Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

SASA HATA KAMA KAKA D ALIMSIMAMIA JK HARUSI NA SALMA [correct me if wrong]ndio ameamua KUINGILIA UHURU WA MAHAKAMA KWA KUPA HADHARANI KUPITIA LUHANJO TSH 500,000. NA KUWAMBIA WAANDIKE MAHITAJI YAO ILI WASAIDIWE.
SASA VIONGOZI WENGINE WOTE WAMEFUTIA NYUMA JINI HII LOWASSA,MEYA KIBISA,KANDORO NA WANAOFUATIA WANAPISHANA NYUMBANI KWA MAREHEMU WANAPELEKA PESA NA JK KASEMA AKIRUDI ASI ATAENDA TENA MWENYEWE.
WANASHERIA MNASEMAJE??? HII HAINGILII UHURU WA MAHAKAMA KAMA MKUU WA NCHI TAYARI AMEONYESHA WAZI INTEREST YAKE KWENYE SHAURI HILI ?? TUNAOMBA LEGAL OPINION.[ ADMINISTRATOR kama unaweza hii kuiwekea thread tofauti ] tnahisi tayari wafiwa wamelainishwa na haki huenda isitendeke.
 
Rais jakaya kikwete jana alimwagiza katibu mkuu wa rais ,ndugu luhanjo kuwasilisha tsh 500,000 kama pole,pia aliitaka familia ya ndugu mbonde iorodheshe mahitaji muhimu kwa misaada zaidi,pia ameahidi kuitembelea mara tu akirudi kutoka asia.pia luhanjo alitoa pole za mh.lowassa
wakati huhuo leo viongozi wa chama na serikali leo wameendelea kufika nyumbani hapo ,mh kandoro na meya wa jiji kimbisa wamewasilisha pole za mkoa wa dar es salaaam ,naye baba wa marehemu amesikika akisema ameridhishwa na misaada anayopata kwa viongozi ,na kusema kifo cha mwanaye ni kazi ya mungu na kusisitiza ushirikiano zaidi na familia.
[haya yote yanafanyika mbele ya kamera tvt ,itv [jana na leo,angalia website za magazeti ya tanzania]
familia imeridhika na inapata nafuu ya maisha kuliko hata mtoto wao [ambaye labda alikua day worker] alipokua hai ,na ilikua familia duni,,sasa na misaada hii watafuatilia tena haki kweli,,hata kama mlalamikaji ni jamuhuri,si anategemea ushahidi wa ndugu na waliokuwepo.,,silaha haionekani,,na hatujui kama postmortem report ipo,na inasema mbonde alikufa kwa kitu gani,,,hakimu anabase kwenye ushahidi usiokua na mashaka...manasemaje wataalamu?
 
Ukweli wa mambo ni kwamba tutashuhudia Ushahidi wa uongo kwenye kesi nzima ya Bwana Mzuzuri Vs Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mimi binafsi nilianza kupata wasiwasi toka siku ya kwanza ya tukio.kwa sababu taarifa za tukio zilikuwa zinatofautiana mno.Kama nipo sahihi tukio la mauaji lilitokea siku ya Ijumaa usiku (kati ya saa moja mpaka saa mbili na nusu).Gwaride la Utambulisho (Identification parade) lilifanyika Jumamosi jioni.Sasa wasiwasi wangu ni kwamba kipindi chote cha masaa yasiyopungua 17 kulikuwa na mikutano kati ya Mzuzuri,Tibaigana na hata Rais au vyombo vya sheria ili kujua hatima yake.Kama mtakumbuka hapo awali tulifahamishwa kuwa Mzuzuri alikamatwa muda kidogo baada ya tukio,lakini baadaye vyombo hivyo hivyo vya habari vilitutaarifu kuwa Ditopile alijisalimisha kwa Bw.Tibaigana.
Bila uoga hapa nadiriki kusema kuwa Bastola imepotezwa na hao viongozi wa polisi na pia Ditopile hakuumia ule mkono aliofunga bandage,ile ilikuwa ni janja yao ya kutaka Mzuzuri apewe matibabu nje ya jela.
Sasa wanatoa pesa za pole ili kumnunua mzee wa Mbonde,Mzee huyu na familia yake ni maskini watamuuza marehemu kwa bei nafuu mno labda hata pungufu ya Tshs 1,000,000,na itapelekea kutoa shukran kwa serikali na kupunguza uzito wa kesi.Tutashuhudia Mzee akisema msifanye upelelezi kwani mtakuwa mnaingilia kazi ya Mungu,na kuingiza maneno ya kiungwana ya "aliyeleta ndio ametwaa".
 
