Mkuu wa mkoa wa Mbeya aagiza kukamatwa kwa mkandarasi endapo atashindwa kusambaza kifusi katika barabara ya Mtaa wa Uzunguni A

Mkuu wa mkoa wa Mbeya aagiza kukamatwa kwa mkandarasi endapo atashindwa kusambaza kifusi katika barabara ya Mtaa wa Uzunguni A

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ameliagiza Jeshi la Polisi katika mkoani hapo kumkamata na kumweka ndani Mkandarasi anayejenga barabara ya Mtaa wa Uzunguni A Jirani na Mahakama ya Mwanzo endapo atashindwa kusambaza kifusi cha changarawe ambacho kimekuwepo maeneo hayo kwa muda mrefu.

Homera ametoa maagizo hayo leo Januari 13,2024 alipoitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kubaini kusua sua kwa mradihuo na kuweka bayana juu ya kutomalizika kwa miradi mingine inayotekelezwa na mkandarasi huyo ikiwemo barabara ya Usafwa inayotumiwa na Wananchi kupita.

Aidha amemtaka Meneja wa Wakala ya Barabara vijinini na mijini (TARURA) Mkoa
wa Mbeya Alberto Kindole kuleta barua ya maelezo ofsini kwake ndani ya siku saba ya kwanini hajahudhuria ziara hiyo.

Awali akitaja manufaa ya barabara hiyo Mwakilishi wa Meneja TARURA Mkoa wa Mbeya amesema mradi huo ukikamilika utachochea mafanikio ya kiuchumi, ajira na Kipato kwa Wananchi wa Jiji la Mbeya kadharika upungufu wa kuharibika kwa Vyombo vya Usafiri vitakavyotumia barabara hiyo.

 
Back
Top Bottom