dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
Salaam Wakuu,
Nimeshangaa na sikuamini Kusikikia Stephen Kagaigai kabadilika kawa mbabe kiasi kwamba sasa hivi anawekwa kundi moja na Wakina Sabaya, Mnyeti. Huyu Mzee kabla ya kuwa Mkuu wa Mkoa, alikuwa Katibu wa Bunge akifanya kazi na Ndugai. Au ni Msongo wa Mawazo baada ya Kutolewa Kwenye ulaji Bungeni?
Watu wameshinda kesi, hukumu ipo, lakini anadai hakimu aliyehuku kesi ni Kanjanja. Hivyo eti akabatilishe hukumu, kwamba hawakupaswa kushinda. Sasa hivi anakata kila anayehusika kwenye hiyo kesi na kuwaweka ndani bila dhamana. Halafu anawaelekeza TAKUKURU wawafungulie kesi ya Uhujumu Uchumi. Anadai yeye ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa so Kwa Mamlaka yake anaweza kumuweka Korokoroni mtu yoyote. Anawatisha na kuwaweka ndani washindi waseme Mahakama imekosea wakati hukumu imetoka. Hivyo watu wanateswa ili waandike maelezo kwamba Mahakama imekosea. Mtu kashinda kesi, halafu unamlazimisha aseme hajashinda kesi au afunguliwe kesi ya Uhujumu Uchumi. Kama anaona uonevu, kwanini Wasikate rufaa kuliko kutesa watu?
Anachofanya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwenye suala la Wakili Edward Chuwa ni kuingilia uhuru wa Mahakama na upotoshaji. Mtu aliedai kushinda kesi ya ardhi na kutetewa na Wakili Chuwa katika kesi hiyo (Land Case No. 1 of 2018) katika Mahakama Kuu, Moshi kati ya Uru Shimbwe na wadaiwa wengine saba, Evarist Mushi alikuwa mdaiwa wa sita na katika kesi hiyo alishtakiwa tu na hakuwa na madai kinzani. Katika kesi hiyo, hukumu haikumtaja kupata ardhi yoyote wala nafuu yoyote kwenye kesi hiyo. Kwenye ukurasa wa tatu wa hukumu waliotajwa kushinda kesi na maeneo kubaki kwao ni mdaiwa 1, 2, 3, 4, 5, 7 na 8. Katika hukumu hiyo hakuna mahali mahakama ilisema ameongezewa kipande cha ardhi kama alivyodai Mkuu wa Mkoa. Wakili Chuwa alikanusha kuwa Evarist ni mteja wake na hakuna ushahidi kutoka kwa Evarist kuwa aliwahi kulipa hela ya uwakili kwenye madai ya takriban shilingi 7,640,000,000 (Bilioni Saba laki sita na arobaini).
Katika Kesi Na. 14 ya 2021 ya Baraza la Ardhi la Moshi, Bw. Chuwa alitamkwa kuwa mshindi wa eneo la ekari moja dhidi ya Evarist Mushi. Baada ya kutoka hukumu ya mahakama, amri ya kumtoa kwenye eneo ilitolewa kwa mujibu wa sheria na madalali wakateuliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu. Evarist amekata rufaa Mahakama Kuu, Moshi, Rufaa Na. 45 ya 2021 ambayo haijasikilizwa. Mkuu wa Mkoa ameingilia Mahakama kwa kutoa maamuzi kupingana na hukumu ya mahakama. Wiki iliyopita aliwaweka mahabusu Bwana Augustini Mushi (Mwenyekiti wa Mtaa), Hipoliti Makoi (Shahidi) na Patrisi Pantaleo (Shahidi) kwa siku tano bila haki ya dhamana. Tarehe 14/02/2022 alimuweka Wakili Chuwa mahabusu bila dhamana na tarehe 21/02/2022 akiongea na waandishi wa habari, Azam News na Kili FM aliamrisha vyombo vya usalama ikiwepo TAKUKURU kupekua sheria na kuhakikisha kuwa Bwana Chuwa anafunguliwa kesi ya Uhujumu uchumi, rushwa na mengineyo kama hatatengua hukumu hiyo mpaka Alhamis wiki hii na kumjengea nyumba Bw. Evarist. Bwana Chuwa ameitwa TAKUKURU Moshi na simu yake imezuiliwa.