Vijana haya mazingaombwe yameanza hayo, hivi rais JK kutoa hela kwa familia ya marehemu ilibidi itangazwe? Mungu si anasema kuwa ukishatangaza tu basi umeondoa baraka yake maana sasa unakuwa sawa na mafarisayo wanaopenda kujitangaza,

Mungu anasema kuwa mkono wa kushoto, usijue wa kulia umefanya nini? Hayooooooooo! mazingaombwe yanakuja, ila leo nimeongea na kiongozi mmoja wa bongo akaniambia kijana Ditopile yuko keko hiyo ninakuhakikishia mwenyewe na leo ninaenda kumuona,

kwa hiyo ni for sure kuwa braza Dito, yuko kweli lupango, maana mimi ninavyoijua bongo hata hiyo nilikuwa siamini, lakini ndugu zangu sasa ndio wameanza, kwanza walinyamaza kimyaaaaa, walikuwa wanaongea kwa milango ya nyuma, sasa tayari wameshaambiwa namna ya kuicheza hiii ngoma na ndio wameanza, sasa na hela kwa familia ya marehemu!, sasa subirini next.........?

Halafu hongera kwa wale waliobeba mabango kwenye mazishi ya marehemu maana viongozi wa bongo hiyo imewakuna kweli wote wanaiongelea hiyo, sasa ninawaambieni wananchi wenzangu hapa forum, jamani tukinyamaza tuu wallahi huyu braza Dito anatoka!

Wallahi nina miambieni, tukinyamaza huyu mzee anaondoka tena bila ya ubishi lazima tuendelee kupiga kelele hao mawakili wake njaa hao waende zao, Ditopile ni kiongozi tena wa siasa na wa serikali, kwa hiyo kama alivyosema Clinton ni public figure, kwa hiyo kumuongelea ni fair game,

uongozi wa wananchi ni responsibility inayokuja na priviledges ambazo wananchi wengine hawana, ndio maana sisi wote sio viongozi, somebody had to be our leader na in this case ni Ditopile, sasa ukiichezea hizo priviledges, wewe lazima uwe mfano kwa wananchi, ndio maana wananchi wakiwa na wasi wasi na system yao ya sheria waliyoiona ikimuachia Rupia, Kingunge, na sasa Mungai, ni lazima waaznze kuonyesha wasi wasi wao mapema!

Na hasa tunaposikia kuwa bastola imepotea, na kwamba ati hakuuwa kwa makusudi, na kwamba ati ".........katika process ya kugombana na dereva aliumia mkono.....", a NONESENSE ya kumpa fursa ya kutumia muda mwingi kwenye wodi ya Muhimbili badala ya kula mandondo Keko!
 
Hakuna kosa kwa JK kutoa rambirambi kwa wafiwa. JK ni mkuu wa kazi wa mtuhumiwa. Mfanyakazi wa kampuni (eg. dereva) akiua ni kawaida kwa kampuni kutoa fedha za ubani. Serikali ndiyo kama kampuni kwenye kifo hiki.

Mrema naye alitoa fedha za rambi rambi (tunasikia ni laki). Hapo kulikuwa na kutumia msiba kisiasa, na JK kutoa rambi rambi wazi wazi ni sehemu ya siasa zinazoandamana na mkuu serikalini kuua mlalahoi.

Kutoa rambi rambi hakuingilii mahakama hata kidogo. Tusimame kwenye logic inayoeleweka jamani. Sisemi kwamba haki haiwezi isitendeke. Na kwa maoni yangu, tayari mfumo uliotumika mahakamani haukuwa wa haki.

Kwa kawaida, mtuhumiwa alitakiwa aletwe toka aliposhikiliwa (mahabusu), na arudishwe chini ya ulinzi wa polisi. Si sawa mwendesha mashtaka kukubali dai la wakili wa mtuhumiwa kwamba "aende kwa daktari". Kuna tofauti kati ya "kwenda kwa daktari" na kwenda "hospitali". Ilitakiwa mtuhumiwa apelekwe hospitali na polisi, na kama hakulazwa, au siku anatoka, aingie kwenye gari la polisi na aende jela kama watuhumiwa wengine.

