Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti hizi chuki zako uwe pia unazionyesha hadi kwa Yanga SC na si Simba SC pekee

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti hizi chuki zako uwe pia unazionyesha hadi kwa Yanga SC na si Simba SC pekee

Raisi pekee Tanzania aliyejulikana timu gani ni Kikwete hadi kadi anayo..hii ya Magufuli ni kujitapatapa tu..hana hata kadi...Kagera anakufunga hadi Taifa ..aarrggghh kwa nini nimechangia mechi za mchangani
Kwani Yanga wana pointi ngapi Ligi Kuu ya Bara? Labda tuanzie hapo 😁😁😁
 
Sasa Timu ya Yanga hapa inaingiaje wakati kesho Ni Kagera sugar vs Simba/Mikia... Punguza Nyodo na wivu uliokukithiri.. Sisi Yanga tupo Zambia tunawaandaa Zesco tuwapapase vizuri..
"Mchonganishi Mfawidhi"
 
Rekebisha Yanga SC ilifungwa goli 1 tu na Ruvu Shooting ya Masau Bwire na siyo goli hizo 2 kama ulivyoandika hapa Ndugu.
Nasisitiza ni 2-0, na TFF ilimfungia kuchezesha mechi assistant referee aliyejaribu kusema goli la pili la Ruvu lilikuwa off-side
 
Duuu kumbe SIMBA mabigwa wa UCHAWI.Yaani umeandika utumbo balaa.
Hukuteuliwa na Rais JPM ili uwe unaikomoa tu Simba SC kila inapokuja huko Mkoani Kwako Kagera kucheza na Timu yako ya Kagera Sugar bali uliteuliwa ili uwe ' Fair ' kwa Wageni wote ambao watakuwa wanakuja huko. Halafu tambua pia kuwa huo Mkoa wa Kagera haukaliwi tu na wana Yanga SC wenzio bali hata wana Simba SC nao wapo na tena hata Kitakwimu tu wao ndiyo wengi ndani ya huo Mkoa wako.

Hii ni mara ya Pili sasa An Eagle Mimi nakufuatilia ambapo kila ukijua kuwa Timu ya Simba SC ( ambayo bahati nzuri hata Boss wako Mkuu aliyekuteua ndiyo Timu yake pendwa ) inakuja Kucheza huko na Kagera Sugar huwa unaibuka kama Zimwi au Jini na kuanza Kuwaahidi Wachezaji wa Kagera Sugar ' ahadi ' nyingi tu wakiifunga Simba SC ila ikija huko Timu yako pendwa ya Yanga SC huwa unanyamaza kama vile hujui kuwa ipo hapo Mkoani Kwako Kagera.

Labda leo nikukumbushe tu kuwa ' Upuuzi ' huu huu ambao leo unaufanya alianza Kuufanya mwana Yanga SC mwenzio Mbunge Mwigulu Nchemba alipokua Waziri na ni hapa hapa ' tulimuonya ' kuwa anachokifanya ' Kitamgharimu ' nafasi yake ya Uwaziri ambapo tulimshtakia hapa hapa JamiiForums kwa Mheshimiwa Rais na hatimaye ' akaliwa Kichwa ' na sasa anajutia.

Hivi nani hajui kuwa CDF Jenerali Mabeyo ni Yanga SC lia lia kabisa? Lakini je umeshawahi Kumuona akiutumia Ukuu wa Majeshi yake ' Kuinemeesha ' Yanga SC yake? Hivi unadhani kuwa ni Wewe tu ndiye mwenye Mahaba niue na Uchungu na Yanga SC kuliko Yeye? Na ulivyo Mnafiki hata Kauli zako ulizonukuliwa leo na Vyombo vya Habari japo umejifanya kuwa upo ' Neutral ' ila kuna moja ulijichanganya kisha Wadadisi na Wafukunyuzi ' Wabobezi ' wa mambo tukajua kuwa Wewe ni mwana Yanga SC haswa na una Chuki kubwa na ya Hatari na Simba SC.

Mwisho nakuambia mapema tu hata kabla Simba SC haijacheza na Kagera Sugar yako hiyo Alhamisi kuwa wape Hela za Kuroga ( Uchawi ) hao Kagera Sugar wako, andaeni kila aina ya Hila / Hujuma kwa Simba SC ila kaa ukijua kuwa Simba SC hasa Kamati yake ya Roho Mbaya ilishatangulia huko Siku nyingi sana na tukajua mbinu zenu zote hasa za ' Kiuchawi ' na kwa Kukuhakikishia hili angalia jinsi Simba SC itakavyotua ' Kimafia ' Kesho hapo Mkoani Kwako Kagera halafu kitafanyika nini hapo Uwanjani kwa nje na Simba SC ( hasa Gari la Wachezaji ) litapita njia gani na Siku ya Mchezo Kitu gani kitafanyika kabla ya Mechi ndipo utajua kuwa kwa Tanzania nzima hakuna Timu inayojua ' Fitna ' na ' Kuroga ' kama Simba SC.

Najua Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime ni Yanga SC Kindakindaki na kwamba kila akicheza na Simba SC ( Kupitia Kagera Sugar ) yake huwa anakuwa na ' Hirizi ' ambayo huiweka sana katika Mfuko wake wa Kushoto wa Suruali yake hivyo mwambie kuwa Siku ya Alhamisi aivae tena na Simba SC tusije Kulaumiwa kama ' Akifa ' pale Uwanjani kwani nakuambia kama kuna Mechi ambayo Simba SC na Kamati zake zote imejipanga nayo ndani na nje basi ni hii dhidi ya Kagera Sugar na ' Jini ' tulilolitumia sasa hata kama wakija Barcelona FC au Timu yangu pendwa Uingereza ya Liverpool FC inafungwa tu.

Badilika upesi na acha Uyanga wako na Chuki za wazi kwa Simba SC.
 
Hilo lingine labda ulipigwa wewe kitandani

1569488101826.png

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
1569487455309.png
 
Raisi pekee Tanzania aliyejulikana timu gani ni Kikwete hadi kadi anayo..hii ya Magufuli ni kujitapatapa tu..hana hata kadi...Kagera anakufunga hadi Taifa ..aarrggghh kwa nini nimechangia mechi za mchangani
kachangie mechi za ardhini,,,,
Sijaona kujitapa na wakati ni kilema
 
Nilivoona eti "hakuna Timu inayojua ' Fitna ' na ' Kuroga ' kama Simba SC.""
Nikajua uzi wako umekaa kipumbavu
 
kwahiyo mwaka huu viporo wanakula vyura fc baada ya mikia fc kuvimbiwa msimu ulipita hadi kupelekea kupigwa na UD songo
Ndiyo ligi yetu hii sijui tatizo wapi upande wa ratiba mbn epl,la liga na nyingne hawanaga jam ya mechi???
 
Back
Top Bottom