa miundombinu ya Kitaifa ikiwemo barabara ya mzunguko (ringroad) na Uwanja wa Ndege wa Msalato kwa lengo la kudai fidia kinyume cha sheria.

"Kwa watakaotoa majina yao ndani ya siku saba wataruhusiwa kufanya hivyo bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria na kwa watakaokaidi agizo hili timu itafanya msako mkali kubaini wanaodanganya kuhusu zoezi hilo," amesema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema kwa watakaobainika kufanya ukaidi huo watahukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Pia, amesema kwa wakazi waliojenga kwenye hifadhi ya barabara ya mzunguko waondoe nyumba zao na maendelezo yoyote yaliyopo na atakayekaidi agizo hilo Serikali itabomoa nyumba zao na watalipa gharama za ubomoaji huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri amesema ili kujiepusha na migogoro hiyo ni vizuri wananchi kujiridhisha kuhusu ununuzi wa viwanja kupitia kwa mkurugenzi wa Jiji.

Shekimweri amesema uongozi wa wilaya hiyo hautasita kuendelea kubomoa maeneo yote yaliyojengwa kinyume na sheria kwa lengo la kujinufaisha kwa kundi fulani.

Aidha, amesema Serikali ya Mkoa imepanga kujizatiti kuboresha kitengo cha maununuzi wa viwanja na upimaji kwa njia ya Tehama ili kuondoa migogoro inayosababishwa na udanganyifu.
 
Screenshot_20220722-152256.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC), Anthony Mtaka ametoa siku saba kwa wakazi wa Msalato waliojiorodhesha kudai fidia ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato kwa njia ya udanganyifu kufika ofisi za Serikali ya Mtaa kuondoa majina hayo kwa hiari...
Ngoja waje CHADEMA a.k.a Mawakili njaa
 
Mambo ya ardhi Dodoma ni magumu,wangeyapima maeneo ijulikane ni mali ya nani na wapi.
 
Mambo ya ardhi Dodoma ni magumu,wangeyapima maeneo ijulikane ni mali ya nani na wapi.
Alimia kubwa wamepima,kilileta shida Dodoma hasa jiji KWa Sasa ulikua ukiritimba mkubwa wa CDA, wale wakubwa wao walijimilikosha maeneo makubwa na kujipatia hati, Sasa kimbembe ilikua KWa wananchi,
Badae ikavunjwa na ardhi ikawa chini ya jiji , wakaleta makampuni ya kupima, ila nao waliokua wanayafanya sight ni kichefuchefu, tutarajie migogoro huko mbele
Kama mh Mtaka ameanza kuona wenda matatizo mengine yanaania huko, akifanya ziara KILA kata hasa za jiji atakutana kero nyingi,
 
Naye tunajua ana kundi lake la kutaka ardhi ya taasisi za serikali kwa kutumia jina la mkuu wa mkoa. Ajisalimishe kabla hatujaanika mambo yake na usumbufu anaotoa kwa taasisis za serikali.
 
Nyuma yake kuna viongozi wa CCM maana ndiyo matapeli wakubwa, wao huwatanguliza wananchi mbele lakini kiuhalisia madiwani na viongozi wa CCM wapo nyuma ya hiyo migogoro.
 
Naye tunajua ana kundi lake la kutaka ardhi ya taasisi za serikali kwa kutumia jina la mkuu wa mkoa. Ajisalimishe kabla hatujaanika mambo yake na usumbufu anaotoa kwa taasisis za serikali.
CCM imejaa matapeli tupu hakuna mwenye unafuu, watengeneza migogoro ni viongozi wa CCM
 
Back
Top Bottom