Kwa kawaida, kesi za mauaji Tanzania huchukua miaka 10. Na kipindi chote mtuhumiwa anakuwa jela. Haitakuwa haki mtuhumiwa huyu wa sasa aharakishiwe kesi yake zaidi ya watuhumiwa wengine.

Wafiwa hawawezi kufuta kesi, kwani sio kesi ya madai. Acheni kusema kwamba kuwapa wafiwa fedha kutayumbisha kesi. Mashahidi wa msingi ni abiria waliokuwa kwenye daladala, na sio wazazi wa marehemu.

Augustine Moshi
 
augustine yako timeyasikia,,,,,,unaweza kuua mtu kama una pesa ukaitunza familia yake na angalau isionekane dhambi,,,,,ndio un"gombe huu ndio uewaweka huru kina kinje na wengine,,,wenje nazo.
hatukatai jk kutoa msaada mbele ya kamera,,,tunakataa rais wa jamhuri ya mungano na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,[mwenye mamlaka ya kuchagua majaji na kwasimamamisha kazi[si kufukuza,wanafukuzwa baada ya tume ya majaji wa jumuia ya madola kupendekeza,,if i am right] kuwa mkuu wa nchi tayari ameonyesha hadhrani antaka nini hapa,,ingekua fununu au ametoa kwa siri kama sadaka hakuna ambaye angelalama,,,katenda haya hadharani,na viongozi wanaomfuatia nao wanapangana kwenye foleni ya kutua...sasa??
 
Hakuna aliyemkataza kutoa pesa kwa familia ya marehemu, lakini why makelele? Mzee Moshi vipi bro? Wewe si una dini je dini yako inasema upige kelele unapotoa msaada? Bahkressa anatoa misaada mingi sana lakini umewahi kuisikia kwenye public?

Nia na madhumuni ya rais wa jamhuri kumtumia pesa familia ya marehemu, na kutangaza hadharani maana yake ni nini wakati huu mgumu wa kesi ya Ditoile ya kumuuua dereva asiyekuwa na hatia?

Gavana wa mkoa ameua mwananchi bila ya sababu kama kuku, gavana aliyechaguliwa na rais, gavana yuko rumande kusubiri kesi ya mahakama, leo rais anaenda na kutoa hela kwa familia ya marehemu, na kutangaza public yaani wananchi wengine, sasa viongozi karibu wote wanaanza kujipanga public kujionyesha kuwa wana huruma na familia ya marehemu, wiki moja baada ya marehemu kuuliwa na kuzikwa wakiwa kimyaaaaaaa!

Halafu leo wewe unasema hakuna tatizo hapo, mzee Moshi vipi mbona uko naive mno bro?

Bastola aliyoonekana akiitumia na public haionekani? Ditopile anakuja mahakamani na Saloon? Amefungwa mkono bandeji na kutumia muda mwingi eti Hospitalini? Rais huyo aliyetoa mapesa hawezi kusema lolote kuhusu the act, maana ungetegemea by now awe ametoa msimamo wake rasmi, kuwa anakilaaani hicho kitendo ambacho kimesababisha raia kupoteza maisha ingawa ataiachia mahakama iamue kama kuna kuvunjwa sheria, lakini angesema ameguswa na kitendo hichi cha kinyama, na ameamua kutoa hela kwa marehemu na anaaahidi kuhudhuria vikao vya kesi hiyo kuona haki ya marehemu inatendeka na familia yake, au ataifatilia kwa makini kesi hiyo kuona mwisho wake, NO! that is not the case, hebu Moshi tuambie je angeuwa kiongozi wa upinzani rais na CCM wangesema nini? wangetoa hela kwa familia ya marehemu basi?

