Vijana haya mazingaombwe yameanza hayo, hivi rais JK kutoa hela kwa familia ya marehemu ilibidi itangazwe? Mungu si anasema kuwa ukishatangaza tu basi umeondoa baraka yake maana sasa unakuwa sawa na mafarisayo wanaopenda kujitangaza,
Mungu anasema kuwa mkono wa kushoto, usijue wa kulia umefanya nini? Hayooooooooo! mazingaombwe yanakuja, ila leo nimeongea na kiongozi mmoja wa bongo akaniambia kijana Ditopile yuko keko hiyo ninakuhakikishia mwenyewe na leo ninaenda kumuona,
kwa hiyo ni for sure kuwa braza Dito, yuko kweli lupango, maana mimi ninavyoijua bongo hata hiyo nilikuwa siamini, lakini ndugu zangu sasa ndio wameanza, kwanza walinyamaza kimyaaaaa, walikuwa wanaongea kwa milango ya nyuma, sasa tayari wameshaambiwa namna ya kuicheza hiii ngoma na ndio wameanza, sasa na hela kwa familia ya marehemu!, sasa subirini next.........?
Halafu hongera kwa wale waliobeba mabango kwenye mazishi ya marehemu maana viongozi wa bongo hiyo imewakuna kweli wote wanaiongelea hiyo, sasa ninawaambieni wananchi wenzangu hapa forum, jamani tukinyamaza tuu wallahi huyu braza Dito anatoka!
Wallahi nina miambieni, tukinyamaza huyu mzee anaondoka tena bila ya ubishi lazima tuendelee kupiga kelele hao mawakili wake njaa hao waende zao, Ditopile ni kiongozi tena wa siasa na wa serikali, kwa hiyo kama alivyosema Clinton ni public figure, kwa hiyo kumuongelea ni fair game,
uongozi wa wananchi ni responsibility inayokuja na priviledges ambazo wananchi wengine hawana, ndio maana sisi wote sio viongozi, somebody had to be our leader na in this case ni Ditopile, sasa ukiichezea hizo priviledges, wewe lazima uwe mfano kwa wananchi, ndio maana wananchi wakiwa na wasi wasi na system yao ya sheria waliyoiona ikimuachia Rupia, Kingunge, na sasa Mungai, ni lazima waaznze kuonyesha wasi wasi wao mapema!
Na hasa tunaposikia kuwa bastola imepotea, na kwamba ati hakuuwa kwa makusudi, na kwamba ati ".........katika process ya kugombana na dereva aliumia mkono.....", a NONESENSE ya kumpa fursa ya kutumia muda mwingi kwenye wodi ya Muhimbili badala ya kula mandondo Keko!