Jamani kwa wwale msiokielewa hiki kiiini macho hebu kaeni pembeni, and I mean it, hii sio siasa as usual NO! kuna maisha ya raia asiyekuwa na hatia ambayo yamepotezwa hapa, na tunataka precedent hapa, yaani mfano kwa ajili ya our future legal system namna ya ku-deal na viongozi wahalifu,

just simply put, ni kwamba tumechoka na huu mchezo wa kina Rupia, Kingunge, na Mungai,

ninarudia asiyeelewa kinachoendelea akae pembeni, and I am dead serious!, kwenye hili tunataka kusikia neno moja kuwa sheria ifuate mkondo na mimi kama rais wa jamhuri nitahakikisha kuwa hilo linatendeka maana tumo katika mazingira ambayo wananchi tayari wanayatilia mashaka kutokana na history!
 
Ni vizuri ieleweke kuwa Tsh 500,000 zimetolea na Ikulu, ndiyo maana Bwana Luhanjo ameziwakilish kwa niaba ya mzee. Kwa hiyo kusema kuwa JK ana haki ya kutoa rambirambi siyo sahihi kama anatumia pesa ya Iklulu. Ingawa najua kuwa Sh500,000 na kitumbua tu kwa JK, kitendo cha pesa hizo kupelekwa na bwana Luhanjo kimeainisha kuwa rambirambi hiyo ni ya Ikulu siyo ya JK binafsi. Kama ingekuwa rambirambi binafsi ya JK, aidha angemtuma Luhanjo privately kama rafiki ambaye angekwenda msibani baada ya saa za kazi na asingepigwa picha magazetini au angemtumia ndugu yake yeoyote ambaye hayuko serikalini.

Kitendo cha maofisa wa serikali kuanza kujaa nyumbani kwa marehemu baada ya mazishi ni unafiki tu. Wakati wa mazishi tuliona makonda wakiomba misaada barabarani na hakuna ofisa wa serikili ayesaidia na leo baada ya mazishi kufanyika ndio wamegundua kuwa walitakiwa wasaidie gharama za mazishi. Jamani hamuoni kabisa kuwa huo ni unafiki wa wazi kabisa.

Wakati wa Mazishi ya mtoto wa Capt Mazula tuliona viongozi wote wakijipanga kuanzia eapoti, lakini wakati wa mazishi ya marahemu mbone aliyeuwawa na ofisa wa serikali kiasi kuwa mazishi hayo yaliigusa serikali moja kwa moja hatukuona kiongozi yeyote wa kiserikalia mpaka pale walipomaliaza kutafakari future ywa mwenzao Ditopile ndipo wakagundua kuwa kuna maiti ya mlalahoi mmoja iliyotakiwa kuzikwa.
 
well said Kichuguu; especially the last two paragraphs.

Habari za michango kwa familia ya marehemu zimefikia wapi? I would like to contribute also.
 
Naungana na waheshimiwa hapa chini... Tulipoanza kutoa hoja hii ya kuchanga ndio tumeoona msululu wa viongozi kuchanga.

Kama kweli walikuwa na huruma hizo basi wangetokea siku ya mazishi kama alivyofanya Mrema...
Issue hii sasa hivi imekuwa Politics na kama kweli wanataka kuisaidia familia ya marehemu, hao waandishi wa habari wanakuja kufanya nini?..
Mchango umetolewa Ikulu kwa baba wa marehemu ya nini zipigwe picha na kutangazwa!.
Tunamsubiri ndugu yetu Mzee Mwanakijiji atuunganishe...
 
Kinachofanyika ni ku-diverge attention ya wananchi kwenye suala la Dito kuua. Sasa hivi maongezi yataanza kuwa ooh Rais huyu mzuri sana katoa msaada wa laki tano, halafu sisi tulivyowasanii tutaanza kusema oh angezitoa wapi hizo laki tano. So, kuna implication kubwa sana katika hili. Kubwa ni kwamba hii kesi ianze kusaulika. And who knows kwamba Dito yupo Keko kweli ukizingatia kuwa aliondoka kwenye saloon yenye vyoo tinted!
 
Mwanasiasa,
Unataka kusema Dito huletwa mahakamani na gari la mtu binafsi?.. maana hiyo saloon tinted siipati bado!..
 
Mkandara,
Mwanasiasa ana maana kwamba Dito hakupanda Karandinga. It was a private saloon.
 
Mkandara,

Blaza Dito aliletwa na gari la Saloon, na siyo ngarandinga, na mpaka leo hakiuna maelezo kamili ile Saloon ni ya nani, na ilipotoka pale ilienda wapi? Waandishi wamekuwa mabubu ghafla bin vuuuu!
 
Loooh tumekwisha, halafu watu wanasema tuache sheria itachukua mkondo wake?... damn!
 
Je watu wanajua gereza alilowekwa Brother Dito? Ninataka kwenda kumtembelea na kumpa pole kama raia wake mwenyeji wa Tabora kutoka Isevya. Kabla ya kuvuluiwa madaraka yake alikuwa mtawala wangu.
 
Mzee Es,
Ikiwa huyu Dito yuko Keko inakuwaje anaingia kortini na saloon car!... au ndio special security kama anayofanyiwa Saadam!..unajua tena ktk hadithi za high profile case wanavyozitafutia sababu.
Hata hilo la Keko nina mashaka sana!... vipi dhamana yake imefika wapi?
 
Nilivyosoma kwenye magazeti ni kwamba hakimu alikubali hoja ya wakili wa mtuhumiwa, hoja iliyoungwa mkono na mwendesha mashtaka, kwamba mtuhumiwa apelekwe kwa daktari. Sasa daktari anaweza kuamuru mgonjwa wake akae nyumbani kwake, au kwenye hospitali yake, au hata hotelini. Cha muhimu ni kwamba anakuwa kwa daktari kama alivyoagiza hakimu.

Mzee ES, naomba nijibu angalau baadhi ya hoja zako. Zingatia ukweli kwamba kiongozi akiua mlalahoi kunakuweko na hali ya siasa. Mchakamchaka waliokimbia vijana wakati mwili wa marehemu unaoshwa ulikuwa ni mchakamchaka wa kisiasa.

Rais, kama mkuu wa kazi wa mtuhumiwa, anapashwa kushughulikia vipengele vya kisiasa vilivyojitokeza. Hii ni pamoja na kuujulisha umma kwamba atasaidia familia iliyoachwa. Angetoa mchango kimya kimya haingetosha.

Umma una hakika kwamba mtuhumiwa alimuua marehemu. Ulikuwepo umma kwenye tukio. Mwajiri wa mtuhumiwa anapashwa kushughulikia, mbele ya umma, utunzaji wa watoto wa wafiwa. Itabidi serikali isomeshe watoto wa marehemu hadi chuo kikuu.

Nikirudi kwenye swali ulilouliza la bastola kupotea, naomba nikujibu hivi: Magazeti yanasema mtuhumiwa alishambuliwa na baadhi ya waliokuwa kwenye basi. Wakati wa vurugu hizo, inawezekana kabisa mtu kuibiwa fedha na hata bastola. Bila shaka walimnyanganya bastola kabla ya kumpiga, na sidhani kama baadaye wangemrudishia. Au wewe ungempiga konzi mtu aliyeshikilia bastola mkononi bado? (Na ambaye ndio amemaliza tu kufyatulia mtu risasi?)

Umeuliza vile vile kama mtuhumiwa angekuwa kiongozi wa upinzani, Rais angetoa fedha? Anabidika kutoa fedha kulipia madhara yanayofanywa na waajiriwa wake tu. Na ni sawa ziwe fedha za serikali kwani hii sio shughuli binafsi. Ni shughuli ya kutuliza zisitokee vurugu.

Mpo wengi mnaolaani kitendo cha maofisa wa serikali kufika kwa mfiwa baada ya mazishi. Ni kwa usalama. Nasikia vijana marafiki wa mfiwa walikuwa wamekasirika wakati wa mazishi, kiasi cha kupiga hata wanajeshi. Wangewaona viongozi wenzake na mtuhumiwa wakati huo wa kupandisha mori si wangewaua kabisa?

Ni wajibu kwenda kuomboleza mahali ambako mfanyakazi mwezako alisababisha janga. Unaenda kutoa pole, na kwa kweli ni kama kwenda kuomba msamaha kwa niaba yake. Sio msamaha wa kutaka kufutwa kesi, kwani sio kesi ya madai, ni msamaha unaoombwa toka rohoni.

Augustine Moshi
 
augustino...it seems you ca make a good defence lawyer..for muhashimiwa ditopille,,,acha sisi wadanganyika tuendelee kumtetea mkeshahoi...although tunajua familia yake imeshalainika but mahakama ndio itakayoamua...rule of law is what we want to see.
 
Back
Top Bottom